Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Tanzania imepuuzilia mbali madai kwamba baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki hayakumpigia kura mgombea Amina Mohammed wa Kenya katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika
Amina ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, alishindwa na mwenzake wa Chad Moussa Faki Mahamat, ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Tume ya AU
Akizungumza na BBC jijini Addis Ababa, Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga, amesema madai katika baadhi ya vyombo vya habari nchini Kenya kuhusu uchaguzi huo ni ya kupotosha, bali ilimuunga mkono mgombea wake wa AU.
Mahiga alizungumza na mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza ambaye alianza kwa kumuuliza kuhusu shutuma hizo wakati wa uchaguzi wa viongozi wa AU.
Chanzo: BBC