Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

Anapenda kula vyakula vya aina gani hasa ???
Kuhusu vyakula ni vile vile ninavyo kula mimi (na wanafamilia wengine.

Lakini sisi wote tunapata choo ila yeyetu.

Week iliyopita tulikula makande na wanafamilia watatu (nikiwemo na mimi) tulipatwa na tatizo la kuharisha lakini mwenzetu wapi! hakunya kabisa mpaka jana ndio aliniambia anajihisi mavi yamembana.

Lakini alipo rudi chooni aliniambia hakupata choo kama alivyo kua akitegemea zaidi ya kujamba tu na kutoa kinyesi kidogo kama cha kuku.
 
Anywe juice ya ukwaju aweke asali vijiko vinne kwa glasi anywe na maziwa ya ng'ombe fresh glass nne atapata choo hadi kitajaa
 
MARADHI YA KUTOPATA CHOO KIURAHISI (CONSTIPATION):






UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.


MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.


NINI HUSABABISHA TATIZO?
Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.


NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda chooni. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu

yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili

kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na

kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.


MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION):

Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama

cha mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa.
Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.


SABABU ZA MARADHI HUSIKA:
(1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B.
(2) Maradhi ndani ya utumbo mpana.
(3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano.
(4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga.
(5) Kutokunywa maji ya kutosha.
(6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi.
(7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo.


TIBA: 1
Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.

TIBA: 2
Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asali robo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.

TIBA: 3 Anywe kwa wingi Maji ya Uvuguvugu kila siku anapo amka asubuhi kabla ya kula kitu anywe maji glasi 3 kisha akae kwamuda wa saa 1 bila ya kula kitu baada ya saa1 kupita anaweza kula chakula. Na wakati wa mchana anywe tena maji glasi 2 afanye kama alivyofanya wakati wa asubuhi. Na wakati wa usiku anywe tena Maji kama alivyo kunywa wakati wa mchana. Na anapokwenda kulala anywe Maji ya uvuguvugu glasi 1 kisha alale akifanya hivyo kila siku atapona. Ukiwana Swali lolote unaweza kunitafuta kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano

 

Attachments

  • constipation.jpg
    13.7 KB · Views: 109
Mkuu hapo kuwa na ulimi wenye utando mweupe umenikumbusha mtu flani
aliye kuwan tatizo hilo la "constipation" na kweli ulimi wake ulikuwa kama na utando
mweupe mweupe hivi....daaa ntaenda kumgusia hizi hadidu za rejea za mzizimkavu.
 

Mkuu nasikia Vitunguu Swaumu vinasaidia kwa watu wenye tatizo hilo je ni kweli?
 
Mkuu MZIZI hizi dawa (tatu) unatumia zote kwa pamoja au unachagua iliyo nyepesi kwako kutumia?
 
kula chungwa na makapi yake ya ndani usile maganda ya nje halafu let's mrejesho kwa maelekezo zaidi...
 
Mkuu MZIZI hizi dawa (tatu) unatumia zote kwa pamoja au unachagua iliyo nyepesi kwako kutumia?
Unaweza kutumia Tiba namba 1 na Tiba namba 3 ukatumia pamoja au pia Waweza kutumia Tiba namba 2 na Tiba namba 3 ukatumia pamoja usije kutumia Tiba namba 1 na Tiba Namba 2 kwa pamoja shauri yako.
 
Habari yako! Kwa tatizo hilo tafadhali jaribu kumshauli aenda kwenye vituo vya afya ili wakajue tatizo linalomsumbua.asante.
 
Pole sana . Nipe namba yako ya simu nikusaidie. Hill tarizo namengine mengi yataisha.
 
Check pioa kama una kaswende(VDRL). smetimes huchangia kwenye hilo tatizo
 
Choo muhimu.

Chakula unachokula kama hukitoi kwa kufikiri haraka haraka hata kama hujapewa darsa unategemea nini?

Lazima ikuletee matatizo ya kiafya mbeleni (baada ya kipindi fulani kupita)
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…