Tanzania ya viwanda

Tanzania ya viwanda

samdala

Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
37
Reaction score
1
03720ec2d2192911ccdf9ddb89b6299e.jpg
03720ec2d2192911ccdf9ddb89b6299e.jpg

Tanzania bado tuko nyuma sana katika mambo ya muhimu kama elimu,afya na technologia... kuweka nguvu nyingi kuhamasisha nchi ya viwanda naisi si wakati sahihi kufanya ilo,,,, bado tunatakiwa kuimarisha elimu, sekta ya afya na kukuza nchi katika technologia na ubunifu apo tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwa nchi ya viwanda kwa nguvu zetu wenyewe bila kutegemea wawekezaji kutoka nje. Kwa wakati huuu kama nchi hatuna technologia na watu wenye uzoefu wa kuviendesha ivyo viwanda,,, the only option itakuwa kuzinunua kwa garama ya juu na kuajiri watu wenye uzoefu kutoka nje na kuwalipa garama kubwa ili waweze endesha ivyo viwanda. Pili dunia sasaivi imekuwa kama kijiji ... competition ni kubwa sana,, je tuna uakika vitu tutakavyo zalisha apa nchi vitaweza kushindana na bidhaa kutoka mataifa mengine yenye uzoefu na technologia ya hali ya juu. Mwisho wa siku ivi viwanda vitakufa na tutakuwa tumetumia pesa nyingi ambazo tungewekeza kwenye elimu afya na ukuaji wa technologia baada ya miaka kadhaa tungekuwa kwenya nafasi nzuri ya kuviendesha ivi viwanda kwa garama nafuu .

Kwa sasa serikali inachoweza kufanya ni kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na uzalishaji,,,,, kupunguza kodi za viwanda ili kuwashawishi wenye viwanda kuhamishia production zao tanzania.,,, kama wakipiga mahesabu na kuona uzalishaji ukifanyika tanzania unakuwa wa garama nafuu watakuja tu kujenga ivyo viwanda. Apo kama nchi tutafaidika kwa kuwapatia ajira vijana wengi wanaolalamika kila siku kukosa ajira na pili serikali itapata kodi kutoka kwa waajiriwa,,, pili tutapata nafasi ya kupata uzoefu na kujifunza technologia mbali mbali zinazotumika katika uzalishaji . Baada ya miaka kadhaa tutakuwa kwenya nafasi nzuri ya kuwa nchi ya viwanda . The only way ya kuwa nchi ya viwanda kwa sasa ni kuweka mazingira mzuri ya wawekezaji., ambapo ni kwa kumake sure production cost zao zinakuwa chini ili kuwavutia kuja.
 
Baada ya miaka kadhaa tutakuwa kwenya nafasi nzuri ya kuwa nchi ya viwanda .

Mkuu;
Kutokana na upinzani mkubwa wa kisiasa, hakuna hata mmoja mwenye uhakika wa kuwepo madarakani kwa zaidi ya miaka 5 ya kikatiba. Mwenye mawazo kama yako anatamani ayaweke hayo mazingira mazuri ila ajaye naye anayafuta yote kama kwamba ni chama tofauti kimeingia madarakani. Naye anaanzisha vya kwake. Mwingine anaviuza viwanda, nyumba za serekali utadhani hakuna tena kiongozi atakaa aje hapo kuongoza. Yaani, hii ni mawazo vurugu tu. Siku zinapita, miaka, unakuta upo pale pale hivyo unaanza kuwalaumu wapinzani huku huna cha kuonesha.
 
Kama tunajipenda kweli tuboreshe kilimo chetu tule vya kwetu na kwa kuboresha elimu tutaandaa mazao yetu kwa kujenga viwanda vya kusindika vyakula vya kila aina na tujiwekee bei wananchi watakayomudu. Kutegemea wawekezaji tu umaskini utabakia pale pale. Sijui kwa nini hatuoni umuhimu wa kila mwananchi kupata elimu ya kutosha!
 
Watu wanaviogopa viwanda.hiv hamjui kuna aina tofaut za viwanda pia hata teknoloj tofauti inayotumika? Uamzi wa kujenga viwanda si mbaya kwa sasa hasa ukiangalia msimamo upo kwenye viwanda vya kusindika vyakula ambavyo haviitaji teknoloj ya juu sana hivo bas hata hii elimu ndogo iliopo inatosha kumudu aina hii ya viwanda.china inaviwanda vingi kwa sasa duniani lakin elimu yao haipo nafas ya kwanza duniani! Jibu ni kwamba wana viwanda vinavoendana na hali yao ya sasa.sipingi elimu.bali tuelewe c kila kiwanda chahitaj elimu ya juu sana.
 
Elimu tunayozungumzia ni ya mwananchi kuelewa kama analima magimbi anunue na mashine ya kusindikia ili yatumike ndani ya muda fulani badala ya siku mbili au tatu yanaharibika. Elimu tunayotaka ni mwanzisha kiwanda ajue mabaki (waste) zinapelekwa wapi zisiharibu mazingira. Elimu tunayotegemea ni ile ya mwananchi kujua akisindika zao fulani atauza wapi ndani ya nchi na vile vile nje ya nchi! Elimu kwa wote ni kila mwananchi ajue umuhimu wa usafi, chakula chenye lishe nk
 
Watanzania tupo tayari kabisa kuanzisha na kuendesha viwanda na hasa vidogo vidogo visivyohitaji technology kubwa. Tatizo ni serikali kutoipa kipaumbele cha kutosha sekita hii. Viongozi na wanasiasa wanatuhadaa sana Watanzania, maneno yao majukwaani ni tofauti kabisa linapokuja suala la utekelezaji wa wanachokihubiri.
Mheshimiwa Raisi ana dhamira nzuri sana ya kuanzisha na kuendeleza viwanda, lakini viongozi ( wasaidizi) alio nao ndio wanaomuangusha. Wengine wanapiga porojo majukwaani lakini ukiwafuata maofisini si msaada sana sana wanakumbatia wawekezaji wa kigeni kuliko sisi wazawa.
Kipaumbele kikubwa kinatolewa kwenye viwanda vikubwa, viwanda vidogo vidogo ambavyo Watanzania wazawa wanao uwezo wa kuvianzisha havithaminiwi badala yake serikali badala ya kuvisaidia kwa kutumia watalaam wake vifanye nini ili viweze kukua na kufikia viwanda vya kati badala yake wanavikandamiza kwa kuvitoza utitiri wa kodi na kuvifungia kwa kukiuka taratibu.
Nina mfano mdogo, siku chache zilizopita nilimsikia mkuu wa mkoa wa DAR ES SALAAM, mheshimiwa Paulo Makonda akisema juu ya ujenzi au uwekezaji kwenye viwanda vidogo vidogo katika mkoa wake, kauli hii ilinihuzunisha sana na ndiyo inayonipelekea nimesema kuwa VIONGOZI wetu hawana dhamira za dhati kwenye uanzishaji na uendeshaji wa viwanda na hasa vidogo na vya kati. Mimi binafsi nilikuwa na kiwanda kidogo cha kusindika chakula. Kiwanda ambacho kilikuwa kina vibali vyote vinavyotakiwa. Kiwanda hiki kilikuwa katika mkoa wa DAR ES SALAAM. Kiwanda ambacho nilikianzisha kwa mtaji wa kudunduliza na kimefanyakazi toka mwaka 2010 hadi 2016 kilipobomolewa kwenye mazingira ambayo ni tata. Nasema mazingira tata kwasababu hakukuwa na wala hatukuwahi kupewa taarifa kuwa kiwanda kiondolewe, lakini tulipewa dakika tano za kuhamisha mali na mashine na kikabomolewa. Malalamiko ya kilichofanyika niliyafikisha ofisini kwa mkuu wa mkoa mheshimiwa Paulo Makonda. Lakini hakuna chochote kilichofanyika niliishia kuzungushwa tu.
Hapa ndipo ninapohoji dhamira safi ya viongozi wetu ya kuhamasisha wananchi kuanzisha viwanda. Kama vilivyopo havisaidiwi hivyo vipya vitaanzishwaje?. Baada ya kiwanda kuvunjwa nimebaki na mashine ambazo zinazidi kuharibika kwa kukaa tu bila kufanyakazi. Kwa sababu mtaji wote uliharibiwa.
Maneno ya mheshimiwa Rais Magufuli kuwa Tanzania ilitakiwa iwe donor country, ni Watanzania wachache tunaomuelewa, ni maneno ya kweli, lakini kuna watu tuliowakabidhi dhamana ya kututumikia ndio wanaotuangusha na ndio wanaotupeleka kwenye dimbwi la umasikini mkubwa. Nilitembelea China mwaka 2015, ziara yangu ilikuwa ni kutembelea viwanda vidogo na vya kati moja ya mambo ambayo nilijifunza ni baadhi ya bidhaa ambazo zikija huku kwetu zinauzwa bei kubwa na wakati hazihitaji technology kubwa kuzitengeneza kiasi kwamba hata sisi hapa tunaweza kuzitengeneza na tukauza hata kwenye nchi zingine za Africa. Na tungetengeneza ajira kwa Watanzania wenzetu. Nikiangalia namba ya vijana wanaomaliza kwenye vyuo vikuu yetu asimilia kubwa wanasubiri serikali iwaajili. Na viongozi waliopewa dhamana hakuna ubunifu wowote wanaoufanya wa kuondoa changamoto kama hizi. Tunaojitahidi kujikwamua kidogo ndio hivyo tena tunarudishwa nyuma hatua zaidi ya 100.
Ninapenda kumalizia kwa kusema haya. 1. KWA VIJANA na hasa wasomi wetu mnaomaliza na mlioko vyuo vikuu tumuunge mkono mheshimiwa Rais kwa kufanyakazi na mtumie elimu mlioipata na mnayoipata kwa kubuni miradi ya uzalishaji mali kwa kutumia technology rahisi ili miradi hiyo iweze kuajili kundi kubwa la vijana wa Taifa hili. Pia tumieni mitandao ya kijamii kwa kuweka mada zinazolenga na kuhamasisha vijana kujitambua na kutumia muda wao mwingi katika kujadili namna na kupeana fursa za kujikwamua ki uchumi.
2. KWA VIONGOZI mliopewa dhamana na hasa viongozi vijana, tutendeeni haki Watanzania kwa kutatua matatizo yetu na hasa haya uzalishaji mali, viongozi mlio wengi mkishapata madaraka/ vyeo mnakaa mbali na wanachi na matokeo yake mnageuka kuwa watesi wetu. Watanzania tupo tayari kuwekeza kwenye viwanda ila baadhi ya sera ni kandamizi, baadhi ya taratibu zinaingiliana kati ya wizara moja na nyingine na kupelekea utitiri wa Ada, tozo, na kodi kuwa kubwa kwa mwekezaji.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wetu. Amina.
 
Umeongea point sana.tatizo lililopo ni kwamba huu mpango mzima wa viwanda haujaeleweka kiuhakika kwa watendaji na viongoz wengi serikalini.kuna ule usemi " the devil is in the details".kushindwa au kufanikiwa kwa kitu chochote kile kipo katika details.
 
Lakini cha kushangaza mkuu VIONGOZI au watendaji hawa hawa ndio wanasafiri kwenda ulaya kujifunza kwa wenzetu, ili yale wanayoyaona huko yenye manufaa kwa jamii yao waweze kuyaleta ili na jamii/ nchi yao inufaike na kupiga hatua za ki maendeleo. Lakini cha kushangaza Waziri mwenye dhamana na jambo hili la viwanda anakuja na kauli kuwa " UKIWA NA CHEREHANI TANO HICHO NI KIWANDA TAYARI." Maneno kama haya mimi nayaona kama ni dhihaka kwa Watanzania. Hatuwezi kuanzisha viwanda vidogo vidogo na hata vikianzishwa havitakua endapo tutaendelea kuwa na watendaji wenye mawazo kama haya. Kwa mawazo kama haya ambayo ni ya kiongozi wa wizara tusitegemee kuona sera nzuri zinazolenga kuvilinda viwanda vidogo na kuvisaidia vipanuke na kufikia viwanda vya kati. Kitachofuatia hapo ni viongozi haohao kutusimanga kuwa Watanzania hatuna mitaji na uwezo wa kuanzisha viwanda au kuendesha biashara flani.
Juzi mheshimiwa Rais alisema kuwa kuzaliwa Tanzania ni mtaji tosha. Ni kweli hapa kwetu fursa ni nyingi sana ila kikwazo ni hawa watendaji tulionao.
 
China kuwa na viwanda vidog vidog vingi na watu kuwa wabunifu imetokana na udhoefu walioupata kwenye viwanda vingi vikubwa vilivyofunguliwa china .... baada ya mda automatically watu waka adapt.
 
Ninakubaliana na wewe mkuu samdala Watanzania walio wengi na hasa vijana hawana mitaji ya kuanzisha viwanda vikubwa hata wakiungana, hivyo serikali isaidie kuweka mazingira rafiki ili waanzishe / tuanzishe hivyo vidogo vidogo ninaamini tunavimudu ki-mitaji.
Na ninapoongelea mazingira mazuri ambayo serikali iweke ni pamoja na kuondoa kodi kwenye mitambo na vifaa vingine vitakavyoagizwa kutoka nje kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo na hasa kwa wazawa. Serikali ipunguze ama iondoe gharama za vibali vya watalaam watakaoajiliwa kuendesha viwanda hivyo. Serikali ipunguze au kuondoa mwingiliano wa majukumu ya kiutendaji wa taasisi zake. Mfano kwenye sekita ya usindikaji vyakula utakuta kuna TFDA, TBS, WAKALA WA VIPIMO, na nyingine ambazo sikuzitaja. Hizi tatu nilizozitaja zinafanya majukumu yanayofanana. Na kila taasisi inatoza Ada za kufanya majukumu yake. Maana yangu ni kwamba kwa utitiri huu wa Kodi na tozo mbali mbali viwanda vyetu hivi vikianzishwa havitaweza kuhimili katika soko la ushindani bidhaa zao zitakuwa ghali ili waweze kukidhi gharama za uendeshaji na kupata faida. Ninayasema haya si kwa lengo la kuogopesha watu wasiwekeze bali kumsaidia mheshimiwa Rais juu ya maono yake mazuri ya Tanzania kuwa na viwanda.
Pia naomba na wengine wachangie hii mada mbona wataalam hamjitokezi hapa?
 
Mkuu;
Kutokana na upinzani mkubwa wa kisiasa, hakuna hata mmoja mwenye uhakika wa kuwepo madarakani kwa zaidi ya miaka 5 ya kikatiba. Mwenye mawazo kama yako anatamani ayaweke hayo mazingira mazuri ila ajaye naye anayafuta yote kama kwamba ni chama tofauti kimeingia madarakani. Naye anaanzisha vya kwake. Mwingine anaviuza viwanda, nyumba za serekali utadhani hakuna tena kiongozi atakaa aje hapo kuongoza. Yaani, hii ni mawazo vurugu tu. Siku zinapita, miaka, unakuta upo pale pale hivyo kuwalaumu wapinzani huku huna cha kuonesha.

Ni kweli,,,,kama nchi tunatakiwa tuwe na mwelekeo wa kitaifa,,,,iii ata aje nani inakuwa ngumu kubadilisha zaidi atakachoweza ni kuboresha na kufanya malengo ya kitaifa yaende kwa kasi,,,,, hatuwezi tukawa tunabadilika badilika kila siku,,,,,, kilimo kwanza saivi kwisha abari yake,,, nguvu zote tulizoweka na pesa nyingi zilizotumika zinakuwa hazina maana tena,,,, maana saivi tumeacha na kuamia kweny viwanda,,,, atakuja mwingine tutaama tena,,,,, ata uwekezaji unakuwa mgumu maana unakuwa auna uakika kama baada ya ii mika mitano au kumi mwelekeo wa taifa utakuwa pale pale.,,,, ... kwa mfano kuamia dodoma... kama mwekezaji unaweza ukaamua kusema ngoja nikawekeze dodoma ,,,,,lakini baada ya miaka mitano au kumi unashangaa serikali yote imerud apa dar es salaam .. inabid kuwa na blue print ya kitaifa isoyo badilika kutokana na upepo wa kisiasa
 
Back
Top Bottom