Tanzania ya hofu chini ya Pombe

activisty

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
315
107
"Nchi hii sio nchi huru na ni nchi isiyo na haki"
Siyo wakwanza kuyatamka maneno haya, yamesemwa na yataendelea kusemwa na kadiri siku ziendavyo ukweli huu utaendelea na unaendelea kujithibitisha.

Sita subiri siku 100 zipite ati ndo nikosoe serikali ya Pombe, hapana siwezi nyamazia yaliyonyamaziwa kwa Mrisho mwaka 2005.Ni serikali ileile ya 2005-2010 iliyojitahidi kuvifunga mdomo vyombo vya habari kwa kuvifungia ati kwa sababu ya kuikosoa na kuweka ukweli hadharani unaohusu uozo wa serikali kiutendaji(mwanahalisi)
Haikuishia hapo, ikaenda bungeni ikashika na kulivaa bunge, miswada mibovu ikapita, bageti haba zikapita, sheria mbovu zikalindwa, na bunge likakosa tumaini na dhamira kuu. Lakini ikaenda mbali zaidi hadi kwenye bunge maalum la katiba, ikaweka makazi yake pale na hadi sasa tumeona matokeo yake kuwa katiba mpya imekuwa ndoto ya mchana kwa watanzania.

Nini nataka kusema hapa.
Kitendo cha serikali hii 2015-2020 kuanza kupita njia zile zile za serikali iliyopita huku ikitufariji kwa fukuza fukuza, ziara shtukiza ambayo kwangu naziona ni mbinu tu za kisiasa za kuhakikisha wasomi wajinga walio wengi wanaendelea kuishi kwa fikra zilizopofuka zinazowaaminisha kuwa sasa wanyonge wamepata dawa, sasa wanyonge wamepata vitanda hospitalini yani kiufupi wamepata mtetezi n.k ilihali tu ni mwendelezo wa wanasiasa kutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha kuwa wanaonekana wema na wenye kustahili sifa ndani ya jamii kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Tunalipa kodi kubwa, kipato chetu ni kidogo, ni haki yetu kupata huduma bora za afya, na huduma nyingine muhimu na wala hatuitaji kumsifu au kumtukuza mtu kwani hiyo ni haki yetu. Bunge ni sehemu ya uwakilishi wa wananchi, serikali ni ya wananchi, ni haki yetu kabisa kupata taarifa zote zinazotuhusu zinazoendelea bungeni na serikalini kwa gharama yeyote ile kwani sisi ndio tunaolipa kodi na ndio tunaolipia gharama hizo.

Tofauti na hapo basi itangazwe rasmi kuwa Tanzania si nchi ya demokrasia tena. Punguza gharama kwenye ofisi ya rais.punguza mawizara yasiyo na faida, mishahara mikubwa ya vigogo, makatibu wakuu, wakurugenzi huko ndo pa kupunguza gharama, huko ndo kwa kubana matumizi, si huku kwenye uhuru wa kupata habari.
Nimalizie kwa kusema
moja serikali hii ya sasa, kama ina nia ya dhati ya kufanya kazi basi na ifanye kazi kwelikweli iache haya maonesho ya sabasaba ya kucheza na saikolojia za watu kwa kuwapumbaza.

Pili binafsi sina imani na serikali ya ccm katika utendaji wake na malengo yake haswa kwa wananchi. Ingawa nawaona wapo viongozi wachache sana ndani ya ccm ambao wana nia ya dhati ya kuwatetea wananchi.

Tatu jicho langu la huruma ni kwa Zanzibar. Natamani kuwaona wanamapinduzi kama che guevara, wakiikomboa Zanzibar. Natamani kuwaona wanasiasa wapinzani ambao wengi ni wazuri wa kunena maneno ya ushawishi tu, wakiingiwa na mioyo ya kimapinduzi waisaidie Zanzibar. Natamani kuiona Tanzania huru na yenye haki, natamani kuiona Zanzibar ya Maalim Seif zanzibar huru na yenye haki,Natamani kuiona Tanzania imara na isiyo na hofu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

By mwanaharakati huru
Activistyi@yahoo.com
 
Mleta Uzi umesema kweli kabisa. Nawaonea huruma wafanyakazi wanaofanyakazi sekta ya umma wanavyofanyiwa na wanasiasa. Hivi watu walio wengi wanawaona Kama mashetani na wanasiasa Kama malaika wakombozi. Hii ni chuki mbaya kuliko ile ya ubaguzi inayojengwa na ccm. Hali hii ikiendelea miezi miwili ijayo serikali ita- stack Kama CD mbovu. Wanasiasa waache kuwatisha wafanyakazi wa umma.
 
wanaohofu watoke zao hii nchi sasa ni nchi ya wazalendo kubana matumizi kwenda mbele.
Nakubaliana nawe kabisaaa! Hofu ya nini kama mtu hana cha kuficha? Hofu ya nini kama alikuwa mzalendo akafuata sheria na taratibu? Hofu ya nini wakati asilimia kubwa ya wananchi hawana hofu wanafurahia kazi inayofanywa na Rais? Hofu ya nini wakati majeshi yetu yote yanaonyesha utii kwa Rais na Amiri jeshi mkuu? Mhalifu ndiye mwenye hofu! Kama mtu si mhalifu hana sababu ya kuhofu!! Uzalendo ndio kinga ya hofu!
 
Nakubaliana nawe kabisaaa! Hofu ya nini kama mtu hana cha kuficha? Hofu ya nini kama alikuwa mzalendo akafuata sheria na taratibu? Hofu ya nini wakati asilimia kubwa ya wananchi hawana hofu wanafurahia kazi inayofanywa na Rais? Hofu ya nini wakati majeshi yetu yote yanaonyesha utii kwa Rais na Amiri jeshi mkuu? Mhalifu ndiye mwenye hofu! Kama mtu si mhalifu hana sababu ya kuhofu!! Uzalendo ndio kinga ya hofu!
Raisi hana kazi anayofanya zaidi yakuendeleza movie ni serikali ya maigizo kama hujui hofu huzaa chuki na visasi taifa analojenga magufuli kwa kujua alipachikwa kwenye utawala yatamrejea hivi punde
 
78EFD972105633E89D366470F929FE_h498_w598_m2[1].jpg
Watu wamesem CCM NI ILE ILE TENA KWA KUZUNGUKA NCHI NZIMA NA WASANII AKINA PLATINUMS,THEN MKAWAONEA HURUMA KWA MANANO YA Tanzania ya Mugufuli.....wakati wamebadili suti tu hawa
 
Back
Top Bottom