TANZIA Mwana JamiiForums mkongwe, Dena Amsi afariki dunia

5a3c60bd921241074264492a4ee27513.jpg

Mazishi yamefanyika leo saa tisa alasiri makaburi mapya mbweni
Asante kwa taarifa mkuu. Tuliambiwa kuwa ni alhamisi, kumbe tayari mazishi.!
Poleni sana
 
Mkuu Mulama, pole kwa msiba huu. Kwa sisi waumini wa life after life, Dena yupo na anasoma kila tunachoandika, kilichokufa na kuzikwa ni mwili, a physical body, lakini roho, a spiritual body haifi, roho ndio inayokwenda mbinguni au peponi kwenye raha ya milele au jehanum kwenye zawa la moto na mateso ya milele, na kwa majibu wa michango ya Dena Amsi humu jf, japo mimi sio Mungu, ila saa hii tunapoendelea kuchangia uzi huu, roho yake iliishapokelewa mbinguni kwa Baba saa nyingi.

Paskali
this HTML class. Value is https://www.google.c
Mkuu kumbe wewe ni kundi la nadharia ile ya philosophical idealism,safi sana huwa munaamini maisha yapo baada ya kifo,ni watu wazuri sana kwakuwa muna hofu ya mungu,na kuamini katika siku ya malipo,na msingi wake ni theology.
Nimefurahi kujua maana kuna wenzetu wako kwenye lilebkundi la pili la philosophical materialism,lakini kila mwisho wa wiki unawakuta msikitini au kanisani,na hawaenendi kiimani,ni wanyama kabisa.
 
Natamani sana angekuwa anazisoma hizi msg na condolences zenu kwakweli inauma sana lakini ndo hivyo Mungu keshatoa uamuzi wake tushukuru tu.

Kifupi huyu Dada ndio alini introduce kwenye Jamii Forums maana alikuwa akirudi home atakaa kwenye laptop akisoma na kuchangia huku akicheka saana! Ilinibidi nimsogelee kumuuliza mbona peke yake kucheka na laptop kila akirudi home na sisi kutupa muda mfupi wa maongezi naye?
Ndipo akanionesha jf na akaielekeza namna ya kujiunga.

Dena Amsi yaani jina la Bibi yake mzaa Babaake sio Id aliyoanza nayo humu, alianza na nyingine nimeisahu kwa mshtuko nilio nao juu ya msiba huu, ila ndugu mtabuzi anaweza kunisaidia kukumbusha id ya kwanza ilikuwa ipi.

Tumempumzisha leo yapata saa tisa alaasiri kwenye makaburi mapya Mbweni Dsm.
Sisi ni Wakristu tunaoamini katika uzima wa milele, hivyo tufarijike kwamba mwenzetu kapumzika katika utukufu wa Mungu Baba.
Pole sana Mulama, andiko lako limaelezea mengi
Mungu amlaze pema.
 
Back
Top Bottom