Me ni miongoni mwa watu tuliopiga interview pale TASAF makao makuu mwaka jana tareh 18 september, Na nimeshataarifiwa kwamba nmefaulu katika usaili huo na Tarehe 1 july ndo natakiwa kureport kwa ajili ya kuanza mzigo.
Kwanza napenda nimshukuru sana Mungu kwa fursa hii ya pekee, kwani ile interview ilikuwa ni kali sana! Na watu tuliofanyiwa usaili chini ya 200.
Pili shukrani kwa wana JF wote kwani hilo tangazo nililiona mwezi Dec 2012 humuhumu JF. Cha msingi tuendelee na ushirikiano huohuo na tuzidi kutiana moyo siku moja tutafanikiwa!
Shukran!!