Tanzania yatengwa EAC community

Let them go... Ila watajikuta wamesahau hazina moja kubwa sana...nayo ni Tanzania! Tanzania ni kubwa kwa eneo kuliko nchi hizo zote zikiungana kwa pamoja. Ukubwa wetu ni hazina tosha. Toka lini samaki akameza mamba, hata kama huyo mamba amelala?

Mimi nafikiri MMEPANIC kusikia wenzetu wanatumwaga!Ukweli ni kwamba Tanzania ndio imekuwa kikwazo kikubwa kwa kuharakisha soko la pamoja la shirikisho la Africa mashariki.Kulikuwa na sababu kadhaa zilizosababisha kutokuharakisha huko ikiwemo elimu kuwa watanzania wengi hawana elimu hivyo watakuwa manamba wa wageni.Pia kulikuwa na hoja ya ardhi kuwa wenzetu wanahitaji ardhi yetu.Na pia kulikuwa na hoja ya ukabila kuwa wenzetu ni wakabila sana kuliko sisi hivyo kuungana nao ni kujifunza Yao.

Kiukweli watanzania tuna USHAMBA na UBINAFSI Fulani hvi,ambao unasababisha watu wadumae kifikra.Sasa kama watu hamsomi na kuzingatia elimu wakenya wakija Tanzania si ndo watawa-mobilize msome?Au kama mataifa mengine Yana ukabila si ndio tutaupunguza huo ukabila kwa kuchangamana nao(refer hotuba za Nyerere),au kama ni issue ya ardhi si ndio tutakuwa makini na kuchangamkia fursa za kumiliki ardhi na kuacha kushinda vijiweni kunywa ghahawa na kucheza draft huku tukiacha ardhi kubwa bila matumizi?

Kwanza hata yale yote tuliokuwa tunajivunia yote tulishayaacha,sasa hivi watanzania ni WADINI,WAKABILA na WABAGUZI kupita maelezo.Ni mara ngapi humu ndani tunapost thread za kibaguzi za KIDINI na KIKABILA?

Mie naona ni wakati wa kuwa waungwana na kuwaomba radhi wenzetu ili tujenge shirikisho letu vyema!Haiwezekani tunahubiri shirikisho wakati huo huo tunawafukuza nchini wenzetu na kuwaita wakimbizi na kuwaacha raia wa Oman,Syria na Egypt wamejazana pale kariakoo wakiwa n pasipoti feki!

TUACHE UNAFIKI!
 
mkuu umesema yote niliyokusudia kusema. me nikiwa mwaka wa pili pale udsm nilisoma course ya regional integration, mwalimu wetu prof. nyirabu mohabe alitueleza kwa undani namna gani Tanzania inavyokwamisha mchakato mzima wa East Africa federation. kuna waganda tulikuwa tunasoma nao pale walikua wanalaumu sana jinsi serikali ya kikwete inavyohujumu huu mchakato. sasa kwa Tanzania kutengwa nadhani ni sahihi kabisa, tuwaache wenye nia ya dhati waendelee na shirikisho, sisi tuendelee na siasa zetu za majitaka na matukio




 
Let them go they are selfish. Rwanda, Uganda and Burundi are same people. They are brothers my worry is on Kenyans. Watch out Kenyatta.
 
Jamaani kwa mtizamo wangu wa haraka mpaka hili linafikia hapa bila ya vyombo vyetu kushtukia mapema ni kosa la kubwa la kiufundi. Nilitegemea ueledi wetu na sifa tuliyonayo kwenye intellegence tungewashutikia hawa jamaa na move yao mapema na tukajihami kuliko sasa wanavyo tuchafua kwenye press kama sisi ni mazuzu. Pia nalaamu upande wa foreign policy yetu nadhani inabidi tuanangalie kwa undani ipo wapi ile diplomasia ya kitanzani tuliyezoea kuiona?matokeo yake watu wanatunyasanyasa kwenye vyombo vya habari kama mazuzu? tulikuwa wapi kusoma game na kujibu kwa diplomsia yetu?? Mimi nadhani tungejipanga vizuri tu tungesema jamaani hii kitu yenu ya EAC tupo nanyi ila kwa haya ya aridhi etc hatutaki na tunajenga hoja in a diplomatic way. Mbona Uingereza as member of EU amekataa Euro isitumike kwake. That aside..

KAMA tunaakili watanzania tuache blaa blaa sasa tuchukue hii criss au challenge kama fursa ya kujipanga kupaa tuna kila kitu tuwaonyesha kwa we can do better or became better without EAC wao wanahangaingaika kuboresha bandari moja ya MOMBASA sisi tuna MTWARA, DAR TANGA soon BAGAMOYO haya interms of wanyama tuna mbuga kubwa kuliko zao na nyingi acha MT KILIMANJARO. Haya MADINI hapa hakuna anayetupata, kwa ARIDHI yenye rutuba sio majangwa ipo. WATANZANIA TUJIPANGE wanasiasa waone mbali nina uhakika tukiwa serious ndani ya miaka mitano tutakuwa sawa na uchumi wa Malaysia au south africa issue ni commitment wajameni!
 
Mbona Ethiopia haimo katika shirikisho tangia mwanzo na sasa imepiga hatua kubwa kimaendeleo? Viongozi wetu waamue kujitoa kabisa humo na tutafanya vizuri tu kwani hawa wanaitamani nchi yetu na hakuna jingine.
 
Kama hizi habari ni kweli basi tatizo si la nchi nyingi bali sisi wenyewe.
Tunahitaji kubadilika na kuona wenzetu kama washirika badala ya kuwaona kama wanaokuja kuchukua tulivyonavyo kwani hata sisi tuna uwezo wa kujua anayechukua kilicho chetu.
Kwa Mhe Sitta kusema nchi hizo zinawaburuza wananchi ni kuchemka kwani hata sisi hatutii sahihi kwenye mikataba baada ya ridhaa ya wananchi (referandum) nani anayeweza kueleza lini wananchi wamehusishwa kutoa maoni ya kujiunga na jumuiya yoyote? SADC hatujauliza wananchi bali ni viongozi walioamua kwa niaba ya wananchi. Lililo muhimu ni maslahi ya nchi kwa ujumla.
Kavulata yeye amesema nchi za Rwanda na Uganda zinatawaliwa kijeshi. Kwa taarifa zilizo sahihi ni kuwa si Uganda na Rwanda pekee zinazoongozwa na wanajeshi. Tanzania na Burundi pia zinaongozwa na wanajeshi na mikoa na wilaya zetu zinaongozwa na wanajeshi hata wale ambao hawajastaafu mfano mzuri ni Gen Ndomba. Je hatuna raia wenye uwezo? Je kwa nini wanajeshi wastaafu na kupata tena ajira wakati watu wanahitimu na kukosa kazi?
Watu tunahitaji mabadiliko kifikra na kiutendeji. Watu hatutaki kuburuzwa.

Tuache kupotosha ukweli, inaonekana tunakimbia nyuma ya viongozi wetu kwa siasa tu si kwa faida za kitaifa.

Anjo
 
Binafsi nitafarijika sana ikiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tz hajashiriki ktk mchakato huo, kwa sababu hautakuwa na Matunda kwa nchi yetu Tanzania, Viongozi wote wa Hizo nchi ni Madikiteta kabisaa! Kagame anatuhumiwa kwa vurugu za kongo, Uhuru Kenyata na Naibu wake wana kesi ya kujibu, Museni yaleyale, Nkurunziza bado kabisa! So mimi binafsi nashukuru ikiwa Mheshimiwa Rais hajashiriki
 
nitashukulu sana kama hatutajiunga hayo mafisi yanamezea ardhi yetu mate. sadec inatosha nduguzangu Watanzania, ni bora tuungane na Mugabe kuliko hawa waloo wa ardhi za watu.
 
tofauti ya Tanzania na nchi nyingine wanachama ilianzia kwenye suala la ardhi miaka mitatu iliyopita. nchi 4 zilipendekeza kuwa wananchi wa EAC wawe huru kununua na kumiliki ardhi ktk nchi yoyote ile mwanachama. Tanzania ndiyo nchi kubwa kuliko zote na ndiyo iliyo na angalau ardhi ambayo haijawahi kanyagwa na binadamu. Tanzania iliogopa pendekezo hili kwa kuamini kuwa raia wa nchi nyingine zitavamia ardhi na kuinunua kwa pupa! jambo hili liliwakera wanachama wengine na ndiyo chanzo cha kuiona Tanzania kama kikwazo kwa umoja wa EAC. je kuhusu hili la Tanzania iko sahihi au la?
 
Huu ni usanii mtupu, ndoto za mchana aotazo mwehu. Huu ni ujanja kujifanya wanaungana ili kumvuta Tanzania naye ajiunge kwani hapa ndiye mlengwa maana hao wengine hawana cha kuunganisha. They are choka mbaya.
 
Tamaa yao ya ardhi Yetu. Inawauma. Tanzania nchi yangu LET IT GO.

Sorry kama nitakuwa nimekutukana. Mtu akikuita ww mse#@nge sio lazma uwe unaliwa kabang...hata hoja zako zikiwa haziendani na kukubalika na asilimia kubwa ya jamii yako basi unakuwa umequalify kuwekwa makundi kama mwanaharamu na hiloo nililokuita hapo mwanzo. Hoja yako inakupa sifa za kuwa m1 wao.
 

hatuwahitaji! waendelee, sisi ndiyo baba na mama!
 
Tanganyika itasimama yenyewe kama Canada alivyokata kuingia kwenye United States Of America...

Na bado tutakuwa Super Power ndani ya East Africa na Gas na Chakula watanunua kwetu
 
Yameshatokea watanzania sasa tuwe pamoja hao marais wa rwanda, uganda na kenya wanachuki binafsi tuo sadc imala
 
Kwanza yalikuwa ni makosa makubwa ya serekali kuzikubali nchi za Rwanda na Burundi kuingia katika shirikisho nakumbuka wananchi tulipiga kelele lakini wanasiasa wanafikiri wao wana akili kuliko wananchi hawakutaka kutusikiliza.


sema mkuu wakusike maana watu wakipingautasikia chadema hao!!
 
Muungano na Zanzibar tu ambayo ki Jiografia ni Ndogo kuliko Temeke , yenye wasomi wachache, most of its Populations are Incompetent when it comes to Job Market etc etc unatutoa Povu Daily Sembuse Muungano na Giant Country kama Kenya na Uganda.
Tushukuru Mungu hao Jamaa wametutenga maana wa Kenya wange hodhi Ardhi yetu yote.
Goba kwangu jirani yangu ni Kenya, ana Eneo zaid ya Ekari 11, hivi wangingizwa Rasmi Jumuiyani na sisi si Tungekoma jaman.
Hebu tushukuruni Mungu kwa Hili la kutengwa
 

Moja,mbili,tatu,inee!! Rudia hapo kwenye nne. Ine. Ahaa kumbe wewe si mtanzania! Watanzania wanasema nne na si INE, pambaf rudi kwenu wewe mnyarwanda.
 

Maoni ya kikimbizi kutoka kwa mkimbizi haram.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…