TCRA amkeni saidieni kupata simu zinapoibiwa

Tyetyetye

JF-Expert Member
Dec 3, 2014
1,026
780
Watanzania tulikuwa tunapigwa kwa kuuziwa simu fake lakini TCRA walikaa kimya mpaka tulipokuwa taabani wakaja na jibu kuwa fake sasa basi.

Leo hii tunaibiwa simu kila siku TCRA wako kimya kama vile hawapo.

Nina namba ya EMEI ya simu yangu iliyoibiwa na siku ilipoibiwa na mtu aliyeiiba. Mwizi huyo aliniibia SAMSUNG GALAXY NOTE 4 akaiuza kwa shilling laki moja.

Mwizi anachofanya ni kujificha tu ili POLICE wasimkamate. TCRA saidieni watu wanapata hasara kwa kupoteza simu zao.
 
Mwenyewe nilishapigwa simu zangu, IMEI ninazo nimehangaika polisi lakn mpaka leo nimekata tamaa, ni bora wangeweka utaratibu hata wa kwenye website kama tulivyokuwa tunaangalia kwa kuweka IMEI namba na kuoneshwa kama ni simu feki au la, wangeweka utaratibu huo ili unapoibiwa tu unaingiza IMEI namba yako unapewa namba ya simu inayotumia simu yako kwa muda huo, ingesaidia kuwapata wezi kwa urahisi
 
May b wanasubiri tamko toka juu
Ila sio siri hawafanyi kazi yao kwa ufanisi kutuhudumia wananchi kama wameshindwa wabinafsishe tu isije kujifia kama TTCL pale
 
Nenda kamata aliyenunua ukiwa na polisi toa risiti nae ataulizwa risiti atakua hana kubalianeni alipe garama pamoja na yeye kumtafuta aliyemuuzia .

Aliyekamatwa na ngozi ndo mlanyama
 
Watanzania tulikuwa tunapigwa kwa kuuziwa simu fake lakini TCRA walikaa kimya mpaka tulipokuwa taabani wakaja na jibu kuwa fake sasa basi.

Leo hii tunaibiwa simu kila siku TCRA wako kimya kama vile hawapo.

Nina namba ya EMEI ya simu yangu iliyoibiwa na siku ilipoibiwa na mtu aliyeiiba. Mwizi huyo aliniibia SAMSUNG GALAXY NOTE 4 akaiuza kwa shilling laki moja.

Mwizi anachofanya ni kujificha tu ili POLICE wasimkamate. TCRA saidieni watu wanapata hasara kwa kupoteza simu zao.
Kwa hiyo ulitoa taarifa kituoni na wakakujibu vipi baada ya kutoa hizo taarifa? TCRA hawawezi ku handle kesi moja moja mkuu kama hivyo. Kwa hiyo wa kuwalaumu ni polisi kwa kutolishughulikia suala lako na si TCRA. Polisi ndo wanapaswa waamue kama suala lako linawahitaji polisi ama la
 
pole sana mkuu...
kama mwizi ni mwepesi hata TCRA wanaweza wasimpate maana akii "upgrade" tu EMEI inachange..
ukiacha hiyo kuna alternatives kibao za kuchange IMEI mkuu..
 
Back
Top Bottom