Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,443
- 40,537
Pamoja na kukataza kuonesha Bunge Mubashara, leo tumeshuhudia kundi zima la walishadadia bunge kutokuoneshwa Mubashara wakiwa na bashasha kwa Mkutano wao Mkuu kuoneshwa Mubashara. Kwa maana nyingine wao wanaona vikao vya chama chao ni muhimu sana kuliko vikao vya Bunge letu ambalo linamuhusu kila mtanzania.
Lakini hicho walichotaka kioneshwe Mubashara si kitu au jambo la muhimu sana kwa watanzania wote. Chama cha siasa kubadili katiba yake ni mambo ya chama husika na kulifanya kama ni jambo la maana sana kwa nchi basi hao wenye mawazo hayo wana mawazo mufulisi!!
Mkwamo kwa nchi yetu hausababishwi na Katiba ya CCM ikoje, bali unatokana na Katiba ya nchi yetu ikoje. Katiba iliyotungwa katika mfumo kwamba nguzo zote za utawala zinawajibika kwa mtu mmoja tu Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania ndiyo inayotakiwa kubadilishwa na wala si ya chama cha siasa ambacho kinaweza kuondolewa madarakani kwenye uchaguzi wowote huru na wa haki.
Watanzania hawana ajira za uhakika, hawana masoko kwa mazao yao, hawana huduma za kuaminika za Afya, huduma za maji ni dhahama,Uchumi wa familia zao umeyumba, mambo mengi yameparaganyika, hata Katiba ya CCM ifutwe kabisa haitaathiri maisha yao bali kinachoathiri maisha yao ni Katiba ambayo pamoja na kuchukia baadhi ya mambo hawana cha kufanya kuyaondoa zaidi ya kusubiri "Rais aamue".