Director D
Senior Member
- Feb 24, 2016
- 192
- 229
Kama kuna kitu huwa kinaniuzunisha hapa TZ basi ni kuona idadi kubwa ya watu maarufu katika nyanja mbalimbali kama vile Michezo, Muziki, Filamu, Siasa, Utangazaji, Dini na nyanja nyingine kadha wa kadha kukosa hali ya utu wema katika kusaidia watu wanaowazunguka kwenye jamii zao, watu hawa wamekuwa ni watu wa kufanya vitu kwa maslahi yao ya kupata pesa tu na si vinginevyonevyo hali hii hutokana na ubinafsi kwa kudhani kuwa kusaidia wengine ni kuwaneemesha, kuna baadhi ya watu wakishakuwa maarufu hujifanya mungu mtu kiasi cha kutotaka kuonana na watu mtaani huu ni upuuzi san utakuta mtu tangu amekuwa maarufu hajawahi kutoa msaada wowote kwa jamii yake either wa pesa, nguvu, au hata japo ushauri, ndio maana utakuja vijana wengi wanaochipukia na vipaji vyao katika fani mbalimbal wanalalamika kuwa wanabaniwa na waliopo juu hivyo kushidwa kutusua na kubaki wakisota miaka mingi sana, nilikuwa na mengi san ya kusema juu ya hii tabia inayonikera san, Rai yangu ni kwa watu hawa maarufu ninawaomba wabadilike na kusaidia jamii zao ili kuchochea maendeleo kwenye jamii.