Tanzania ya miaka ya 1980

watu tulikua wangapi??? nani alikua anaogoza nchi?? nani alikua msemaji na mwenye sauti ya mwisho???
 
yaani haukuelewa alichosema? hivi mnakuwaga serious wakati mnasoma nini? meseji za mpesa?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ww mwehu kweli hutakua serious kwny txt zote ila sio ya MPESA
 

Shashi kapoor ..Amjad Khan(RIP), Rheka, kisura Zeenata Aman ..Cameo cinema. UDA walileta IKARUS toka Hungary zilikuwa ndefu LHD ..na baadae zikaja fupi pia. Enzi hizo ku drop kwenye basi ndio ujanja ...una suruali ya mchelemchele na chachacha ...Handkerchief unanininginiza nje ya mfuko wa suruali yako yenye celebrations. Enzi za ile coaster "Scaba Scuba"....safari buti aka mbwa na raba za ikarus za Bora...duu kipindi sana
 

Aisee umenikumbusha enzi zile unaenda na kitabu chako cha ration dukani kila baada ya wiki mbili kununua sukari .
Operesheni Nguvu kazi...nakumbuka polisi walikuwa wanakuja wamevaa kiraia na kama wanapiga tizi (jogging) ..halafu inapigwa filimbi wanatawanyika na wanaanza kamata watu...
 
Ukisema miaka ya 80 ndio Turn point ya Tanzania ilipoanza
Kuteka ndege ya ATC na akina Member Lee kutoka Mwanza hadi Uingereza wakidai Nyerere ajiuzuru
Vita ya hujumu uchumi kuna wahindi walimwaga pesa barabarani.
Kufukuzwa kazi makamu wa kwanza wa raisi Jumbe na kuvuliwa hadhi zote hadi akawekwa under house arrest.
Kifo cha Waziri Mkuu Sokoine kilishtua umma,ili kupoza hasira za wananchi Nyerere akamteua Salim Mohamed Salim kuwa Waziri Mkuu.
Uncle Tom alikula njama na maofisa wa jeshi kumpindua raisi Nyerere,lakini jaribio lilizimwa na watu kadhaa kukamatwa,Commando Tamimu aliepanga kumua Nyerere alipigwa risasi na kachero Mabele Marando.
Nyerere alingatuka chini ya shindikizo za nje na ndani mwaka 1985.Mwinyi akachguuliwa raisi wa Tanzania.
 
Mkuu huyo Nkapa na familia yake ndio walio filisi nchi yetu.Banks nyingi lakini inayo niuma zaidi ni ya NBC Kabla hajawapa makaburu.Viwanda alivyo vigawa kwa familia yake na wapambe wake.Watu wengi walisota wakati wa utawala wake na Bila ya kusahau mauwaji ya Wazanzibar.Yule nkapa Mungu anamuona.shenzi taipu
Ana haki ya kutuita sisi Malofa
 

Kweli kabisa,pamoja na kuelezwa NBC inajiendesha kwa faida bado akaiuza kwa bei pouwa kabisa.Kweli Mkuu tunahaki ya kuitwa MALOFA
 
Duuu wahenga nyie,mbona leo hakuna kureport ukienda sehemu au watu wamekuwa wengi mno?
 
Mwinyi hakupigiwa kura?na ilikua mwaka gani
 
Casius Clay (Mohamed Ally) alikuja kipindi hichi pia
 
Jamani endeleeni kutiririka,wengine ndiyo miaka hiyo tunakua kua!
 
Kadi za kijani za ration ya unga wa yanga na sukari zilikua ndo mpango mzima. Mafuta aina ya petrol na diesel ilikuwa kuuziwa mwisho lita 6 kwa wiki. Ukimaliza kabla imekula kwako. Magari kuendesha ilikua mwisho saa saba mchana siku ya jumapili isipokua kwa kibali maalum. Kununua gari lazima upate kibali kutoka State Motors Corporation. Ni kipindi ambacho kituo cha tv kilikua zanzibar tu. Na kituo cha redio kilikua kimoja tu. RTD. utake usitake lazima usikilize kipindi cha malenga wetu. ndio kipindi ambacho wazungu walianza kuongezeka nchini kwa gia ya expatriates na magari yao yalikua na vibao vyekundu na kuanzia na herufi TX. unaweza fananisha na DFP kwa sasa.
 
Ngoja Nikae Vzr Nipate History Nzur Ya Taifa Langu

Kiviere Wa Usangi
 
Kipindi hichi ndio nchi yetu ilikua kwenye transition kutoka siasa ya ujamaa na kuanza siasa za kibepari . Ndio kipindi ambacho utaifa ulianza kupotea na kuja kwa ubinafsi na tamaa iliyopita kiasi. Kilikua kipindi kibaya sana. Madawa ya kulevya yakaanza kuingia kwa kasi miaka ya 1985 na kuendelea. Shule za serikali zikaanza kuwa mbaya taratibu na kufanya watu wenye hela kuanza kupeleka watoto Kenya na Uganda kusoma. Maadili yakaanza kushuka kwa kasi mno.
 
Viwanja vya kujirusha Dar vilikuwa YMCA, Ushirika, Lang'ata, vision, Mbowe na Msasani club (Pamoja na Disco toto).
 
yes uchumi ulikuwa ni mzuri,services deliveries kwa wananchi zilikuwa above average,zahanati,shule,mahakama,n.k.ufanisi ulikuwa mzuri mno,unamaliza kidato cha nne unapewa form maalum ya kujaza wapi future yako itakuwa,combinations za kidato cha tano unazozitaka na kuwa na uwezo nao,mwishoni mwa 80s ninaingia pale Mkwawa CNE ni evergreen,mabweni safi kuanzia Magembe hadi Shaaban Robert W,CHAKULA SAFI NA MWISHO WA MWEZI UNALIPWA KICHELE ,yes maisha yalikuwa safi kwa familia nyingi,tatizo kubwa lilikuwepo ni mawasiliano,barabara zilikuwa nyingi hazipitiki hasa kipindi cha masika,hasa mikoa ya kusini but in general nchi ilikuwa na adabu ,uwezo wa kutembea alfajiri ya saa 8 kutoka magomeni kondoa(DDC sikinde) hadi kinondoni shamba ulikuwepo uhakika wa asilimia 99 utafika salama.yeah personal iam mic yale maisha.poleni for this generations sijui ijao.
 
Wakati mwingine Lugha yako huwa sio ya STAHA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…