Tatizo ni Polisi au wanasiasa?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
19,101
35,681
Tangu kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini Jeshi la Polisi limeonekana kuwa kinyume na vyama vingine vya siasa isipokuwa CCM. Lakini mkuu wa jeshi hilo (Inspector General of Police - IGP) kwa wakati wowote ule hajawahi kutoa tamko ni kwa nini Jeshi analoliongoza linawatendea hivyo watu wa vyama vingine vya siasa.

Kwa mfano wakati Daudi Mwangosi alipouawa Pale Nyororo kwenye uliotarajiwa kuwa Mkutano wa CHADEMA, aliyekuwa Mkuu wa Operesheni wa POlisi alitoa tuhuma kwamba Mwangosi aliuawa na kitu kizito toka kwa wananchama wa CHADEMA waliokuwa wanawarushia Polisi. Kilichofuatia ni historia ambayo sote tunaijua.

Lakini kwa mfano kwa miaka 10 ya Kikwete kama Rais wa Tanzania, ni wabunge na viongozi wangapi wa CCM walikamatwa au kupigwa na Polisi. Ni wakati gani Polisi aliwahi kutoa tamko mahsusi (Specific) dhidi ya vitendo vyake ama kwa wapinzani wao au dhidi ya raia wengine.

Kwa mfano Mama Rose Kamili aliteswa na kudhalilishwa mbele ya viongozi wa CCM na hata Polisi walikwenda kumchukua akiwa amejeruhiwa na kudhalilishwa ndani ya jengo la Ofisi ya CCM mkoa wa Iringa, Polisi mpaka sasa haijawahi hata kuwahoji waliomtia ulemavu mama huyo kwa kuwa tu ni Mwana - CHADEMA.

Hivi matamko na mazuio yatolewayo na Polisi ni kwa ajili ya vyama tu vya Upinzani CCM haihusiki? Kwa mfano inapotangazwa kwamba hakuna kufanya maandamano wala mikutano, hivi sheria ya vyama vya siasa inampa mtu mwingine yeyote zaidi ya OCD wa eneo husika kuzuia maandamano au mikutano ya hadhara?

Kwa mfano Mkuu wa Mkoa anaposema hakuna kufanya maandamano au Mikutano kwenye Mkoa "wake" maana yake kisheria yeye hahusiki na sheria ya vyama vya siasa?
 
Back
Top Bottom