Kwanza anza kwenda hospitali ukachunguzwe mkuu,nilikuwa na tatizo kama la kwako ,nilienda mhumbili,pia nilifika kitengo cha magonjwa ya moyo cha jk hapo muhimbili lakini hawakuona tatizo,hapo muhimbili nilifika Mara mbili,baadae nikaja Bugando kama Mara nne nikafanyiwa vipimo vya kila namna lakini wapi.
Mwisho wa siku nikaona nionanae na daktari wa mfumo wa chakula ,hapo hapo Bugando anaitwa Dr majinge ,nishukuru mungu hapo ndo ulikuwa mwisho wangu wa kwenda hospitali, hadi sasa Nina miaka miwili bila kwenda tena hospital, maana ilionekana Nina madonda ya tumbo hivyo nilipewa masharti ya namna ya kuishi na madonda ya tumbo na vyakula amabavyo sipaswi kutumia.
Nishukuru mungu kwa sasa hata madonda ya tumbo sioni tena dalili,lakini pia nikili kuwa watu wengi hufa kwa kukosa matibabu na huduma mzuri za afya kwanini kwa namna hali yangu ilivyokuwa imefikia nilikuwa nimekata tamaa sana lakini kwa sasa Niko buheri wa afya.
Ushauri wangu ni kuwa hebu nenda hospitali ukafanyiwe vipimo vyote vya moyo ili kubaini tatizo baada ya hapo Pima vipimo vya mfumo wako wa chakula.
Mwisho nakupa pole sana,lakini pia kama huna bima ya afya na kiuchumi hauko vizuri naongeza kukupa pole.