Tanzania tunahitaji level seat kwenye daladala kuepusha janga jingine kubwa la ajali za kujitakia linalotumaliza walalahoi wengi tulio masikini

CHIBE BOYS

Member
Apr 20, 2019
91
118
Baada ya janga la mlipuko wa gari la mafuta uliotokea jana na kuua ndugu zetu wengi walioona fursa,bado janga la kujaza daladala mpaka pomoni linatusubiri,tujiandae kwa hilo.

Mfano,daladala inatoka kituo chake ikiwa imejaa pomoni na bado njiani inapakia

Kwa mfano dodoma jiji,root zinazojaza pomoni pale pale stendi ni root za udom,swaswa,veyula

Huo ni mfano tu unaowakilisha sehemu nyingine achilia mbali mbagala,goms,tegeta hizi root zimekuwa mfano wa kitaifa

Mbaya zaidi gar zinazofanya hivyo nyingi zinafeli kupanda milima,zinahatarisha maisha ya makumi ya abiria waliopo ndani

Gari hizi zinapotoka stendi huwa zinakaguliwa na maofisa wetu wa polisi,sasa huwa najiuliza,hivi ajari zinapotokea na daladala kuonekana ilijaza watu kupita uwezo wake hawa polisi huwa wanaponaje vibarua vyao?

Daladala kujaza abiria kupita uwezo wake ni janga jingine tunalosubiri limalize roho zetu walalahoi wengi tulio masikini


IMG_20190811_052217_000.jpeg
 
Siku moja nilikuwa na rafiki yangu kutoka Kenya, wakati tukizunguka alifanikiwa kuona daladala iliyosheheni watu. Aliniuliza 'matatu yenu yanajaza watu hadi wasimame' nikamwambia ndiyo.

Alishangaa sana..
 
Mkuu bora hata hizo daladala kuliko haya ma mwendo kasi!!
Mwendo kasi zinajaza kuliko Lori la ng'ombe mkuu na kama hauko makini utapitishwa vituo zaidi ya viwili bado unaangaika kufika mlangoni!!
 
Kifo kimeumbwa and all humans are mortal beings. Kuwapo kwa kifo is a fact, Lakini hakuna kifo kisicho na sababu na lawama pia mara nyingi.

La muhimu Omba sana Mungu akujalie mwisho mwema.
 
Basi Uganda level seat jambo la kawaida sana labda kama wamebadilila hivi karibuni
Biashara ya Daladala au Matatu mnazijua
mbona mwezi mmoja tu umefilisika, Level seat haina faida, kuna SUMATRA, TRA, BIMA, kulipia Njia, kulipia Stand, si bora ukawe Baba Ntilie
Uganda hakuna kitu km hicho bila kapicha, juzijuzi tu wamepataajali usiku basi limegundulika lilijaza kuliko!
 
Mkuu kuna mambo mengi ya hovyo huwa yanafanyika kwenye hizi daladala zetu halafu hatua hazichukuliwi hii inahashiria kuna vitendo vya rushwa na tunaoumia ni sisi wananchi. Mfano kwa Mwanza kule kuna daladala za kwenda Sweya huko Malimbe ikifika jioni nyingi haziendi zinakwenda kupakia route ya Butimba hizi chache zinazobaki watu huingia kwa kugombania hivyo ni rahisi kupata majeraha ya kukatwa hata na vyuma na zinajaza kweli hata za kwenda Buswelu na Igombe zina afadhali .

Magari mengine ni yale yanayokwenda Bwiru baadhi huwa yanakatisha route njiani hayafiki ile stend mpya hivyo husababisha usumbufu kwa abiria wakati mwingine mtu hulazimika kuchukua boda ili kuwahi maana wengi wanaokwenda kule ni wanunuzi wa dagaa na mwalo upo mbali.

Sasa huwa najiuliza inamaana mamlaka husika hawalijui hili swala? Ni nani anayetakiwa kuwajibika kwa hili au wanaona ni haki kwa wananchi kunyanyaswa na watu wanaovunja shereia? hivi na wananchi wakiamua kupambana na huu udhalimu hawaoni kama kutakuwa na uvunjifu wa amani?

Tunaomba mamlaka husika mtusaidie, mambo madogomadigo kama haya ndiyo yanayofanya watu wachukie serikali yao wakati Mh. Raisi anafanya vizuri sana, basi na nyie wasidizi wake msimuangushe kuna mambo mengine hatutegemeami kama yangeendelea kuwepo chini ya utawala huu.
 
Mkuu bora hata hizo daladala kuliko haya ma mwendo kasi!!
Mwendo kasi zinajaza kuliko Lori la ng'ombe mkuu na kama hauko makini utapitishwa vituo zaidi ya viwili bado unaangaika kufika mlangoni!!
Daaa umenikumbusha mwaka 2008 nilipanda treni to Kigoma,daraja la 3.Sijapata kuona kama kuna usafiri unajaza kuliko treni,hasa kuanzia Tabora to KGM.Yaani uliposimama huwezi hata kunyanyua mguu na bado TT au Cleaner anasema treni haijaagi.Watu wanakaa hadi kwenye mabehewa nje kwa juu.Kama umeshaonaga treni za India na bongo ilikuwa hivyo.
 
Hata ulaya na Japani wanakotengeneza mabasi mijini hakuna levositi, mabasi ya mijini huchukua abiria wanaosimama, hili liko kisheria.
Mbona wenzetu wa Uganda wameweza!?nimeishi kule miaka minne daladala tulikua tunakaa levelsiti.
 
Biashara ya Daladala au Matatu mnazijua
mbona mwezi mmoja tu umefilisika, Level seat haina faida, kuna SUMATRA, TRA, BIMA, kulipia Njia, kulipia Stand, si bora ukawe Baba Ntilie
Uganda hakuna kitu km hicho bila kapicha, juzijuzi tu wamepataajali usiku basi limegundulika lilijaza kuliko!
Usibishe mkuu hata mm nimeishi kule level seat ni kawaida sana kule
 
Back
Top Bottom