TANZIA: Rapa maarufu wa Wenge Musica BCBG afariki ghafla Kinshasa..


GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,921
Likes
37,175
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,921 37,175 280
Aliyekuwa Rapa maarufu wa Bendi Bora zaidi nchini Congo ya WENGE MUSICA BCBG inayoongozwa na JB Mpiana Kikongo wanaitwa ATALAKUS Kijana aitwae Katemo Vanga CELLULAIRE amefariki dunia jana huko jijini Kinshasa wakati akikimbizwa Hospitali baada ya kuugua ghafla tu.

Hakika hili litakuwa ni pigo kubwa katika Tasnia nzima ya MARAPA nchini Congo kwani Marehemu CELLULAIRE aliweza kuwashawishi Vijana wengi wa Congo kujikita hasa katika " kughani " na aliweza kujizolea sifa nyingi sana na kukubalika mno.

Marehemu CELLULAIRE ( Katemo Vanga ) alijiunga na Bendi ya Wenge Musica BCBG mwaka 2003 akitokea katika Bendi ya Kikosi cha pili cha Wenge Musica BCBG kiitwacho PPU baada ya kuonwa na Mwalimu wa MARAPA wengi nchini Congo Tutu Caludgi ( Yombo Lumbu ).

Marehemu CELLULAIRE amefanya Kazi nyingi ndani ya Wenge Musica BCBG ila aliweza kung'ara zaidi katika albums za ANTI TERRO, KIPE YA YO na QUEL EST TON PROBLEM na moja ya RAPU yake iliyombeba ilikuwa ikijulikana kama " KIPALAKIPALA KIZUNGWAKO ".

Marehemu CELLULAIRE aliweza kuleta USHIRIKIANO mkubwa sana katika upande wa ATALAKU au KUGHANI huku akishirikiana kwa ukaribu mno na Kiongozi wa MARAPA ndani ya Bendi ya Wenge Musica BCBG aitwa Pitshou Lisimo maarufu kama GENTAMYCINE au ANTIBIOTIQUE ambapo kwa pamoja wakiwa wanaweka vionjo vyao pale wimbo unapokole katika SEBENE hakika lazima tu utaamka katika kiti na ama kulisakata au kucheza na hata kwenda kuwatunza.

Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa sana nafasi yake ikazibwa na mmoja wa MARAPA wa Kikosi cha pili cha PPU akina Pajo na Bin Laden ambao wamekuwa wakifanya vyema sana japo JB Mpiana huwatumia hawa Vijana wa Kikosi cha pili PPU kwa shows za Congo na kila mwaka hupandisha Vijana kutoka PPU na kuja kwa Wakubwa.

Marehemu CELLULAIRE ( Katemo Vanga ) anatarajiwa kuzikwa Keshokutwa Jumamosi na ameacha Mke na Watoto Watatu ( 3 ).

Kwa wale wana WENGE MUSICA BCBG wenzangu humu JF nawapeni pole sana kwa huu Msiba ila binafsi tokea nipate hizi taarifa nilipatwa na mshtuko mkubwa na nimekosa raha hadi hivi na kuwa mnyonge kwani hakuna furaha ninayoipata katika maisha yangu kama kusikiliza nyimbo za Wenge Musica BCBG kwani naipenda hii Bendi na Wanamuziki wake wote.

Ni hayo tu na R.I.P Katemo Vanga CELLULAIRE.
 
J33

J33

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Messages
1,461
Likes
1,006
Points
280
J33

J33

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2014
1,461 1,006 280
We jamaa unaujua sana muziki wa Congo nafurahia sana maandiko yako kuhusu huu mziki, ni vyema ukawa unatuletea updates au kuanzisha thread za matukio mbali mbali ya mziki huu ili nasi tupate kuelewa!!!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,921
Likes
37,175
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,921 37,175 280
We jamaa unaujua sana muziki wa Congo nafurahia sana maandiko yako kuhusu huu mziki, ni vyema ukawa unatuletea updates au kuanzisha thread za matukio mbali mbali ya mziki huu ili nasi tupate kuelewa!!!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Akhsante kwa compliments zako Mkuu na nitalifanyia Kazi ombi lako ili ikiwezekana niweze kukidhi haja yako / zenu " Bana Congo " wenzangu.
 
Mamaya

Mamaya

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Messages
3,816
Likes
564
Points
280
Mamaya

Mamaya

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2011
3,816 564 280
Bana lunda, bana congo, poleni sana
 

Forum statistics

Threads 1,235,853
Members 474,755
Posts 29,238,576