Mkuu Kiluwiluwi, POLE...Unajua Magonjwa mengi leo, yametokana na mtindo wa maisha(Lifestyle), hii ikiwa na maana, magonjwa mengi ikiwemo Fungus(Fungi) yanaweza kuzuilika iwapo tutabadili mitindo ya maisha hada uvaaji kama vile kupunguza nguo nyingi/nzito mfano leo hii vijana wengi pamoja na nguo za ndani(boxer) huvaa kaptula moja au mbili na kisha suruali/jeans na kina dada pia huvaa nguo za ndani(bikini,/G-string)na kuongezea nyingine, skin tight/ underskirt na kisha skirt/jeans nk.
Kwa kawaida kila eneo la mwili lina bacteria wasio na madhara(Normal flora) na hawa hubadilika na kuleta magonjwa pale joto linapozidi(kwa wanaume) na mabadiliko ya siku za mwezi(mzunguko) na joto linapozidi(kwa wanawake).
-Punguza kuvaa nguo nyingi (hii hupunguza joto)
-Usivae nguo za ndani zilizo mbichi
-Hakikisha hutumii sabuni kali(Antibacteria), .kwa mfano
mtu hana tatizo la bacteria katika sehemu za siri, na
anang'ang'ana kutumia ANTIBACTERIAL SOAPS, ili
iweje?
- Fika katika kituo cha Afya/ Hospitali uonapo dalili za
muwasho, kubadilika kwa rangi ya ngozi n.k
FUNGUS SUGU:
Mara nyingi wagonjwa hulalamika, nilitumia dawa ikaisha na sikupona, hii hutokana na kwamba nguo za ndani hazipaswi kuchanganywa na nguo zozote na hivyo mara baada ya kupata matibabu.
1.Hupaswi kurudia nguo za ndani za zamani.
2.Hupaswi kuchanganya nguo za ndani na nyingine hasa
socks.
3.Nguo za ndani zinapaswa kufuliwa na kisha kuanikwa
katika mwanga wa Jua au kupigwa pasi kwa moto mkali
kwa muda mfupi.
4.Epuka kutumia sabuni zinazoweza kuua bacteria wenye
kuleta kinga(Normal flora), yaani antibacteria mathalani
ukiwa huna tatizo lolote.