TATIZO NI ELIMU NGUMU AU MAZINGIRA MAGUMU YA UTOAJI ELIMU?

Kozo Okamoto

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
3,391
1,544
Kumekuwa na madai mengi sana kwa watu wengi sana kuhusu ubora wa elimu kati ya Tanzania na Uganda kwamba elimu ya Uganda iko chini kuliko ya Tanzania na wengine wakidai vice versa. Nchi zote zina mfumo wa 7-6-3*4.moja inakuwa je bora kulilo nyingine?Je ELIMU YA TANZANIA NI NGUMU AU MAZINGIRA YA UTOAJI WA ELIMU HII NDIYO MAGUMU?
karibuni wadau wa elimu tujadili
 
Mi nijuavyo ubora unaozungumziwa, Uganda hata mtu aliefeli form four anaenda tu advance tofauti na Tanzania
7-4-2-3
 
Mi nijuavyo ubora unaozungumziwa, Uganda hata mtu aliefeli form four anaenda tu advance tofauti na Tanzania
7-4-2-3

Ok,hivi hapa kwetu mtu ukifeli form 4 then ukaenda kuendelea advanced shule private haiwezekani?
 
Tusiseme mtu aliyefeli O'level hapa Tz, anaweza kwenda kusoma A'level Uganda; bali tuseme mtu aliyekosa sifa za kujiunga na A'level hapa tanzania, anaweza kwenda kusoma A'level Uganda.
Kwa elimu ya Tanzania, mtu alifaulu mtihani ni yule aliyepata kati ya div. 1 hadi 4. Ila mwenye sifa za kujiunga na A'level ni mwenye angalau credit tatu.
 
Ubora wa elimu unatokana na
1. Ubora wa mitaala iliopo,
2. Umahiri wa utekelezaji wa mitaala hiyo,
3. Mazingira ya kutolema kwa elimu,
4. Usimamiaji,
5. Raslimali zilizopo,
6. Tathmini.

Sina uhakika kama Tz tunawashinda/tunashindwa na Uganda ktk namba 1-5. Ila nahisi tunawashinda ktk namba 6.
 
Back
Top Bottom