TBC1 wamdhihaki Dk Slaa Mkutano wa Mabibo na wanavyuo ktk kipindi cha Fataki la wiki

Inatia uchungu kuona TBC aliyoijenga Tido Mhando kugeuka kuwa Kinyago. Mimi toka wamtose Tido sijaangalia TCB1. Jamani hata matangazo msipeleke huko tena wapeleke CCM na IKULU (Matangazo ya Mkopo)
 
Hata hawa ccm watumie tv au radio; na magazeti bado mimi nasema ccm ni mafisadi tu, kumbukeni wakati wa uchaguzi walitumia radio, tv, magazeti, mabango makubwa sana, helikopta, magari na bado hata greengard bado maji yaliwazidi hadi shingoni mpaka ikabidi watumie uchakachuaji wa matokeo.

Cha msingi tupiganie na tuseme sana hata kwa kelele kali juu ya hii katiba mpya pamoja na mambo mengine tume ya uchaguzi itayotenda haki ni muhimu sana. Ccm iondolewe chama kingine kishike hatamu, najua taifa hili litabadirika tu. Hata hivyo vyombo vya habari vitatangaza mambo yatakayowavutia wananchi na siyo ya kitapeli na kinafiki kama hivi sasa.
 
Mkuu kama kusema umesema! Kusikia kwetu ndio kudogo! Kuelewa kwetu kunachukua muda! Tunashtaki kwa wafadhili ili watuondolee miba njiani kwa maana hatuna viatu! Tunalalamika kwa sababu tunahitaji wengine wajue kwamba tunalalamika! Na mwisho wa siku wakishajua kwamba tunalalamika watuite WALALAMISHI! sijui nani tena atatusikiliza hapo! Napenda kuongezea pale na hapo, Siasa za nchi hii watu wanafuata watu na hawafuati vyama. Kwa ibada hizi za kuwaabudu watu wasisemwe, inamaanisha kwamba watu wanawaangalia watu na si vyama!! ikiwa leo Dr. Slaa atahama Chadema kwenda CCM sijui hali itakuwaje? Nashangaa sana watu hatujifunzi toka enzi za kina Mrema na Marando? Nini kilitokea na nini kilifuatia. Ikiwa kweli tunajali basi na TUJENGE VYAMA SI WATU! Tukiwajenga watu vyama vitaendelea kubaki dhaifu. na kwa mujibu huo CHAMA KITUKANWE MFALME ASIGUSWE!
 
Kweli ccm wako kwenye usingizi mzito. Zama hizi si za kulipa watu aina ya Tambwe kwa kazi isiyo na tija. Hivi hawa vilaza wa tbc wanajua kuwa hawapaswi kujifungamanisha na chama chochote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…