Tatizo la Kupepesuka lenye Ukosefu wa Umakinifu (TKUU) ni tatizo la kiakili la aina ya ukuaji wamishipa ya fahamu na ubongo ambapo inaleta matatizo makuu katika umakini wa mtoto hata watu wazima. Tatizo hili huweza kuonekana kwa mtoto kuanzia miaka 6-12 ambapo liaathili upande wa usomaji na tabia ya mtoto. Tatizo hili husababishwa na matatizo mbali mbali yanayoleta usumbufu katika ubongo kwa muda mrefu, na mara nyingi huathili zaidi maeneo yanayojishughulisha na usikivu/utulivu (attention), kujizuia(impulse/self control), kumbukumbu(memory) na mahusiano na jamii au watoto wenzao (social interaction)
Tatizo hili linawasibu watoto wengi na wazazi huenda wakajua au wasijue, na hii ni kulingana na uelewa walionao kuhusu mahitaji maalumu kwa watoto. Unaweza ukamuona mtoto anafanya mambo ambayo hayalingani na umri wake ukafikiri ni makusudi kumbe ana tatizo hili. Ili ijulikane kama mwanao ana tatizo hili ni vema akafanyiwa uchunguzi, ambapo dalili hizi ni sharti ziwe zimeanza mtoto akiwa kati ya miaka sita na kumi na mbili na zidhihirike kwa zaidi ya miezi sita. Kukosa umakini hufanya matokeo kuwa duni anapokuwa anafundishwa kitu chochote au akiwa shuleni. Licha ya hali hii kuwa tatizo la kiakili lililotafitiwa na kutambuliwa mara nyingi katika watoto na vijana, kisababishi chake katika visa vingi hakijajulikana.
Kimsingi tatizo hili lipo duniani kote ingawa huwapata zaidi wototo wa kiume kuliko wale kike. Karibu asilimia 30 - 50 ya watu wanaotambulika kuwa na tatizo hili wakiwa watoto huendelea kuwa na dalili hizi katika utu uzima, na asilimia 2 - 5 ya watu wazima wana hali hii. Hali hii inaweza kuwa ngumu kutofautisha na matatizo mengine sawia na yale yenyekutomakinikakwa kawaida. Kuna vituo maalum ambavyo matibabu ya kwanza kwa watoto wenye dalili kali wanaweza wakafanyiwa uchunguzi na kupewa dawa na ushauri, pia kwa wale wenye dalili za wastani wasiorekebika baada ya kushauriwa. Athari za muda mrefu za dawa hizi hazijulikani na matibabu haya hayapendekezwi kwa watoto walio chini ya umri wa kwenda shule.
Ishara na dalili
Mara nyingi kutomakinika, kupepesuka (kutotulia kwa watu wazima), na tabia ya kuzua vurugu na malumbano ya ghafla hupatikana katika TKUU. Kutatizika katika masomo hutokea mara nyingi pamoja na matatizo ya kimahusiano. Dalili zinaweza kuwa ngumu kufasili kwa sababu ya ugumu wa kutambua mwanzo wa kiwango cha kawaida cha kutomakinika, kupepesuka na mwisho wa viwango muhimu vinavyohitaji usaidizi. Mtu asiyemakinika anaweza kuonyesha baadhi ya/au dalili hizi zote:
- Kuvurugika mawazo kwa urahisi, kutotambua habari za kwa kina, kusahau na kubadili shughuli kutoka moja hadi nyingine mara nyingi.
- Kuchoshwa na kazi baada ya muda mfupi isipokuwa pale mtu anapofanya kazi inayomvutia
- Ugumu wa kuwa makini katika kujifunza jambo jipya
- Tatizo la kukamilisha au kuwasilisha kazi ya ziada (individual assignment/ home work), mara nyingi kutokana na kupoteza vifaa (kwa mfano penseli, vitu vya kuchezea, kazi ya ziada) vinavyohitajika kukamilisha kazi au shughuli hizi.
- Kutokuwa msikivu anapoongeleshwa
- Kuzubaa, kuchanganyikiwa kwa urahisi na kutembea polepole
- Ugumu wa kuchakata habari haraka na kwa usahihi kama watu wengine
- Ugumu wa kufuata maagizo
- Kuhangaika na kufurukuta anapoketi.
- Kuzungumza bila kukoma.
- Kukimbia huku na kule, kugusa au kuchezea kitu chochote au kila kitu anachokiona.
- Ugumu wa kukaa kwa utulivu wakati wa chakula, shuleni, akifanya kazi ya ziada na wakati wa kusimuliwa hadithi
- Kuwa mbioni kila mara
- Ugumu wa kufanya kazi au shughuli zinazohitaji ukakamavu.
Matatizo yanayoambatana na hali hii
- Kukosa subira
- Kuropoka maoni yasiyo mwafaka, kudhihirisha hisia kwa uwazi na kufanya mambo bila kuzingatia matokeo yake
- Ugumu wa kusubiri vitu wanavyotaka au kusubiri zamu yao katika mchezo
- Mara nyingi hukatiza mazungumzo au shughuli za wengine.
TKUU katika watoto hutokea yakiambatana na matatizo mengine kwa takriban 67%. Baadhi ya hali zinazohusiana na hali hii mara nyingi hujumuisha:
Kuna uhusiano kati ya mtoto kukoja kitandani bila kuaha, mtoto kuchelewa kuongea(speech delay ) na tatizo la kudumaa .
- tatizo la ukaidi, upinzani na na ukosefu wa maadili, hali hizi hutokea pamoja zikiambatana na TKUU kwa takriban 50% na 20% ya visa mtawalia. Hali hizi hutambulika kwa tabia za kupambana na jamii kama vile usumbufu, uchokozi, hasira za kila mara, ulaghai, udanganyifu na wizi. Inaonekana kuwa nusu ya watu wanaopepesuka na wana tatizo la ukaidi wa kiupinzani au tatizo la kitabia hupata tatizo la kutojichanganya na jamii katika utu uzima.
- kukosa uangalifu, jambo linaloashiriwa na viwango vya chini vya umakini na uzingatifu, na pia ugumu wa kutolala. Watoto hawa huelekea kuhangaika, kupiga miayo na kujinyoosha na kuonekana kupepesuka sana ili wapate umakini.
- kuwa na wasiwasi na hii hutokea mara nyingi kwa watu wenye TKUU.
- matatizo ya utumizi wa awa za kulvya. Vijana na watu wazima wenye TKUU wapo katika hatari zaidi ya kutumia dawa za kulevya na mara nyingi huwa ni pombe au bangi. Sababu ya hali hii inaweza kutokana na njia ya kuzidiwa ya ubongo wa mtu mwenye TKUU. Hali hii hufanya matibabu ya TKUU kuwa magumu zaidi, huku matatizo ya athari ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya yakitibiwa na kutibiwa kwanza kwa sababu ya hatari zake kuu.
Kisababishi
Kisababishi cha tatizo hili huhusishwa huhusishwa na maambukizi ya awali au jeraha kwenye ubongo. Lakini pia tafiti zinaashiria kuwa tatizo hili mara nyingi hurithiwa kutoka kwa wazazi huku jenetiki ikisababisha takriban asilimia 75 ya tatizo hili. Kwa leo nnaomba niishie hapa…nakaribisha mawazo zaidi…..au kwa wale wenye watoto wenye mahitaji maalum na wanahitaji ushauri wanaweza wakawasiliana nasi kwa email hii specialneed4all@gmail.com