Tanzania na watanzania

Tanzania na watanzania

seif gadafi

Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
28
Reaction score
12
MTANZANIA MZALENDO NA SAUTI YETU

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Barnard Membe anatuhumiwa kufanya kampeni nzito kwa wabunge waishambulie na kuiangusha serikali bungeni kupitia saakata la escrow. Mpango huu unaendeshwa kwa usiri na umakini wa hali ya juu huku kachero huyo wa zamani akiwatumia wabunge wa upinzani na si wa chama chake CCM.-

Taarifa zilizovuja kutoka ndani ya kambi ya Membe zinaeleza kuwa Membe anaitumia nafasi hii ya sakata la ESCROW kama fimbo ya kujiimarisha kuelekea 2015 kwa kumshughulikia mtu anayetajwa kumvurugia upepo wake wa kisiasa waziri mkuu Mizengo Pinda. Katika kufanikisha jambo hili, Membe anatumia ushawishi na hata kuwahonga fedha baadhi ya wabunge wa upinzani akimtumia mpambe wake wa karibu ambae ndiye humtumia katika kusimamia mipango yake ya urais Jack Steven Gotham.-

Mpambe huyu wa Membe ndiye aliyesaidiwa kupata tenda ya mabilioni ya shilingi ya vitambulisho vya taifa ambavyo hadi leo bado vimekua ndoto. Jack Gotham ambae ametua na kujichimbia Dodoma kwa siri kubwa, amekuwa akifanya vikao na wabunge mbalimbali ili kufanikisha zoezi hilo. Baadhi ya wabunge ambao tunawahifadhi wanaotoka vyama vya upinzani wameitwa na kupewa maelekezo maalum ya kuhakikisha kuwa wakati wote Pinda ashambuliwe, achafuliwe na kushinikizwa awajibike kisiasa kwa kujiuzulu. Baada ya maelekezo wabunge hao walipewa fedha za kimarekani USD kama posho ya kazi kufanikisha anguko la Mizengo Pinda.-

Inasemekana Membe ameamua kuendesha mkakati huu kwa siri kubwa akiwa amejificha nyuma ya kivuli cha waziri mkuu wa zamani EDWARD LOWASSA ambaye ndiye anatajwa kuwa anawatumia wabunge kumshambulia Pinda na serikali ili ajiuzulu kama njia ya kumsafishia njia ya Urais 2015. Hivyo Membe ametumia akili zake za ukachero kucheza na fikra za watu, na kufanya kampeni ya siri kumuondoa Pinda.

Aidha, Membe amekataa kuwatumia wabunge wa CCM akihofia kuwa watavujisha siri. Hadi sasa maelfu ya dola na shilingi yameendelea kutumika kufanikisha kazi hii. Taarifa za ndani zinaonesha kuwa Membe amekuwa akivujisha siri na kuwapa wabunge hao juu ya mipango inayofanywa na serikali kukabiliana na sakata hili. Chanzo cha kuvuja kwa habari hii ni baadhi ya wabunge hawa kuzungumza na wenzao wa CCM.
Mpambe wa Membe Jack Gotham amekuwa ndiye muwakilishi wa Membe katika vikao vyake vya kushawishi watu wamuunge mkono Membe. Aidha amekuwa akimuwakilisha Membe katika vikao vya kusaka pesa za kampeni. Kabla ya kutua Dodoma, Jack alikua katika ziara ya nchi za kiarabu ambako Membe anasemekana kupata fedha za kampeni ya Urais.-
Hongera Membe. Tuungane kuiangusha serikali.Endelea na moyo huo wa kuwasaidia wabunge wetu wa upinzani.
 
Back
Top Bottom