TANZANIA TUSIJIINGIZE KWENYE EPA.

TANZANIA TUSIJIINGIZE KWENYE EPA.

Tulime

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Posts
248
Reaction score
104
TANZANIA TUSIJIINGIZE KWENYE EPA, NI HATARI KWA USTAWI WETU:

Wakuu wa nchi za Afrika mashariki leo wanakutana nchini Tanzania , na miongoni mwa agenda kuu zitakuwa ni kuingia kwa Sudan Kusini kama mwana chama mpya na Kujadili kuhusu ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za Afrika Mashariki na bara ulaya,(Economic Partnership Agreement).

Sote tunajua kuwa ushirikiano/umoja siku zote ni nguvu, ila ushirikiano huu wa kiuchumi baina yetu sisi na bara ulaya una hasara nyingi zaidi ya faida.
Tuangalie tuu katika maeneo machache ambayo kwa namna yeyote ile hatuwezi kushindana na bara Ulaya kwa sababu lengo lao ni kuturudisha nyuma hatua kadhaa na si kutupeleka mbele.
Mbali na misamaha ya kodi unahitaji usafirishaji wa mazao ghafi ya kilimo yaani pasiwe na uzuiaji wa kusafirisha nje ya nchi, unahitaji pia zabuni mbalimbali katika nchi zitakazosaini mkataba huu kutangazwa katika nchi zote wanachama.... Kiukweli vipo vipengele ni hatari kwa Mapinduzi ya viwanda na ustawi wa uchumi wa Afrika hususani Tanzania tunaohitaji Mapinduzi ya viwanda

Athari nyingine kwa uchumi wa nchi zinazoendelea zitakazotokana na mkataba wa EPA ni kuwa mkataba unataka wanachama kuondoa kodi katika bidhaa zinazozalishwa katika nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya hii itatuathiri sana kwani kodi ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi kwa nchi zetu, pia tutakuwa dampo la bidhaa zao pamoja na kuathiri viwanda vyetu au kufifisha ukuaji wa viwanda hapa kwetu... Kwa maana nyingine wenyewe wanataka waingize bidhaa zao Nchini mwetu pasipo kulipa kodi, na hivi tufikilie ni bidhaa gani isiyozalishwa barani Ulaya?(Bila shaka jibu ni hapana)

Pia, kuruhusu wakulima wa nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya kuuza mazao yao hapa kwetu bila kizuizi. Wao wanatuhadaa eti tutauza kwao pia bila vizuizi.... Haiwezekani Tanzania tukashindana na Ujerumani, Ufaransa, Austria kwa ubora wa bidhaa.... Mwl alisema mkataba huu ni sawa na kuwachukua mabondia waliopo madaraja tofauti wapambane yule wa chini utakuwa umemuonea...

Ikumbukwe kua wiki iliyopita Rwanda n Kenya wamesign mkataba huo.(Kenya anadai amesaini kwa sababu anauza Maua na mirungi Bara Ulaya.)
Maslahi ya nchi yakizingatiwa ktk mkataba huo nchi haitaingia mkataba tajwa. Tusubiri kikao cha Eac summit kitakuja na maazimio gani kwasababu tayari council of ministers kilikaa kikao kilichodumu kwa masaa 10 bila kupata muafaka.
Nchi kwanza jumuiya baadae!
 
Back
Top Bottom