Ujamaa system siku zote huwa laana, watu huwa wameshikiliwa akili na hakuna mwenye uwezo wa kufikiria, wenye hela zao wanafanya yao ila maskini na walalahoi wanapigwa sounds za uzalendo, yaani watu wazima wenye mindevu wanakubali kuamini kwamba hamna corona kisa rais katoa tamko kwamba haipo.
Mpaka sasa utakuta matajiri wengi wameshatoka nje na kuchanjwa kimya kimya ila maskini wanaendelea kuambiwa waimbe mapambio ya hakuna corona Tanzania, tumeishinda corona, imeshindwa na haijawahi kuwepo.
Kule jukwaa la siasa humu JF naona nyuzi za tanzia mwanzo mwisho yaani hali mbaya ila jamaa wameshupaza shingo, utakuta watu bado wanabanana kwenye midaladala na kupumuliana kisa waliambiwa corona haipo.