Tanzania yetu: Tafakari, chukua hatua

Tanzania yetu: Tafakari, chukua hatua

Mwanavisu

Member
Joined
Jan 24, 2015
Posts
26
Reaction score
22
TANZANIA YETU: TAFAKARI, CHUKUA HATUA
Haya ndio mambo tunayoyafamu kuhusu TANZANIA yetu:
1. Kwa miaka 50 hii inchi imeongozwa na ccm peke yake ambayo ni zao TANU na ASP.

2. Tz ina ukubwa ukubwa wa 945,000 km square yani sawa na uchukue Denmark, Ufaransa, Uingereza, Uholanzi na Ireland, ujumlishe zote kwa pamoja.

3. Tz ni nchi ya tatu kwa uzalishaji dhahabu afrika na ipo top 20 duniani.

4. Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani.

5. Tz ina migodi pia ya almasi,uranium kule dodoma ambao unamilikiwa na warusi,chuma kule lganga na mchuchuma mbeya ambacho kimechanganyika na tatinum ambacho kilo 1 ni karibia laki moja. Tz ina hifadhi ya kubwa ya makaa ya mawe kule Mbeya.

6. Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 kilometers bahari inaleta fursa za usafirishaji,uvuvi,utalii na nyinginezo,

7. Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda mengi duniani baada ya Marekani na Uturuki

8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza afrika) na ziwa Tanganyika ni la sita kwa ukubwa(la pili afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani.Ziwa nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani(ni la tatu afrika).

9. Tz ina mito mikubwa mingi ambayo kama vile Kagera, Ruvuma, Rufiji, Wami, Malagarasi, Mara, Pangani, Gombe, Kilombero, Mbwemkuru, nk.

10. Tz ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii duniani.

11. Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu duniani Serengeti na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro.

12. Tz ni nchi ambayo hajawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi,magonjwa kama ebola,mafuriko na vimbunga au ukame.

13. Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nnchi za Afrika zimekikosa AMANI kwa miaka yote 50 ya uhuru hajawahii kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.

14. Tz ni nnchi ambayo imepakana na nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi na DRC, ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.

15. Tanzania imechaguliwa kama Nchi ya kwanza Afrika kwa kuwa na vivutio vinavyohamasisha Utalii. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.

16. Tz ndiyo nchi ya kwanza africa kuwa na maji mengi yasiyo na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia(fresh surface water) kutokana na kuwa na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.

17. Nadhani kila mtz anajua juu ya sifa ya Tanzania kwenye swala ya kuwa na ardhi ya rutuba inayofaa kwa kilimo.

NB: Pamoja na sifa zote hizi, lakini Tz bado ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini zaidi duniani, ambazo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku.
TATIZO LENU NI NINI?
NANI ALIYESABABISHA HUU UMASKINI?
NINI KIFANYIKE? ILI TUTOKE HAPA TULIPO?
 
Back
Top Bottom