TBC kwa nini mnapiga mziki tu usiku!

TBC kwa nini mnapiga mziki tu usiku!

King Octavian

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2011
Posts
403
Reaction score
353
Jamani mimi hili jambo linanikera sana kwa hii televisheni yetu ya Taifa kwa upande wa vipindi vyake kuanzia saa5 usiku. yaan wanapiga tu music, hivi kweli televisheni ya taifa inayoendeshwa kwa kodi za wananchi wanashindwa kuwa creative kutafuta vipindi vikarushwa muda huo, basi waweke hata mikanda ya wanyama wapromote utalii, TBC2 music ukienda TBC1 music what is this, tafutane hata documentary muwe mnaweka mbona zipo nyingi zenye kufunza. mfano ikitokea msiba wa taifa ambao utaradhimu bendera kushushwa nusu mlingoti eehee usiku mtapiga music? au mtazima mitambo?
 
Media zetu baaado sana si wao tu Dtv wao kutwa nzima usiku kucha ni bongo flava...udhaifu mkubwa kwa tvs station nyingi tu hapa kwetu hata redio!taarifa ya habari radio one habari za taifa dkka 3?wanashindwa hata na ki redio station kidogo cha WAPO FM jamaa wana ma reporter nchi nzima!hadi vijijini!sikiliza patapata asbuhi ni kama ume tune Bbc swahili!we utakuja ona Azam tv itawapiga bao wengi!Tv hazina habari?wanatuunganisha na tvs za nje muda mwingi!au tamthriya za kigeni kutwa su nigerian movies!wakati kuna mengi ya kuonyesha/kuelimisha/burudani humuhumu lkn waandishi wetu hawaoni hayo!clouds tv/radio wao ni watu wa kutangaza biashara tu!za kuwanufaisha wao na si jamii!wanajitia changamkia fursa...mpira kuoneshwa wa tanzania ni mbinde bora waweke nigerian movie au isifingo mpira titaendelea kweli?
 
Jamani mimi hili jambo linanikera sana kwa hii televisheni yetu ya Taifa kwa upande wa vipindi vyake kuanzia saa5 usiku. yaan wanapiga tu music, hivi kweli televisheni ya taifa inayoendeshwa kwa kodi za wananchi wanashindwa kuwa creative kutafuta vipindi vikarushwa muda huo, basi waweke hata mikanda ya wanyama wapromote utalii, TBC2 music ukienda TBC1 music what is this, tafutane hata documentary muwe mnaweka mbona zipo nyingi zenye kufunza. mfano ikitokea msiba wa taifa ambao utaradhimu bendera kushushwa nusu mlingoti eehee usiku mtapiga music? au mtazima mitambo?

Anytime unapoajiri watoto wa shanganzi, mjomba, dada, kaka, lazima ufanisi unakuwa mdogo. Hii TV kwa kweli ni janga na ni haibu sana kuiita ya taifa. Utashangaa viongozi wapo na wanaona haya ila kimyaaaaaaaa!
 
Tbc ni upuuzi mtupu kwanza upatikanaji wake ni wa taabu hasa kwa watumiaji wa dishi yaani bora utafute tv za mozambique utazipata, pili vipindi vya kipuuzi wanashindwa kunyesha hata documentary za kawaida kama za kilimo, tatu kimekuwa ni kijiwe cha mafisadi wachache mfano mkurugenzi anakaa mbele ya waandishi anaropoka hatutaonesha mpira kwenye tbc 1 ili tuuze ving'amuz vya star times wakati hela ya kulipia hizo mechi imetokana na kodi za wananchi
 
Back
Top Bottom