Tanzania nchi ya 119 kwa rushwa duniani kati ya nchi 174

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Tanzania imekuwa nchi ya 119 kwa rushwa duniani kati ya 174 ikifuatiwa na Msumbiji, taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Tansparency International.


*Kenya ya 145,
*Uganda 142.

"Kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, Rwanda imefanya vyema katika kupambana na rushwa ikishikilia nafasi ya 55, ikifuatiwa na Tanzania katika nafasi ya 119, na Uganda ni ya tatu katika nafasi ya 142. Kenya ni ya nne katika nafasi ya 145 na Burundi inashika mkia katika jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa katika nafasi ya 159."

====

Transparency International yasema rushwa ni tatizo kwa wote:
0,,18107130_303,00.jpg


Katika ripoti yake ya leo (03.12.2014) shirika hilo lilisema rushwa inaonekana kukithiri Uturuki na China na limetaka kuwepo ushirikiano wa karibu wa kimataifa kuangamiza kabisa rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Katika ripoti yake shirika la Transparency International hilo lenye makao yake Berlin Ujerumani lilisema rushwa ni tatizo kwa uchumi na kuna umuhimu wa taasisi kubwa za fedha katika Umoja wa Ulaya na Marekani kufanya kazi pamoja na nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi kuwakomesha mafisadi wasikwepe mkono wa sheria.
Katika faharasa ya 20 inayoonyesha viwango vya rushwa katika mataifa 175, China imepata alama 36 kati ya 100, Uturuki imepata 45 na Angola 19, zikiwa nchi ambazo zimeanguka kwa alama kati ya 4 na 5, licha ya uchumi wao kukua kwa wastani wa asilimia 4 katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Transparency International hutoa alama 100 kwa nchi ambayo haina visa vya rushwa na sufuri kwa nchi ambayo rushwa imeshamiri.

Kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, Rwanda imefanya vyema katika kupambana na rushwa ikishikilia nafasi ya 55, ikifuatiwa na Tanzania katika nafasi ya 119, na Uganda ni ya tatu katika nafasi ya 142. Kenya ni ya nne katika nafasi ya 145 na Burundi inashika mkia katika jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa katika nafasi ya 159.

Zaidi ya theluthi mbili kati ya nchi 175 katika faharasa hiyo zimepata pointi chini ya 50 huku Somalia, Korea Kaskazini, Sudan, Afghansitan na Sudan Kusini kwa mara nyingine tena zikishika nafasi za chini.
Mkurugenzi wa Transparency International katika mataifa yaliyo kusini mwa jangwa la Sahara, Chantal Uwimana, alisema, "Vipindi vya mizozo huchochea rushwa, kuyumba kwa hali ya kisiasa na kukosekana uthabiti kwa sababu mifumo hudhoofika au wale wanaotakiwa kuisimamia mifumo hii wanapoteza muelekeo.Si jambo la kushangaza kwamba Sudan Kusini na Somalia ambazo zimekabiliwa na vita kwa muda mrefu zinaonekana kuwa na vitendo vya rushwa iliyokithiri."
Denmark ni mfano wa kuigwa
Nchi iliyofanya vizuri kabisa na kushika nafasfi ya kwanza ni Denmark ikijipatia pointi 92, ikifuatiwa na New Zealand, Finland, Sweden na Norway, zote kwa mara nyingine tena zikiwa katika tabaka la nchi tano za kwanza aktika faharasa ya rushwa.

0,,18106309_404,00.gif

Faharasa kuhusu rushwa ya mwaka 2014

Ukraine ilipata pointi 26 na kubakia kuwa nchi inayoongoza kwa kiwango kikubwa cha rushwa barani Ulaya. Italia,Ugiriki na Romania kwa pamoja zimafanya vibaya miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zikiwa na pointi 43.
Mwenyekiti wa Transparency International, Jos¨¦ Ugaz alisema maafisa mafisadi huficha mali walizozipata kwa njia isiyo halali na kuzificha katika maeneo salama kupitia kampuni. Ugaz aidha amesema ufisadi mkubwa katika nchi zenye uchumi mkubwa haukandamizi tu haki za binadamu kwa watu masikini, bali pia husababisha matatizo ya utawala na uthabiti.
Ripoti hiyo ilizitaka nchi zinazoshika mkia katika orodha iliyochapishwa zichukue hatua madhubuti za makusudi kupambana na rushwa kwa masilahi ya umma. Ugaz aliyataka mataifa yanayoshika nafasi za juu katika faharasa hiyo yasieneze vitendo vya ufisadi katika nchi ambazo hazijaendelea.
Shirika la Transparency International liliuhimiza Umoja wa Ulaya, Marekani na kundi la G20 la mataifa yaliyostawi na yanayoinukia kiuchumi, kuiga mfano wa Denmark na kuanzisha daftari la umma linalojumuisha tarifa muhimu za wamiliki kwa kampuni zote zilizoshirikishwa.

Ripoti kuhusu viwango vya ufisadi duniani yatolewa

Afghanistan, Korea ya Kaskazini na Somalia ndio nchi zinazoonekana kuwa na ufisadi mkubwa zaidi ulimwenguni, wakati Denmark na New Zealand zikiwa ndio nchi zenye zaidi.

0,,16718804_303,00.jpg

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka iliyotolewa leo na Shirika la Kimataifa la kupambana na Ufisadi la Transparency International. Shirika hilo limesema kuwa kutokana na ukweli kwamba zaidi ya thuluthi mbili ya nchi zinaghubikwa na ufisadi, ni hali ambayo itaathiri ukuaji wa uchumi na kukwamisha vita dhidi ya umaskini na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa mujibu wa Shirika la Transparency International ¨C TI lenye makao yake mjini Berlin, kuwa karibu asilimia 70 ya mataifa yote ulimwenguni yanafikiriwa kukabiliwa na ¡°tatizo kubwa¡± la ufisadi katika sekta ya umma, na hakuna moja kati ya nchi 177 zilizofanyiwa utafiti mwaka huu iliyopata alama nzuri. Orodha ya kila mwaka ya TI ndicho kipimo kinachotumiwa zaidi kuangazia ufisadi katika vyama vya kisiasa, polisi, mifumo ya mahakama na utumishi wa umma, janga ambalo lina athari juu ya hatima ya maendeleo ya nchi na vita dhidi ya umaskini.

Maskini ndio wanaoumia

Wananchi wakiandamana Nigeria kuhusiana na kuondolewa ruzuku kwa bidhaa za mafuta
¡°Ufisadi unawaumiza sana watu maskini¡± amesema Mtafiti mkuu Finn Heinrich, na kuendelea kueleza kuwa hicho ndicho unachokiona wakati unapoziangalia nchi zilizoshika mkia kwenye orodha. Ndani ya nchi hizo, amesema mtafiti huyo, watu maskini ndio wanaoumia sana, na nchi hizo kamwe haitaweza kuondoka katika janga la umaskini ikiwa hazitapambana na ufisadi.
Miongoni mwa nchi ambazo zimeshuka zaidi kwenye Ripoti ya Orodha ya Ufisadi mwaka wa 2013 ni Syria inayokabiliwa na vita, pamoja na Libya na Mali, ambazo pia zimekabiliwa na migogoro ya kijeshi katika miaka ya karibuni.
Miongoni mwa nchi ¡°zilizopiga hatua nzuri¡±, ijapokuwa kutoka kiwango cha chini, ni Myanmar, ambako utawala wa kijeshi umefungua milango ya mchakato wa demokrasia na huku ikineemeka na nafasi kubwa ya uwekezaji, na kugeukia zaidi sheria za uwazi na uwajibikaji. Heinrich anasema hiyo ndiyo njia pekee nchi zinaweza kuepuka ¡°laana ya raslimali¡± ambako raslimali hupatikana tu kwa walio wachache na wenye uwezo. Nigeria, na nchi nyingine zenye utajiri wa mafuta bila shaka ni mifano mizuri.

Nchi zenye migogoro zinaongoza kwa rushwa

"Ugiriki imesifiwa kwa kupunguza ufisadi"

Nchi zilizoorodheshwa katika nafasi za mwisho ni pamoja na Iraq, Syria, Libya, Sudan na Sudan Kusini, Chad, Guinea ya Ikweta, Guinea Bissau, Haiti, na Yemen. Nazo nchi zilizofanya vyema ni Denmark, New Zealand, Luxembourg, Canada, Australia, Uholanzi, Uswisi, Singapore, Norway, Sweden na Dinland.

Rwanda iliyo katika nafasi ya 49 ulimwenguni imetajwa kufanya vyema katika eneo la Afrika Mashariki ikifuatwa na Tanzania iliyo katika nafasi ya 111, Kenya katika nafasi ya 136, Uganda inayokuja katika nafasi ya 140, na Burundi iliyo kwenye nafasi ya 157. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inajikuta katika nafasi ya 154 kwenye orodha hiyo.

Heinrich amesema ufisadi unahusishwa na nchi zinazosambaratika kutokana na migogoro na ambazo serikali haziendeshwi kikamilifu na hivyo watu ni lazima watumie kila mbinu kuendesha harakati zao, kupata huduma, kupata chakula na kuishi.
Mtafiti huyo amesema Afghanistan ambako majeshi mengi ya magharibi yanayoongozwa NATO yanaondoka mwaka ujao baada ya kuwa nchini humo kwa zaidi ya mwongo mmoja, ni ¡°hadithi ya kutisha¡±. Kwa sababu hawajaona mabadiliko yoyote makubwa. Nchi za magharibi zinawekeza kiasi kikubwa siyo tu katika masuala ya usalama lakini pia zinajaribu kurejesha mkondo wa sheria, lakini bado utafiti wa miaka ya karibuni unaonyesha kuwa idadi ya watu wanaotoa hongo bado ni ya juu kabisa ulimwenguni.


Chanzo: DW
 
Utandawazi umeanza kuwaharibu Wazungu taratibu nao miaka ya karibuni wameanza kuwa "makanjanja" especially kwenye mambo yanayohusiana na Siasa.

Takwimu/tafiti zao haziaminiki tena kwasababu zinaendeshwa ki-Propaganda.
 
Naona thread kipande (haijitoshelezi), lkamilishe Kwanza ndio tuanze kudadavua huo urojorojo!
 
Mnachoshangaa nini watanzania hii ndio hali halisi Kama ikulu yenyewe inaongoza kupokea rushwa huku kwenye mamlaka za chini ndio kumeoza hapafai. Serikali ya ccm ndio inaongoza kupokea rushwa unategemea nini.
 
Sijaelewa! Number moja ndo nchi yenye rushwa zaidi, au number 174
 
Mtoa mada tupe hiyo list, yaan vinara wa kula rushwa au ndio angalau rushwa hakuna?
 
Maudhui Yanayohusiana: Tarehe 09.07.2013

Ufisadi waongezeka duniani
Shirika la Transparency International linasema mtu mmoja katika kila wawili duniani anaamini ufisadi umeongezeka ndani ya kipindi cha miaka miwili hii, ingawa watu wengi wanaamini wanaweza kubadilisha hali ya mambo.

0,,16085015_303,00.jpg

Occupy Korruption Krise Krieg Protest


Kupitia kile kinachoitwa "Kipimo cha Ufisadi Ulimwenguni" cha mwaka 2013, ambacho kimechukua maoni kutoka jumla ya watu 114,000 kutoka nchi 107, shirika la Transparency International linasema ufisadi umesambaa duniani kote.
Asilimia 27 ya walioulizwa, walisema wamewahi kutoa rushwa kwa ajili ya kupata huduma za kijamii ndani ya miezi 12 iliyopita, hali inayomaanisha kwamba hakuna maendeleo yoyote inapolinganishwa na muda kama huu mwaka jana, pale ripoti ya mwisho ilipotolewa.
Hali inaonekana kuzidi kuwa mbaya katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, hasa nchini Tanzania na Uganda, ambako matokeo ya utafiti huo, yanaonesha kuwa huduma muhimu za kijamii zimeendelea kupatikana kwa rushwa.
"Kwenye eneo la Afrika ya Mashariki tuna takwimu ambazo zinaogofya sana, kama vile Uganda au Tanzania, ambako takribani asilimia 70 ya watu wanaamini kuwa ufisadi umeshamiri. Ni jambo la kuogofya zaidi kuona kwamba huduma kama vile elimu ni miongoni mwa maeneo matano yaliyoathiriwa sana na ufisadi, na hilo linayaathiri moja kwa moja maisha ya watu, maana fikiria kwamba unalazimika kutoa rushwa kutibiwa hospitalini." Amesema Lucas Olo Fernandes, afisa wa Transparency International kwa kanda hiyo ya Afrika.

Taasisi za kupambana na rushwa haziaminiwi

0,,2421989_4,00.jpg

Ufisadi wazidi kusambaa duniani badala ya kupungua.

Linalozidi kuvunja moyo, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo wa Transparency International, ni kwamba taasisi ambazo zimepewa jukumu la kupambana na ufisadi na uhalifu mwengine zenyewe haziaminiwi na wananchi.
Kwa mfano, watu katika mataifa 36 wanawaona polisi kuwa mafisadi wakubwa kabisa, kwani katika nchi hizo kiasi cha asilimia 53 ya watu walishawahi kuombwa rushwa na polisi.
Hali inafanana na hiyo kwenye taasisi za mahakama, ambapo asilimia 30 ya watu kutoka nchi 20 walishawahi kutoa rushwa mahakamani na hivyo wanaamini kuwa mfumo wa sheria umejaa ufisadi.
Hata hivyo, la kutia moyo ni kwamba, watu 9 katika kila 10 walioulizwa walisema wangelichukua hatua dhidi ya ufisadi na robo ya wale walioombwa rushwa walikataa kutoa.
Matokeo haya yanaelezea haja ya serikali, asasi za kiraia na sekta ya biashara kufanya mengi zaidi katika kuwashirikisha watu kwenye mapambano dhidi ya ufisadi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Transparency International, Huguette Labelle, serikali zinapaswa kukibeba kilio hiki cha raia dhidi ya ufisadi kwa umakini mkubwa na kuchukua hatua madhubuti kuleta uwazi na uwajibikaji. Kimsingi, serikali zimeonekana kutokufanya ya kutosha kupambana na ufisadi ndani na nje yake.


DW
 
Sijaelewa! Number moja ndo nchi yenye rushwa zaidi, au number 174

NB: Nchi zinazofanya vema kuzuia RUSHWA au UFISADI ndiyo zinakuwa za kwanza, na nchi zinazo kuwa na rushwa kubwa au ufisadi kwa wingi ndizo zinashika nafasi za mwisho: kwa mfano kwenye Ufisadi Afrika mashariki na kati; " Rwanda iliyo katika nafasi ya 49 ulimwenguni imetajwa kufanya vyema katika eneo la Afrika Mashariki ikifuatwa na Tanzania iliyo katika nafasi ya 111, Kenya katika nafasi ya 136, Uganda inayokuja katika nafasi ya 140, na Burundi iliyo kwenye nafasi ya 157. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inajikuta katika nafasi ya 154 kwenye orodha hiyo".
 
Jinamizi la rushwa laiporomosha Tanzania kimataifa-Utafiti
Hosea.jpg

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah


Dar es Salaam.Tanzania imetajwa kushuka miongoni mwa nchi zinazofanya jitihada katika kupambana na rushwa, baada ya Taasisi ya Tranasparency International (TI) kueleza kwamba imeshuka kwa nafasi nane kutoka ya 111 mwaka jana hadi ya 119 mwaka huu.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa TI, Jose Ugaz ilieleza kwamba hata hivyo, imeweza kujiongezea umadhubuti wake kwa kushika nafasi ya 33 mwaka uliopita hadi ya 35 miongoni mwa nchi 100 zilizoshindanishwa.
Takwimu hizo zinazilenga nchi 175 kwa kulinganisha viwango vya uwajibikaji na udhibiti wa rushwa katika sekta za umma na tafiti 13 zimefanywa na wataalamu mbalimbali.
Ripoti hiyo inaifanya Tanzania iliyoshika nafasi ya 119 kuwa nchi inayofuata baada ya Rwanda iliyoshuka zaidi kutoka nafasi ya 49 mwaka jana hadi ya 55 mwaka huu, ikifuatiwa na Uganda inayoshika ya 142, Kenya ya 145 na Burundi nafasi ya 159, ikitajwa kuwa nchi inayoongoza kwa rushwa Afrika Mashariki.
Rwanda imekuwa ikitajwa kufanya vizuri katika mapambano ya rushwa kwa miaka iliyopita, lakini kwa mwaka huu, imeonekana pia kuzembea na kushuka kwa nafasi moja.
Kwa nchi za Afrika, ripoti hiyo inaitaja Botswana kuwa nchi inayofanya vizuri zaidi kwa kushika nafasi ya 31, ikiwa imeshuka kwa nafasi moja kutoka ya 30 mwaka jana.
Kwa mujibu wa TI, rushwa imekuwa kikwazo kikubwa cha upatikanaji wa haki na maendeleo ya kiuchumi, pia kupoteza kabisa imani ya wananchi kwa Serikali na viongozi wao, kutokana na kukosekana kwa huduma bora za elimu na afya.
Ugaz alisema uchaguzi unaotumia fedha nyingi kwa ajili ya watu kupata madaraka ni tatizo kubwa linalofanya rushwa ikue zaidi kwa jamii.
Alipoulizwa kuhusu Tanzania kutajwa miongoni mwa nchi ambazo udhibiti wake wa rushwa unazidi kuwa dhaifu, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah alisema hawezi kuzungumzia ripoti hiyo kwa sasa hadi atakapoipitia.
kw akina na kujua kulichomo ndani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo ina dhamana ya kupitia na kuhakiki mapato na matumizi ya Serikali, Zitto Kabwe aliitaka Serikali kuipokea ripoti hiyo ya TI na kuangalia ili kubaini maeneo yenye matatizo ambayo yamekuwa yakigharimu maendeleo ya taifa kisha kuchukua hatua.
Alisema ukiacha rushwa kubwa ambazo zimekuwa zikichangia kuzorotesha juhudi za serikali katika kutoa huduma muhimu, rushwa ndogondogo pia zimekuwa na athari kubwa kwa taifa na zinakwamisha juhudi za kupamnana na umasikini.
Mkurugenzi Mtendaji wa asasi siyo ya kiserikali ya Sikika, Irenei Kiria alieleza kwamba hashangazwi na Tanzania kushika nafasi hiyo na wala hatarajii kuona mabadiliko chanya katika siku zijazo, kwa kuwa wale wanaojihusisha na rushwa hizo hasa zile kubwa wanalindwa na Serikali.
 
Kwa kweli tumezidi! Hata hatustahili kuitwa no 2 kwa Rwanda maana 55 na 119, wapi na wapi? Hata hivyo wametusamehe tu ukweli rushwa imekithiri
 
Rushwa ndio eneo pekee tunalofanya vizuri,akifuatiwa na mapenzi.
Maeneo mengine kama uchumi,siasa,utamaduni,sanaa,elimu, ni utumbo utumbo tu
 
Hapana.

Tutakuwa tumetoa rushwa ili tutoke namba za hatari.tehh tehh tehh.


Duh! Na kweli inawezekana ikawa hivyo. We fikiria katikati ya umaluuni huu uliofanyika eti ndo utafiti unatoka kuwa tuko vizuri...mawe!
 
Ukitaka kutawala fikra za watu anzisha mada kwa kuandika "utafiti unaonesha kwamba....." they just belive simple phrase..
 
Back
Top Bottom