M-pesa sikutegemea kuwa utakuwa na mtazamo chanya juu ya mabenki. Binafsi naomba nipinge hoja yako kidogo tafadhali.
Kwa kukaa kwangu nchi nyingi zenye mifumo mizuri ya mabank naweza kusema yafuatayo.
1: Tanzania ina masikini wengi sana wasio na uwezo wa kusave au kutumia bank.
2: gharama za kumiliki bank account ni kubwa sana, hili nilishawahi kulizungumza kwenye supa mix ya ea radio sikumoja. Kuwa na ac unayotozwa service charge wakati hakuna faida nyingine yeyote unayopata ni ujangili. Mf, nbc wanachange sh 1200 kwa mwezi kama sercive charge, let's say wana wateja 1,000,000 hizo ni sh ngapi kwa mwezi wanapata kutoka kwetu, pia bank zote zinatunyanyasa tunapotoa pesa kwenye atm na dirishani kwa kutucharge kati ya 600 na 1000 kwa transaction, sasa bank yenye 4000 transaction per atm per day inajizolea pesa za walalahoi ngapi?
3: kiwango cha huduma kwa wateja ni sifuri kabisa kama sio hasi... Hizi bank wanazoongeza zina kazi gani kama hazijawa peoperly regulated zile zinazooperate sasa?
3: ajira ya waliosoma finance na accounts sio tu banks, ni wakati sasa wenye biashara zozote waweze kutambua umuhim wa kuwaona wataalamu wa hesabu za biashara, kwani hasara na kupotea kwa mali zao na fedha kumepita kikomo... Hii ni kwasababu hawafati business ethics na kuhudumiwa na wataalamu. Kuna watu wana biashara za mil 50 lakini hawana accountant... Wala hakuna financial advisors...nchi haiweZi kuendelea namna hii.
4: kwakuwa bank kama crdb zinatangaza profit ya mpaka bil60 kwa mwaka, ni wakati muafaka kuwapa taarifa za kibenki wateja wake wote kwa kupitia bank statements nk, lakini ni bank chachesana zinazotoa huduma hizi. Hii ni kwasababu wanaibia sana watu mpaka kuangalia salio kwa atm ndio maana wanashindwa kuwahabarisha raia. Na bot imekaa inayajua haya na inaendelea kusajili bank kufanyaje ziendelee kufunguliwa.
5:mtazamo wangu ni mpana sana, nikisema niandike yote hapa tutakesha...bank zinacharge cash books, kuangalia salio, kutoa pesa, na bado huduma mbovu, we kaweke laki moja kwenye ac, halaf kaangalie baada ya mwaka umebaki na ngapi utashangaa, unaweza kukuta uko overdrawn...
Nina mengi wakuu, ila ntaua keyboard ya simu hapa kwa kutype gazeti... Gggrrrr.