Tanzania tunaanza kuwa na Makaburu weusi wasiovumilia lolote kuhusu marekebisho ya Katiba au haki za uchaguzi, wakiviona ni uvunjifu wa amani nchini!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
14,176
Reaction score
25,919
Imefikia mahali ambapo viongozi wa upinzani, viongozi wa kidini, taasisi za kijamii za ndani na nje, ofisi za ubalozi, watu binafsi mmoja mmoja au kama vikundi, nk, wakatamka jambo lolote kama mashauri au kukosoa kuhusu mustakabali wa uongozi nchini Tanzania wenye kuboresha haki, uongozi bira na usawa, jibu la viongozi wetu ni moja tu "tutawashughulikia kwa nguvu zote wanaotaka kuvunja amani yetu"

Tangu lini mapendekezo ya kuboresha utawala bora na haki na usawa katika taratibu za uchaguzi vikawa ni tishio kwa amani ya nchini, isipokuwa kwa mtu au chama cha Makaburu weusi nchini?

Na ni mtu mpumbavu tu ndani ya Tanzania ambae hadi sasa hataelewa kwamba pendekezo la badiliko lolote lenye kuleta usawa ambalo litaonekana ni tishio la kuleta ukosefu wa amani nchini! Hata kuwakosoa viongozi wa nchi siku hizi wanapoendesha nchi hii kinyume cha asili ni kutishia amani ya nchi.

Tumefikia mahali tuna Makaburu weusi ndani ya Tanzania, ambao kama ilivyokuwa kwa Afrika Kusini, wananchi kudai uboreshaji wa demokrasia na usawa imekuwa ni kutishia amani ya nchi,. Na kama ilivyokuwa Afrika Kusini, watu wanauwawa ndani ya Tanzania au kufungwa jela kwa ajili ya hilo. Makaburu walimfunga jela Mandela kwa miaka 27 kwa kudai tu mabadiliko ya katika ya Afrika Kusini ili kuleta usawa kwa kila mtu. Leo hii makaburu wa Kitanzania wanaofanana na wale wa Afrika Kusini ni hawa watu wanaojiita viongozi wetu, hususa ndani ya CCM, ambapo pia wako tayari kuwafunga jela na hata kuwaua wananchi wanaodai turekebishe mifumo ya usawa ndani ya nchi yetu kwa faida yetu wenyewe.

Wewe kama Mtanzania mwenye kuona mbele, unafikiri tunaelekea wapi kama nchi? Kama tuliwasaidia Afrika Kusini, Angola, Msumbiji, Namibia, Zimbabwe nk kuondokana na Makaburu waonezi na wauaji, wakandamizaji waovu wa demokrasia wenye mikono iliyajaa damu, na kuwa tayari kupambana vita ya ukombozi, kwa nini tunashindwa kujisaidia wenyewe ndani ya Tanzania? Kwa nini tuliyachukia yaliyofanywa na Makaburu wa Afrika Kusini kwa Waafrika Kusini, na tukajitoa muhanga kuwasaidia, lakini leo tunashindwa kuwaondoa Makaburu weusi wa ndani ya Tanzania, kwa ajili yetu wenyewe?
 
Sababu hata upinzani haujui jinsi ya kuunganisha Tanzania hasa Watanzania wa vijijini na Mjini, Watanzania wasiopiga kura, wasio na vyama wana CCM wanaotaka utawala wa haki, kweli.

Atatokea kiongozi kama Traore, Faye watakaounganisha Watanzania wote, makundi yote.
 
Sababu hata upinzani haujui jinsi ya kuunganisha Tanzania hasa Watanzania wa vijijini na Mjini, Watanzania wasiopiga kura, wasio na vyama wana CCM wanaotaka utawala wa haki, kweli.

Atatokea kiongozi kama Traore, Faye watakaounganisha Watanzania wote, makundi yote.
 
Nani alieyesema marekebisho ya usawa nchini yasubiri upinzani kama Chadema au ACT Wazalendo wayalete au Traole wa Tanzania ajitokeze? Nguvu iko ndani ya Watanzania wenyewe, wenye kujitambua.
 
Mtu yeyote nchini atakaeona siko sawa kuwaona CCM kama chama tawala kimebadilika na kuwa Makaburu weusi aniambie katika thread hii, akieleza wazi kwa nini hatupaswi kuwalinganisha CCM wanachofanya na kile kilichofanywa na Makaburu wa Afrika Kusini
 
Nani alieyesema marekebisho ya usawa nchini yasubiri upinzani kama Chadema au ACT Wazalendo wayalete au Traole wa Tanzania ajitokeze? Nguvu iko ndani ya Watanzania wenyewe, wenye kujitambua.
Unimenisoma,umenielewa? Kwanza umesema ni kujitambua. Hakuna mtu anayepinga CCM ni tatizo, hasa uongozi huu wa sasa. Ni bora wakoloni.

Muhimu zaidi ni kutambua jinsi ya kupata ushindi, hesabu, calculation, ili kushinda inabidi uunganishe makundi, uungwe mkono, upate ushawishi kupata mabadiliko.

Ni number game, siasa, you have to appeal across the board, across thee section of population, rich, poor, different party, no parties.
 

Katiba mbovu na zisizofaa daima huwa zinawanufaisha Watawala dhalimu waliopo katika nchi husika, hivyo, jaribio lolote lile la kutaka kurekebisha au kubadilisha katiba hizo Watawala hao wadhalimu huwa wanalichukulia kuwa ni tishio kubwa sana la Usalama wao binafsi pamoja na Usalama wa maslahi yao binafsi wanayopata kutokana na Ubovu wa Katiba iliyopo.

That's why unaona kwamba Watawala wa namna hiyo huwa wanamchukulia Mtu yoyote yule mwenye dhamira ya kutaka kuleta mabadiliko kuwa ni Adui yao mkubwa zaidi, Mabadiliko au marekebisho ya Katiba kwao huwa wanaona Kama ni TANGAZO LA KIFO.

Ndio maana unaona kwamba duniani kote kabisa Katiba Mpya zilizo nzuri Kamwe Huwa hazipatikani kwa njia za AMANI na za Kidemokrasia.

Ni lazima kwanza Watu wachapane mijeredi ili kushikishana adabu na kurejesha hali ya kuheshimiana ndipo Katiba nzuri ziliweza kupatikana. Uthibitisho wa Hoja hii unapatikana duniani kote kabisa ambako kuna Katiba Nzuri.

Hii ni njia chungu Sana lakini kwa bahati mbaya sana haiepukiki!
 
Andiko bora kabisa,

Alafu unajiuliza kati ya wananchi watako mabadiliko katika mifumo yetu ya sheria, kupitia katiba mpya, na hao ccm ambao hawataki nani yupo na viashiria vya kutaka kubagaza Amani ya nchi yetu .

Leteni katiba mpya, fanyeni reforms kwenye sheria mbalimbali zenye kuleta haki, muone izo kelele kama zitaendelea.

Mkiwa na sheria bora kwanza hata yeyote alie apo juu kama mkuu wa nchi mnakua mmempunguzia kazi .

Mtu akipewa nafasi anajua anaenda kufanya kazi ya kusidia nchi sio kufisidi nchi, teua ,tenguzi zitapungua , tutapata watu ambao ni smart kwa nafasi mbali mbali katika utumishi wa umma ,maendeleo lazima yaje kwa kasi maana kila mtu atatimiza wajibu wake
 
Ndugu Mwandishi sasa ni nini kifanyike? Kwa sababu kuandika hapa na ku lament haitatutoa hapo tulipo. Leta practical solutions na tuweke mikakati ya kutekeleza hizo solutions!

Mojawapo ni kuanza kudai hayo mabadiliko kwa vitendo kwa wananchi kujitokeza hadharani ila hizi za kuandika, uzi nyingi sana zimeshaandikwa na ikifika usiku watu tunaenda kulala asubuhi tunaamka tena tunaendelea pale tulipoishia jana.
 
Nadhani unasahau kwamba CCM inaelewa sana aina ya wapiga kura wa Kitanzania. Kama ilivyokuwa katika serikali ya Makaburu ya Afrika Kusini, ili utawala wa Makaburu uendelee kudumu,jambo la kwanza ilikuwa ni kuwa brainwash wazungu kwamba utawala wa demokrasia serikali ya Kikomunisti ya ANC ambayoingewachinja weusi wote. Sasa kwa kiasi kikubwa sana CCM imefanikiwa sana kuwa brain wash wapiga kura wa Tanzania dhidi ya lolote litakalotoka kwa vyama vya uinzani, hata kama ni zuri la dhahabu. CCM imewafanya watu kuwa chawa wasio na akili
 
Mkuu ume-define Makaburu weusi vizuri sana - na hapa ndipo CCM imefikia
 
Mtu yeyote nchini atakaeona siko sawa kuwaona CCM kama chama tawala kimebadilika na kuwa Makaburu weusi aniambie katika thread hii, akieleza wazi kwa nini hatupaswi kuwalinganisha CCM wanachofanya na kile kilichofanywa na Mkaburu wa Afrika Kusini


Kwahiyo lengo la uzi wako ni wana JF kutambua CCM ni wakoloni weusi, hilo liko wazi. Lengo linatakiws liwe Watanzania wote ukijumuisha Wapinzani wanawezaje kupigania maslahi, haki zao, uongozi kwenye nchi yao.
Jiulize ANC ilifanya nini kuunganisha nchi ili kushinda uchaguzi.

Walipata kura kutoka kwa wazungu, Inkatha Freedom party, wasio na vyama, section tofauti ndani ya ANC. Kuna somo hapo.
 
CCM sio wakoloni weusi, ni Makaburu weusi. Makaburu wa Afrika Kusini hawakuwa wakoloni, walikandamiza haki na demokrasia katika nchi iliyokuwa huru. Kilichofanyika Afrika Kusini 1994 ni uchaguzi uliozingatia haki na usawa, ndio ANC wakashinda. Hilo ndilo jambo ambalo serikali ya Makaburu ililikandamiza kwa miaka mingi, kama ambavyo serikali ya CCM imekuwa ikifanya hapa Tanzania, ndani ya nchi huru. Kwa hili CCM wama-qualify kuwa Makaburu weusi
 
Tumekuwa kama SA ya makaburu sasa, na wapiga debe ni Tyson, na Tumbili, Stelingi Msoga na Kizimkazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…