Tatizo Letu ni Kuwa na Bonge la Chama Tawala na Upinzani Kiduchu!

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Shina la taabu ya nchi hii si ufisadi, ndiyo, yawezekana hilo likawa ni mingoni mwa majani mengi yanaouzunguka mti huu mkubwa!

Tena nazidi kukataa. Shina la taabu yetu si matumizi mabaya ya madaraka, naam, yawezekana hili likawa ni tawi katika mti ule-ule!

Shina na Shida yetu kuu sisi tuna wanasiasa wazito wa kuelewa kuwa katika nchi za kidemokrasia; maendeleo huja baada ya kuwepo kwa msuguano wa hoja!
Na ili uwepo msuguano huo; ni lazima uwepo mringano wa nguvu kati ya chama tawala na vyama vya upinzani.

Tazama eti kwetu sisi bado tunaviangalia vyama mbadala kama maadui wa taifa! na hapo ndipo tulipokwama!

Binafsi, kwa nia njema kabisa mimi ni miongoni mwa watu wanaotamani siku moja utokee mpasuko wa maana ndani ya ccm kwa maslahi mapana ya nchi.
Pande moja libaki katika ccm na lingine likauimalishe upinzani.

Ndiyo, nasema kwa maslahi mapana ya kuujenga upinzani imara unaoweza kuja na mawazo mbadala ya kuijenga nchi hii.
Zaidi ya hapo tuwe na upinzani utakaofanya chama tawala kiwe imara na makini kwa hofu ya kukataliwa na wananchi.

Kwa bahati mbaya sana pengine kwa sababu ya uelewa mdogo; katika nchi hii mtu anapoongelea upinzani wengi wetu wanadhani kuwa si ccm inayoongelewa hapo!

Ni muhimu tukaelewa kuwa ccm ni upinzani mtarajiwa!

Ndiyo maana mimi sitopenda ccm ife au iwe dhaifu pindi kitakapokuwa nje ya dola, pindi ikitokea hivyo, lakini bado natamani ije kutoa upinzani mkali kwa chama tawala kitakachokuwa madarakani.

Mwisho Ndugu zangu watanzania ni kwamba; hivi vyama ni njia za kilaia za kuendeshea nchi na si zaidi ya hapo.
Taifa liko juu kuliko vyama vya siasa.
Hivi ni kama nguo unaweza kubadiri kama upendavyo!
 
Sio kweli kwamba upinzani ni kiduchu... tatizo ni goli la mkono na tume ya uchaguzi isiyo huru... usidanganye watu mkuu...
 
Sio kweli kwamba upinzani ni kiduchu... tatizo ni goli la mkono na tume ya uchaguzi isiyo huru... usidanganye watu mkuu...
Hayo uliyoyasema ni matokeo ya kuwa na upinzani kiduchu!
Nadhani uliona katika bunge la katiba.

Ili uzuie hilo goli la mkono unalosema unahitaji uwe na wingi katika vyombo husika vinginevyo jeuri itabaki kuwa jeuri tu dhidi yako.
 
Back
Top Bottom