POSHO MAVYEO
JF-Expert Member
- Jun 28, 2011
- 371
- 112
WAZIRI wa Fedha, Dk.William Mgimwa, amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya Sh 1,000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu ya kiganjani. Alisema serikali inaendelea kupokea maoni kuhusiana na suala hilo.
Dk. Mgimwa alisema jana kuwa tangu itolewe kauli hiyo yamekuwapo manung'uniko mengi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo watumiaji wa mitandao ya simu.
Alisema serikali haikuwa na nia mbaya isipokuwa ililenga kuboresha na kuongeza ukusanyaji wa kodi na kukuza uchumi nchini.
"Watumiaji watakuwa wanakatwa Sh33.35 kwa kutwa nzima ambayo ni sawa na Sh 100 kwa siku tatu, hatua itakayosaidia kuboresha maeneo mengine ya kukuza uchumi," alisema.
Alisema tozo hiyo ililenga kupatikana Sh bilioni 160 kwa ajili ya kuendeleza na kuimarisha miundombinu ya barabara vijijini, maji na umeme. http://www.mtanzania.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=8340:dk-mgimwa-zungumzia-tozo-ya-sh-1000-simu-za-mkononi&catid=8:siasa&Itemid=57
Soma hapa chini mkuu...
Wamiliki wa simu kutozwa 14.5%
Hiyo ndio habari nilikua nimeigusia pale awali...
hahahahaha..umeona eeh..halafu leo hii wanakataa wakati walikaa na kupitishaWatu wapo kazini wanatafuta fedha za kuonga kwenye kampeni kuikataa rasimu ya katiba, uchaguzi 2014 na 2015
Huu usanii una hatari zakehahahahaha..umeona eeh..halafu leo hii wanakataa wakati walikaa na kupitisha
Siyo elfu 36 tuu. Ukitumia M-Pesa au benki yako kuhamisha zaidi ya sh. 30,000 utakatwa kodi pia: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/489275-kodi-mpya-barua-ya-tra-kwenda-kwa-mabenki.html
mkuu jana nimetoa m-pesa 50000 nikashaangaa nimebakiwa 447800 kwasababu nilikua na sh 500000 ktk m-pesa yangu, kwa mantiki hiyo sh 50000 inakatwa 2200 kitu ambacho before hakikua hivyo cuz gharama yake ingekuwa ni sh 1000 tu, sasa hivi wameamua kutumaliza watu wa chini kabisa, hizi m-pesa, tigo-pesa nk zimeshakuwa ni mzigo tena, sijui tunaelekea wapi na hii sekta yetu ya mawasiliano?sijui kama wamefanya ka utafiti lau kadogo kutizama impact ya kitu walichokianzisha au wamekurupuka as usual
mkuu ata mimi nimeshangaa sana nafikiri kuanza kutumia tena mfumo wa kibenki kama zamani cuz hizi gharama siwezi kuzimudu kwa sasa, maisha yatazidi kuwa magumu sana huku tunakoelekea cuz wanaotakiwa kulipa kodi stahiki hawalipi wanazidi kukimbiza na sisi mafukara.Mbona wanachukuwa pesa nyingi sana ?!! hiyo hela ni ndefu kweli wanachukuwa ya nini? haya mambo ya kibank sio kufanya hivyo
Hiyo ni kodi tofauti na hiyo ya bank kwneye barua
Mbona wanachukuwa pesa nyingi sana ?!! hiyo hela ni ndefu kweli wanachukuwa ya nini? haya mambo ya kibank sio kufanya hivyo
mkuu ata mimi nimeshangaa sana nafikiri kuanza kutumia tena mfumo wa kibenki kama zamani cuz hizi gharama siwezi kuzimudu kwa sasa, maisha yatazidi kuwa magumu sana huku tunakoelekea cuz wanaotakiwa kulipa kodi stahiki hawalipi wanazidi kukimbiza na sisi mafukara.
WAMILIKI WA SIMU KUTOZWA 14.5% KUCHANGIA ELIMU TANZANIA. JE MDAU HII IMEKAA SAWA?Soma hapa chini mkuu...
Wamiliki wa simu kutozwa 14.5%
Hiyo ndio habari nilikua nimeigusia pale awali...
kwahio it means hio ya vifurushi kupanda kwa kiasi cha tshs 100 na bundles kupanda kwenye net ni kodi walizopigwa wenye makampuni nao hawakufanya ajizi bali kumsukumia mtumiaji ?, Duh all in all mi naona ni vema tukapata clarification zaidi juu ya hizo kodi nyingine pia, kama ni kweli vifurushi vimepanda sababu ya hizi kodi au hizi kampuni nazo zimepata fursa ya kutukamua
huenda ikawa ni hio lakini zile bundles lets say kifurushi cha tshs 500/= (14.5% ingebidi iwe tshs 72.5 na sio kupanda kwa tshs 100) na zile bundle za net zilizopanda buku tano sijui justification ipo wapi I mean je hio yote buku tano na tshs 100/= inakwenda kwenye elimu ?
Mkuu unawezafafanua?
Ina kuna aina ya kodi tatu hapa?
- Kodi ya sh. 1000 kwa mwezi kwa simkadi moja
Mie zimenichanganya.
- Kodi ya asilimia 14.5?
- kodi iliyosemwa kwenye ile barua ya TRA
Hii Kodi inapingwa sana kwasababu sio Progressive. We huwezi kumchaji mtu anayetumia millioni 2 kwenye simu ya mkononi Tshs 1000 na ukamchaji anayetumia Tzs 1000 Tzs 1000. Ni kichaa tu ndo anaweza kukubali hii.
Kama wangeweka kwa kiwango cha utumiaji bado wangepata even more. Mfano:
Ukitumia kuanzia Tzs 0 mpaka Tzs 1000 kwa mwezi kodi inakua 0 Tzs
ukitumia kuanzia Tzs 1001 Mpka Tzs 5000 kwa mwezi kodi ni Tzs 50
Ukitumia kuanzia Tzs 5001 mpaka Tzs 10000 kwa mwezi unalipa Tzs 100
Ukitumia kuanzia Tzs 10,001 Mpaka Tzs 15,000 kwa mwezi kodi unalipa Tzs 300
Ukitumia kuanzia Tzs 15,001 Mpaka Tzs 30,000 kwa mwezi unalipa Tzs 500
Ukitumia kuanzia Tzs 30,001 Mpaka Tzs 100,000 kwa mwezi unalipa Tzs 1000
Ukitumia kuanzia tzs 100,001 mpaka tzs 500,000 kwa mwezi unalipa tzs 2,000
Ukitumia above Tzs 500,001 unalipia Tzs 10, 000
Naamini wangezidi target yao ya Billion 8 TZS.
Ahuitaji kufika darasa la pili kuona hili.