Habari wana jamvi?!
Naomba kujua dawa ya kuondoa uchafu wa masikio. Tatizo langu ni kuwepo kwa vitu vigumu/uchafu ambao najaribu kila siku kuutoa au kuupunguza bila mafanikio .nimeshatumia mpaka dawa ila naishia kupata maumivu.Wakati wa kuoga maji yakiingia kwenye masikio hayatoki hivyo kuziba masikio KWA siku kadhaa.Pia nikitumia njiti maalum za kutolea uchafu masikioni naumia na masikio yanaziba.
Nitashukuru kwa ushauri!