TANZIA: Mmiliki wa mabasi ya Ngorika, Stephen Mberesero afariki dunia

Issa SLuu

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
2,303
1,801
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Ngorika Bus service, yenye makao yake makuu Kisangara mkoani Kilimanjaro, bw. STEPHEN Mberesero amefariki dunia mjini hapa baada ya kugongwa na gari aina ya Land cruiser wakati akizungumza na simu.

Kamanda wa polisi wa MKOA wa Tanga Mihayo msikhera alisema Jana kuwa ajali iyo ilitokea juzi SAA 2;30 usiku katika Barbara kuu ya segera-njiapanda ya himo mjini Korogwe.

Alisema Mberesero ambae mabasi yake hufanya safari Kati ya mikoa ya Arusha,tanga,Daresalaam na singida,marehemu alikuwa amesimama pembeni ya kituo cha mafuta cha Lake oil na kugongwa na gari hilo.

Mfanyakazi wa kampuni hiyo ,Adam Miraji alisema bosi wake huyo alikwenda Korogwe kuangalia Kiwanja kwajili ya kununua kujenga kituo cha mafuta.

Kama unavyojua bosi wetu pamoja na kufanya biashara ya Mabasi,alikuwa anamiliki vituo mbalimbali vya mafuta mkoani Kilimanjaro,Dar es Salaam na Arusha,hivyo alipokuja Tanga alituambia anakwenda Korogwe kuangalia Kiwanja cha kujenga kituo kipya cha mafuta,alisema Adam.

Alisema bosi wake huyo alikuwa ameliweka gari lake katika kituo cha mafuta cha Lake oil na kwamba alishuka kwajili yakuelekea katika Kiwanja hicho.

Wengi waliokuwepo eneo la ajali hawakujua kama ni yeye hadi tulipokwenda kuchukua mwili wake ndipo wakashtuka,Alisema.

Kamanda Mihayo alisema wanamsaka Dereva aliyesababisha ajali hiyo kwa uzembe na kusababisha kifo.

Source, MWANANCHI_27/FEB/
 
Pia ni mmiliki wa Vituo vyote vya mafuta vya TOTAL kanda hii ya kaskazini
Usihofu mleta mada, picha ya namba ya gari tumeshaiwasilisha

Mana dereva aligeuza gari kuona amegonga, alipofika eneo la tukio akakuta jamaa kafariki
hivyo akawasha gari akakimbia, kumbe watu washapiga picha namba za gari yake
 
Lakini ni swali la msingi.......
Sio kweli

Skiza, maisha yana njia nyingi kwenye kila Wakati kutegemea na mazingira na hasa kwa kuwa tupo huru.
Halikuwa swali la msingi labda kwa kuwa tuko tofauti na kila mmoja anapenda apate dondoo flani kwenye habari ila sio kwa hii ya msiba
HIVI KWA MFANO ASINGESHIKWA UMAUTI HALAFU UNGESKIA TU KWAMBA BOSS WA NGORIKA ALIENDA KUANGALIA KIWANJA JANA USIKU. JE UNGESHTUKA NI KWANINI ALIENDA MDA HUO.
 
rip sir!

10254029_991012640985601_8230991028086474135_n.jpg
 
Kuna jamaa hapo kasema Steven ni Mpare!
Jamaa sio Mpare ni Mchaga! Baba yake marehem mzee Mberesero alifanya kuhamia Pale Kisangara Na Kuanzisha Mashamba Kisangara, Kiruru Na Kileo kabla ya kuruka Daraja la Kileo ukiwa unatoka MOSHI! Wanamiliki shamba Kubwa pale upande WA Kushoto! Kwa kifupi alikuw jamaa Mpole Na Mchapa Kazi San!

Na ameipeleka Kampuni Mbali sana baada ya kifo cha Baba yake!
Amewacha Wake wawili Na Watoto Kadhaa!
Mola iweke Pema Roho ya Marehem STEVEN aka. ( NGUTO )
 
kampuni yake Ngorika ndoo pekee iliyobaki kati ya zile za zamani, Majira, Rombo Investment, Mango, Star n.k.
 
Back
Top Bottom