Tathmini - Saba Saba hali mbaya

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,405
Reaction score
289,554
Hili jambo watu wengi wanataka kulificha , sijui ni kwa faida ya nani ?

Kwanza Mabanda mengi ni matupu ( yamekosa wapangaji ) , makampuni mengi ya binafsi hayapo kabisa , tofauti na miaka yote iliyopita.

Zilizojaa ni taasisi nyingi za serikali ambazo kiukweli hazifanyi maonesho ya biashara badala yake zinafanya maonesho ya huduma zao .

Makampuni mapya ya kigeni hakuna kabisa , watu ni wachache sana kuliko miaka yote , na wala hakuna foleni ya barabarani wala milangoni , hii haijawahi kutokea , miaka yote tarehe 6-8 hizi ni sku za pilikapilika hasa , lakini mwaka huu hakuna kitu ! Mengi ya makampuni yaliyojitokeza ni yale yale , yakiongozwa na makampuni ya simu pamoja na wauza pombe .

Pamoja na kwamba wizi wa mifukoni na wizi wa simu haukubaliki , lakini kutokea kwake kunaakisi mlundikano wa watu kwenye eneo husika , kama kuna mtu aliyepoteza simu kwenye maonesho haya , basi labda atakuwa ameisahau kwenye bar ndani ya maonesho au atakuwa ameisahau kwenye daladala aliyoipanda.

Hii kiuchumi maana yake ni kufeli na kuanguka kwa mipango ya uchumi wa nchi ,
 
Ngoja tujenge viwerndor ndo tuje tuoneshe bidhaa
 
Mkuu sijafika ila nilisikia Suala la foleni wamelitatua kwa kuweka machine za kukata risiti fasta Ndio maana hakuna kupanga mstari!
Ingawa inaweza kuwa defensive mechanism baada ya kudoda maana viongozi wa awamu hii kwa ndimi mbili hawajambo.......
 
sizonje anaharibu nchi, hali ya uchumi ni mbaya
 
Mkuu sijafika ila nilisikia Suala la foleni wamelitatua kwa kuweka machine za kukata risiti fasta Ndio maana hakuna kupanga mstari!
Ingawa inaweza kuwa defensive mechanism baada ya kudoda maana viongozi wa awamu hii kwa ndimi mbili hawajambo.......
Na za barabarani zimetatuliwa na nini ?
 
TRA wanahusika kuua biashara sekta binafsi, ukweli ndio huo, wajitathmini, hawakomoi wafanya biashara, wanakomoa uchumi wa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…