Tanzania taifa lenye utakaso

Tanzania taifa lenye utakaso

kibunange

Senior Member
Joined
Feb 18, 2015
Posts
165
Reaction score
148
Habari za leo wananzengo!?

Ni matumaini yangu wote ni wazima wa afya. Leo ningependa kutoa mtazamo wangu wa kiroho juu ya taifa hili teule la Mungu. Taifa lenye misingi ya utu na umoja. Taifa lililobarikiwa kwa kila aina ya baraka, ardhi, watu wapole, mimea, madini, mito, wanyama, milima, maji n.k..

Kuna maswali mengi ambayo nimekuwa najiuliza sana kuhusu taifa hili. Baba wa taifa alifuta laana ya taifa hili kwa kutokumwaga damu za watu wake na hivyo aliondoa unajisi kwenye nchi yake, aliondoa dhulma, ubaguzi, ubinafsi nk. Na kuwafanya watanzania wamoja na ndio maana leo hii taifa hili haliwezi kutumbukia kwenye hila za maadui wawe wa nje au wa ndani kwani mkono wa Mungu upo na wananchi wa tanzania.

Taifa hili ni taifa mama limechagiza ukombozi wa nchi nyingi za bara la Africa, limekuwa kimbilio la wanyonge na wote waliokimbia makazi yao sababu ya vita na dhiki mbalimbali na hivyo Mungu analiangalia taifa hili kwa jicho la huruma na upendo na hivyo kamwe hatoliacha taifa lake teule liangamie.

Amen!
 
Huo ni mtizamo wako Kibunange, lakini kwa maoni yangu Tanzania haikufuta LAANA bali ilijitafutia LAANA yenyewe kwa kitendo cha kutaifisha mali za wawekezaji. Kutaifisha mali ya mtu pasipo kosa nii DHULUMA, ni tendo lisilo la haki, ni tendo la uonevu na ni ukatili. Mwenyezi Mungu kakataza na hafurahishiwi na DHULUMA Aidha, UBAGUZI na UBINAFSI ni kansa ya Tanzania, anayebahatika kuwa kiongozi anataka kila kitu afanye yeye na familia yake tu, kuanzia ajira, biashara na fursa mbalimbali. Ndiyo LAANA kubwa hiyo. Watu wa chini wananung'unika, hawana haki kwenye Taifa lao. Mifano ya matendo ya DHLUMA, UBINAFSI na UBAGUZI ni uwiano kati ya posho/mshahara/kiinua mgongo vya Mbunge na vile vya mtumishii wa umma. Pia zipo tetesi kuwa baadhi ya wafanyabiashara /wawekezaji wamenyang'anywa pesa na mali zao, ikiwa tetesi hizi ni za kweli ni LAANA nyingine hii... Mh. Rais anajitahidi sana kupambana na haya ila sijui kama anaungwa mkono kwa dhati
 
Habari za leo wananzengo!?

Ni matumaini yangu wote ni wazima wa afya. Leo ningependa kutoa mtazamo wangu wa kiroho juu ya taifa hili teule la Mungu. Taifa lenye misingi ya utu na umoja. Taifa lililobarikiwa kwa kila aina ya baraka, ardhi, watu wapole, mimea, madini, mito, wanyama, milima, maji n.k..

Kuna maswali mengi ambayo nimekuwa najiuliza sana kuhusu taifa hili. Baba wa taifa alifuta laana ya taifa hili kwa kutokumwaga damu za watu wake na hivyo aliondoa unajisi kwenye nchi yake, aliondoa dhulma, ubaguzi, ubinafsi nk. Na kuwafanya watanzania wamoja na ndio maana leo hii taifa hili haliwezi kutumbukia kwenye hila za maadui wawe wa nje au wa ndani kwani mkono wa Mungu upo na wananchi wa tanzania.

Taifa hili ni taifa mama limechagiza ukombozi wa nchi nyingi za bara la Africa, limekuwa kimbilio la wanyonge na wote waliokimbia makazi yao sababu ya vita na dhiki mbalimbali na hivyo Mungu analiangalia taifa hili kwa jicho la huruma na upendo na hivyo kamwe hatoliacha taifa lake teule liangamie.

Amen!
unaijua historia ya Tanzania vizuri au umeandika tu kujifurahisha?
 
Sasa hivi Kuna laana imeingia ya kutekana tekana, sema ubaguzi upo wa kimakabila na kisiasa hasa serekalini
 
Back
Top Bottom