ngivingivi
Senior Member
- Mar 29, 2013
- 189
- 109
Maji safi Morogoro limekuwa tatizo la kudumu ambalo mamlaka husika inaonekana zimeshindwa kutatua tatizo kwani maji safi kwa sasa Morogoro hayatikani kabisa Mimi ni mkazi Wa Area six au maarufu kwa jina la Ninja, hapa ninapoongea Nina zaidi ya miezi mitatu sijapata maji kabisa pamoja na kufuatilia ofisi zinazohusika kwa maana ya Moruwasa lkn majibu tunayopatiwa ni dhaifu sana kwa kweli, haiingii akilini unapoambiwa tena na muhandisi eti hupati maji kwa sababu uko kwenye mwinuko wakati ni wao wenyewe walikagua wakafunga mabomba pamoja na mita, na kila mwezi wanatucharge service charge kama sio wizi ni nini? Juzi namwona Mkurugenzi wao kwenye taarifa ya habari ITV akijitetea eti tatizo linasababishwa na kupungua kwa kina cha maji katika bwawa la Mindu kitu ambacho sio kweli kabisa, ukichukulia kwamba hata kipindi cha mvua hatujawai kupata maji. Ushauri wangu kwa mkurugenzi wa mamlaka ajaribu kuwa mbunifu kwa kuwekeza kwenye vyanzo vingine vya maji kama visima vikubwa aache kufanya kazi kwa kukariri kwani uongo una mwisho, aseme ukweli kwa nini kuna upungufu mkubwa Wa maji Morogoro na sikuleta siasa kwenye Maisha ya watu.