analysti
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 731
- 614
Tatizo la watumishi hewa limekuwa maarufu tangia ilipotolewa katika report ya aliyekuwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ndg Ludovick Utoh. Tatizo hili lilirepotiwa kuwa chanzo cha upotevu wa mabilioni ya shilingi za wavuja jasho wa Tanzania. Pamoja na ukweli huu, tatizo hili halikupewa uzito unaostahili mpaka ilipofika kipindi ndugu Mwigulu Nchemba alipoteuliwa kuwa naibu waziri wa fedha. Hata hivyo waziri huyu alijaribu kulipigia kelele lakini kulikosekana msukumo wenye tija ulioakisi nia ya dhati katika kupambana na tatuizo hili na serikali ilionekana kushindwa kupambana nalo.
Kufuatia kuchaguliwa kuwa rais wa awamu ya Tano kwa Dk.JPM kumekuwa na mfufuko wenye nguvu katika mapambano dhidi ya Tatizo la watumishi hewa. Hii ilijidhihirisha pale rais alipotoa maagizo kwa wakuu wa mikoa kuhakikisha wanalimaliza kabisa tatizo la watumishi hewa ama la wakurugenzi watawajibika ikitokea kuna mtumishi hewa atalipwa mshahara baada ya kipindi kilichotolewa kulimaliza tatizo hilo. Wakuu wa mikoa wamefanya kazi yao kwa ushirikiano na malaka zote zinazosimamia rasilimali watu, na naweza kusema wametekeleza kwa mafanikio makubwa. Kutokana na kazi hiyo, hivi juzi waziri mwenye dhamana alileta taarifa kwa uma juu ya idadi ya WATUMISHI HEWA waliobainika na kiwango cha pesa kilicho okolewa kutokana na kubainika kwao.
THE QUESTION IS...
Hawa watumishi hewa ni kina nani? ni nani anawaajiri hawa watumishi hewa? Watumishi hewa wanapokeaje mshahara wao? Je, kwa kuwa wao ni hewa na mshahara wao nao ni hewa?.
Tumelezwa kuwa miongoni mwa watumishi wanaounda kundi la watumishi hewa ni pamoja na
watumishi waliositautumishi wao kutokana na sababu mbali mbali, watumishi waliofariki dunia, watumishi walio masomoni bila ruhusa rasmi n.k.
Nikiangalia makundi yote yanayounda watumishi hewa inaonekana dhahiri kabisa kuwa ni watu waliokuwa chini ya usimamizi wa watu fulani. Je, ilikuwaje watumishi hawa wakapata sifa ya kuwa watumishi hewa ilhali wapo chini ya usimamizi wa watu hawa fulani, je, hawa wasimamizi walikuwa wanasimamia watumishi hewa na kuendelea kuruhusu mishahara iwaendee watumishi hewa??. Natambua kuwa kuna utaratibu ambao unawaongoza hawa wasimamizi wa namna ya kutoa taarifa punde tu mtumishi anaposita au anapopoteza sifa ya kuwa mtumishi wa uma. Je, hawa wasimamizi taratibu hizi walikuwa hawazitekelezi.
Naomba niseme kuwa, Tanzania hatuna tatizo la watrumishi hewa. Kamwe watumishi hewa si tatizo kwa nchi hii. Tatizo tulilonalo ni hawa viongozi wenye jukumu la kusimamia watumishi katika halmashauri na taasisi za uma. Nashindwa kuelewa ni kwa nini suala hili lilionekana kuwa ni gumu mno kulidhibiti wakati kumbukumbu zipo na watumishi wote wanafahamika?.
Naomba nitoe wito kwa serikali, ili kuweza kudhibiti na kuliondoa kabisa hili tatizo (SI LA WATUMISHI HEWA) la hawa watu wenye jukumu la kusimamia watumishi, kujitengenezea njia ovu za kujipatia pesa kutoka serikalini kwa kupitia watumishi hewa;ifanye uchunguzi ya kuwa ni nani alitengeneza na kutunza watumishi hewa na kuendelea kuneemeka na mishahara ya watu wasiokuwepo kiuhalisia. Ifanye uchunguzi ili ijulikane je, tatizo ni idara, mkurugenzi au ni Utumishi/hazina. Maana yawezekana taarifa zilishafika hazina lakini wao wakaendelea kupeleka mshahara hewa.