Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

wa UDOM

Member
Apr 10, 2011
34
2


MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU TATIZO LA SIKIO
Mwanangu ana umri wa miaka 2 na nusu.

Ameanza kuugua ugonjwa wa sikio kuuma na ku_discharge mara kwa mara na doctors wamekuwa wakimpa atibiotics ambazo nimeona hazimsaidii.

Mara hii anaumwa ni awamu ya 3 ugonjwa kumrudia, nifanye nini jamani?
---
---
---
---
---
---




Sikio ni sehemu ya mwili inayowezesha kusikia sauti. Wanadamu na wanyama mamalia wana masikio mawili kichwani. Wanyama wengine husikia sauti kupitia viungo vingine kama vile buibui kupitia nywele za miguu au samaki kupitia neva ndefu iliyopo chini ya ngozi kando ya mwili.

Sikio la binadamu huwa na sehemu ya nje inayoonekana na sehemu isiyoonekana iliyopo ndani ya fuvu. Usikivu wenyewe hutokea kwenye sehemu ya ndani.

Sehemu ya nje yenye kazi ya kupokea na kukusanya mawimbi ya sauti na kuyaelekeza ndani ya njia ya sikio inayoishia kwenye kiwambo cha sikio ambacho ni ngozi inayotikiswa na sauti.

Kucheza kwa kiwambo kunatikisa mifupa sikivu ambayo ni mifupa mitatu midogo inayoungwa nacho na mwendo wa mifupa sikivu unapokelewa na mishipa ya fahamu ya sikio la ndani ukibadilishwa kwa mishtuko ya umeme inayopita kwenye neva hadi ubongo. Chumba cha sikio la kati kimeunganishwa na koromeo kwa njia ya neli ya koromeo.

Sehemu ya kiwambo cha sikio pamoja na chumba nyuma yake penye mifupa sikivu huitwa sikio la kati. Nyuma yake kuna sehemu ya sikio la ndani. Kiungo cha mwili kinachobadilisha mwendo wa mishipa sikivu kuwa alama za neva huitwa komboli.

Kazi nyingine za masikio

Pamoja na kupokea sauti, sikio la ndani pia lina kazi ya kutunza uwiano wa mwili likiweza kutofautisha kati ya juu, chini, kulia na kushoto.

Wanyama mbalimbali hutumia masikio pia kwa kupoza mwili. Hivyo tembo anatumia masikio yake kama feni.

Matatizo na magonjwa ya sikio

Sehemu zote tatu za sikio zinaweza kuathiriwa na magonjwa na maumivu.
  • Sikio la nje huwa na ngozi laini ambayo inaweza kuumizwa na vidonda na kuambukizwa. Njia ya sauti inaumizwa kama watu wanajikuna ndani yake kwa kidole kichafu au kwa kutumia vijiti. Mara nyingi inajazwa hasa na nta ya mwilini inayokusanyika hapa na kuzuia sauti kupita vema. Daktari anaweza kusaidia kwa kuondoa nta au uchafu mwingine uliokusanyika akitumia mpira mdogo na maji ya vuguvugu.
  • Sikio la kati linapata matatizo yafuatayo: kiwambo cha sikio kinaweza kuumizwa, kwa mfano kwa kuingiza kitu ndani ya sikio, kutokana na mlio mkubwa mno kama mtu yuko karibu na mlipuko na pia kutokana na magonjwa. Magonjwa inayotokea mara yingi ni mchonyoto wa chumba cha mifupa sikivu kwa sababu bakteria zinaweza kupitia neli ya koromeo na kuingia ndani; wakati wa magonjwa ya shingoni neli hii inaweza kuvimba na kufunga bakteria ndani ya sikio la kati ambako zinasababisha mchonyoto. Mchonyoto katika sehemu hii inaleta maumivu makali. Isipotibiwa ambukizo linaweza kuathiri hata kuharibu mifupa sikivu.
  • Sikio la ndani huumia kama makelele yanazidi. Kuzidi kwa makelele au pia kupokea mlio mkubwa wa mlipuko wa karibu unaweza kuharibu neva ndogo zinazobadilisha mwendo wa mishipa fahamu kuwa alama za neva. Sehemu hii inaweza kushambuliwa pia na maambukizi ya virusi mbalimbali.
Kuna pia matatizo ambayo hayajaeleweka vema na wataalamu kama tinnitus ambako mtu anasikia sauti ya kudumu ndani ya sikio hata kama wengine hawawezi kusikia kitu. Tatizo lingine ni upotevu wa usikivu upande mmoja unaotokea hasa kwa watu wanaobanwa na matatizo na shughuli nyingi. Matatizo haya yana upande wa nafsi na majaribio ya tiba huenda sambamba na kumpatia mgonjwa kipindi cha raha na mapumziko pamoja na athari nyingine za kutuliza moyo.

Pia watumiaji wa earphones ni rahisi kuumia sikio ukitumia sauti kubwa.

MAONI NA USHAURI ULIOTOLEWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
----

----
---
---
 
Hiyo ni very serious aiee.

Nenda ENT muhimbili na uhakikishe anatapa huduma muhimu... madhara ya sikio ni makubwa sana ndugu yangu

Kuna Dr. wanamwita Kimario ni mzuri sana na ana priavte clinic yake... kama uko dar mtafute through 0784 883190
 
Mh! Bangi??? Hata km ni dawa simshauri, sikio ni kitu kngne, ukikosea kidogo ndo ushamtia mtoto uziwi. Nenda kwa wataalam wa ENT, achana na bangi imekaa kienyeji sana!
Chemsha bangi, chuja, maji yake mtie sikio lenye matatizo, tone moja asubuhi, mchana, na usiku. Siku tatu, kama hajapata nafuu muone "specialist" wa ENT.
 
mh! Bangi? Hata km ni dawa cmshauri, sikio ni k2 kngne, ukikosea kdgo ndo ushamtia mtoto uziwi. Nenda kwa wataalam wa ENT,achana na bangi imekaa kienyeji sana!

Hapo wala sijafanya mchezo wala utani, anaeongelewa ni mtoto mdogo na ninathamini sana afya na furaha ya watoto, mimi nna vijukuu tayari.

Kuhusu bangi, naomba ufahamu kuwa ni dawa kubwa sana na imetumika kwa miaka mingi sana kama tiba ya mambo mengi tu, na mojawapo ni hiyo ya kutibu masikio.

Nakuomba google kidogo "marijuana cures" upate kuona bangi inavyo-tibu, ina-tibu mpaka baadhi ya cancer.
 
Zamani tulitumia majani ya bangi mabichi. Unatwanga kisha unakamulia tone kwenye sikio. Pia tulitumia mafuta ya kuku! Kizazi cha sasa so delicate kuhimili tiba za aina hii! Achana na hosp. za kitaa nenda Hospital kaone wataalamu.

Kama uko Moshi nenda KCMC. Kwa sasa utapata huduma nzuri maana hakuna wagonjwa wengi sana wote wametimkia kule!
 
Sijasema haitibu, ila kumbuka sikio la mtoto limemwuma kwa muda mrefu na ame2mia aina tofaut za dawa bla mafanikio, sa kuendlea kumjazlisha madawa huoni ni hatari? Unaonaje km ataenda kwa hao specialst wa ENT?

Hata mimi nafaham bangi ni dawa ila hii imeshakuwa serious case!
 

Hilo sipingani nalo kabisa na ndio maana kama utasoma vizuri "post" yangu, mimesema atumie siku tatu, kama haimsaidii aende akawaone ma "specialist" wa ENT.

Tunamuombea Mungu huyu mtoto apone kwa haraka. Sikio linauma vibaya sana. Na yote tuyasemayo hapo ni ya kujaribu kumtakia afya yake irudi na awe salama.
 
Mungu akubariki ndugu yangu!
 
Nawashukuru sana ndugu zangu. Michango yenu ninaithamini sana na ninaanza kuifanyia kazi mara moja.
 
Hilo tatizo je ulikuwa wakati anatumia antibiotic unamsafisha hilo sikio kwa kutumia zile pamba za masikio inasaidia sana huku anatumia dawa na wewe unamfanyia usafi asubuhi mchana na jioni na hicho kipamba unatubukiza kwenye maji ya vuguvugu kabla hujamsafisha nacho.
 
Pole sana ! Naamini mtu wa karibu anapooumwa familia nzima inakuwa na mfadhaiko. Umefanya vema kuuliza kwa wana-jf, Mungu alitupa mimea na wanyama kama dawa zetu na chakula, ndiyo maana hata mchungaji wa Loliondo amefunguliwa hayo.

Bangi na mafuta ya kuku ni tiba kwa maradhi ya sikio. Miye, niliwahi kushuhudia tiba hiyo kama walivyoeleza wana -jf !. Kama hutafanikiwa nenda kawaone wataalamu, usisahahau kumfanyia usafi mara kwa mara, hiyo ndiyo dawa ya kwanza. Mungu akutie uvumilivu na nguvu.
 
nawashukuru sana ndugu zangu.
michango yenu ninaithamini sana na ninaanza kuifanyia kazi mara moja.

Niliwahi kuelezwa kuwa mafuta ya kenge pia ni dawa nzuri. Binafsi sijawahi kujaribu ila Usukumani inatumika sana na wanaisifia.
 
MWONE dR. eDWIN WA MUHIMBILI 0715 283569 make appointement with him! is a gud ENT specialist
 
Pole sana utakapopata matibabu na tibu naomba uje utuambie as maisha haya uwezi jua lini itakuwa kwako
 
Nenda Magomeni karibu na kwa Shehe Yahaya kuna hospitali ya mmasai mmoja ni madocta wa koo, masikio na pua. Mwanangu alikuwa na tatizo hilo akiwa na miezi kama nane hivi. I attended a clinic there for sometime (almost six months once a week).

It took him two weeks to recover but we kept going there to as recommended by doctors. na sasa hivi anakaribia miaka minne tatizo halijajirudia tena. Walinambia ni fangus (walimpima) na walikuwa wanamsafisha kwa dawa kila nikienda na wanampaka dawa. I strongly recommend that clinic. Ni madokta wa Muhimbili. Si unajua kwenda muhimbili ni issue.
 
Pole sana maana mtoto mdogo hivyo akiumwa hata wewe mambo yako yanasimama.
 
Kuna doctor wa Muhimbili anaitwa Ekenywa, ila ana hospitali yake magomeni mwembechai, Mimi mwenyewe nilishaumwa sikio sana kama ambavyo mwanao ameumwa lakin nilipomuona ilinichukua wiki moja tu kupona. kufika kwenye hospitali yake fuata barabara ya lami iliyopo kwenye petrol station ya mwembechai, ukifuata hiyo barabara unatokezea magomeni Mikumi.

Ukiwa hapo sheli jaribu tu kuuliza kwa doctor Ekenywa utaoneshwa. Kwa bahati mbaya namba yake nimeiacha hom, by now cko tz. Lakini nakupa ukweli usiache kumpeleka kwani matibabu yake ni ya uhakika.
 
wa UDOM,
Omba rufaa mpeleke MUHIMBILI na nakupa namba za Madaktari bingwa Dr. ENICA 0754307717 na Dr. KIMARO 0784883190. Angalizo usikubali mtoto atibiwe PRIVATE.Atibiwe hapo hapo Muhi2.Yaani sina cha kuwalipa hao wataalam kwa jinsi walivyo toa tiba sahihi kwa mwanangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…