Tanzania na Utajiri wa Marais wa Sifa Tofauti

Rulleger

Member
Aug 29, 2015
84
60
Ebu tujipe nafasi ya "siasa nyepesi" na tumwangalie Rais wetu katika mtazamo wa kihistoria tukimlinganisha na Marais wengine. Baadhi ya watu wanapata shida kumwelewa Rais Magufuli. Japo amekuwa maarufu na kupendwa sana bado yuko tofauti sana na marais waliopita.

1. Anafanana na Nyerere katika kuwajali wanyonge, kupinga rushwa na kuleta nidhamu ya uongozi kazini. Hata hivyo wanatofautiana sana pia. Magufuli hana mvuto wa hotuba, hayuko karibu na waandishi wa habari na hana umaarufu katika jukwaa la kimataifa kama Mwalimu.

2. Magufuli anaamini katika uwekezaji na soko huria. Hii ndo sifa pekee inayomfananisha na Mwinyi. Lakini wawili hawa wako tofauti sana. Magufuli hana Kiswahili cha Mwinyi, hana tabasamu ya Mwinyi, na hana sera za Ruksa katika soko huria.

3. Magufuli ana tabia moja tu sawa na Mkapa. Kujiamini na kusimamia anachoamini bila kujali media - mmeona ishu ya sukari na Bunge live. Hata hivyo hafanani na Mkapa katika sera ya uwazi na ukweli. Mkapa alileta Bunge live Magufuli kaondoa.

4. Magufuli na Kikwete wana Sera moja ya uchumi - Magufuli karithi hiyo sera bado haijabadilika. Wanatofauti nyingi tu. Kikwete mtu wa smile na kuchukulia mambo kirahisi, Magufuli ana sura ya kazi na kila jambo linapewa uzito. Kikwete mwanadiplomasia Magufuli hapana. Kikwete alikuwa soft kwa maafisa wake, Magufuli very strict. Kikwete anapenda michezo Magufuli anaweza asiende uwanja wa taifa kwa miaka mitano ijayo.

Hata Hivyo Magufuli ana sifa 3 ambazo wote waliomtangulia hawana. Kwanza yuko results-oriented. Anachotaka nikuona matokeo ya haraka ya utendaji wa serikali yake. Pili anajali efficiency katika matumizi ya resources - afikie malengo kwa gharama ndogo. Tatu ni msimamizi mahiri asiyechoka katika kusimamia principles zake. Yuko very strong katika hilo. Hata Mwalimu hakuwa that strong. Anafana na Sokoine na Mrema (enzi zake) lakini hawa hawakuwa marais.
 
nyie mpeni sifa mutakazo lakin atatukumbushs enzi za mwalimi na maduka ya kijiji siku sio nyingi.bado watanzania hamuoni.nch imesimama hakuna kinachoendelea?
 
Back
Top Bottom