Tatizo letu kubwa tunategemea sana wanasiasa!!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
7,276
9,973
Nilikuwa najiuliza kila siku je ni kitu gani hasa kinacho tuchelewesha kwenye harakati zetu za maendeleo. Kwa uzoefu wangu na nimeweza kuishi nchi mbalimbali duniani nimeona tatizo kubwa ni kwamba tunaserikali kubwa sana na wananchi wanategemea sana wanasiasa kutatua matatizo yao mengi ambayo ni ya kiuchumi na kimfumo.

Kila kitu Watanzania tunategemea serikali kwenye kazi, shule, ndege-- , na ubaya zaidi hata wataalamu wengi wanatoka kwenye elimu/vyuo kama walimu lakini hatuna wafanyabiashara au viongozi wa makampuni kama watu wanao saidia kwenye sera nchi za wenzetu hata wakibadilisha viongozi uchumi kuna watu ambao tayari wameshaweka mfumo tegemezi kwenye bank na uchumi kwa ujumla.

Korea kusini, Japan, German utaona kampuni ndiyo zinaweka sera nyingi za kazi na ajira sio wanasiasa pekee
 
Kwenye kitabu cha OUTWITTING THE DEVIL,Napoleon Hill anamfanyia interview shetani,anasema huwa anashughulika sana na akili zisizotaka kuwfikiri,zinategemea sana watu wengine wafikiri kwa niamba yao amabao ni wanasiasa,walimu wa dini,na walimu mashuleni ni kifaa mojawapo ambao ni mtaji wa shetani kuwarubuni watu wa Mungu,unaambiwa binadam alikuwa nyani unakubali tu huwez hata kufikiri kivyako hata kidogo,wanasiasa ndio waharibifu wa maendeleo ya watu na ustawi wao katika masuala muhimu
 
Siku ukianza kutoa fikra ya role ya serikali kwenye maisha yako utafeli, serikali ipo kila sehemu, na ki kawaida serikali inatakiwa i solve matatizo ya wananchi, direct au indirect, kwa sababu wana nchi wana lipa kodi.
So hata nchi za wenzetu serikali ina weka mazingira mazuri ya mtu anaye jiongeza kidogo tu afanikiwe.
 
Siku ukianza kutoa fikra ya role ya serikali kwenye maisha yako utafeli, serikali ipo kila sehemu, na ki kawaida serikali inatakiwa i solve matatizo ya wananchi, direct au indirect, kwa sababu wana nchi wana lipa kodi.
So hata nchi za wenzetu serikali ina weka mazingira mazuri ya mtu anaye jiongeza kidogo tu afanikiwe.
Serikali inatakiwa kufanya vitu ambavyo wananchi mmoja moja hawawezi kufanya sio kila kitu wafanye serikali na ndiyo sababu kubwa ya umasikini wetu wa kupindukia
 
Kama kitu gani Mkuu kidogo raia anaweza kufanya bila serikali.. Kumbuka kila jambo linafanyika juu ya ardhi, ardhi ni mali yako? Na huwezi kufanya lolote bila kibali au idhini ya serikali,! Huwezi kuagiza chochote kikaingia nchini bila serikali. Kwahiyo waza tena tutafanikiwaje kupitia serikali hii kubwa yenye ukanda na uchama?
 
Back
Top Bottom