Tanzania wenyeji Kombe la Mataifa ya Afrika 2009


Kibunango

Kibunango

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2006
Messages
7,712
Likes
259
Points
180
Kibunango

Kibunango

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2006
7,712 259 180
BARAZA la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) litaishauri na kuunga mkono Tanzania kuwa mwenyeji kwa mara ya kwanza wa Kombe la Afrika kwa wachezaji wasio wakulipwa.

Michuano hiyo ambayo itakuwa ikifanyika kila baada ya miaka miwili inaandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) hususan kwa wachezaji wanaochezea katika ligi zilizo nchini mwao.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye alisema Tanzania ina kila sababu ya kuuanda michuano hiyo.

“CECAFA itaongea na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwashawishi kutuma maombi ya kuwa mwenyeji wa Kombe la Afrika 2009 ambayo inahusisha wachezaji wasio wakulipwa,” alisema.

Musonye alisema sifa za Tanzania zinazowapa nafasi kubwa kuwa mwenyeji ni uwanja mpya wa kisasa, ukarabati wa uwanja wa zamani zote zikiwa Dar es Salaam na hoteli myingi za kisasa.

Alisema iwapo Tanzania itapata fursa ya kuuanda michuano hiyo, CECAFA itakuwa na wawakilshi wawili na kwamba itakuwa nafasi nzuri kuitangaza Tanzania kwa ajili ya Kombe la Dunia 2010 itakayofanyika Afrika Kusini.Musonye alisema michuano hiyo itajumuisha timu nane kutoka kanda sita. Kila kanda itawakilishwa na timu moja isipokuwa kanda moja itakayokuwa na timu mbili. Kanda mwenyeji itatoa timu mbili.

Alisema kila kanda itakuwa na michuano yao ya kutafuta bingwa atakayeshiriki Kombe la Afrika.

Wakati huo huo, Musonye alisema nchi 11 zinazounda CECAFA zimethibitisha kushiriki Kombe la Challenge zitakazofanyika Dar es Salaam kuanzia Desemba 8 hadi 22 mwaka huu.

Katibu Mkuu huyo wa CECAFA alisema mazungumzo na wadhamini yanaendelea vizuri na wiki ijayo wataweka saini na kutengeneza ratiba.

Musonye alisema wana matumaini makubwa kwamba michuano ya Kombe la Challenge yataonyeshwa moja kwa moja kwenye runinga.

Source: Dimba
 
Mtaalam

Mtaalam

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2007
Messages
1,279
Likes
43
Points
145
Mtaalam

Mtaalam

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2007
1,279 43 145
kwa viwanja vipi tulivyo navyo vya kuhost match nyingi kama zile kwa just 3 to 4 weeks?lets just kip on dreaming ndoto za saa sita mchana..
 
Kibunango

Kibunango

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2006
Messages
7,712
Likes
259
Points
180
Kibunango

Kibunango

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2006
7,712 259 180
Ipo haja ya kuwasiliana na TFF kujua kama wazo hili bado lipo
 

Forum statistics

Threads 1,238,902
Members 476,226
Posts 29,336,217