aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 828
- 1,209
Tanzania ni nchi iliyojaliiwa kuwa na utajiri mkubwa wa mali asililia na hali ya hewa ya wastani yenye kupendeza, mvua zinazonyesha na kustawisha miti, mito na maziwa ya maji safi, ardhi pana za kulimia zenye rutuba, misitu mikubwa, mbuga zenye wanyama mwitu wengi na bahari yenye samaki wa kila aina.
Katika maliasili kuna migodi ya kutoka dhahabu hadi almasi na Tanzanite. Hali kadhalika ni nchi inayosifika duniani kwa usalama na kwa serekali inayojinata ulimwenguni kuwa haina dini na kuwa inazihishimu dini zote bila mapendeleo.
Lakini, kwa sababu ya nguvu na sauti kubwa walizonazo Wakristo wenye msimamo mkali wa udini, tunashuhudia kuwa serikali imelazimishwa kuwa na mapendeleo makubwa kwa watu hawa na msimamo wao mkali dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Hii ni khatari kubwa inayoisukuma Tanzania mahala pabaya sana, katika kitabu hiki tutaonesha waziwazi kadiri gani serikali ya Tanzania imeachilia siasa za huo msimamo mkali wa udini dhidi ya wananchi wa Kiislamu kutapakazwa mpaka katika shule bila ya kizuwizi chochote.
Tokea Waislamu walipokuwa wananung'ung'unika pembeni mpaka imefika hadi kulalalmika hadharani.
Kama hawa wachache wenye nguvu za dola wenye msimamo mkali wa udini wataachiliwa waendelee kutapakaza sumu za siasa zao dhidi ya Waislamu, na serikali itaendelea na mwendo wa mbuni wa kuyafumbia macho mambo haya ambayo ni khatari iliyoikabili nchi, basi tusistaajabu tukija kushtukia vita vya maneno kugeuka ghafla na kuwa vita vya kutowana roho baina ya wananchi wa dini hizi mbili kubwa kama ilivyokwisha kutokea na vinavyoendelea kutokea katika nchi mbali mbali ulimwenguni.
Mambo ya dhulma hayawezi kuendelea, lazima patatokea mripuko iwapo hapatatokea wenye busara na uadilifu watakaoyandosha haya kwa upesi sana; na kama haya niliyoyaeleza kwa mukhtasari juu ya hali ya udini iliyotanda Tanzania na khatari zake hayakutwangi akilini mwako, basi endelea kusoma asaa ukaelewa.
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nasikiliza na kusoma madukuku ya Waislamu Tanzania na mijadala baina yao na Wakristo, na kutokana na haya nikawa najadiliana baina yangu mimi na nafsi yangu nini cha kafanya.
Mimi nilikuwa najiambia kuwa hii khatari unayoiona iliyoikabili Tanzania isikushugulishe kwani huna uwezo wa kuubadilisha chochote, maana Watanzania wameshaingia katika vita vya maneno na hawana budi mwishowe watoane roho.
Kwa upande mwengine, nafsi yangu inaniambia kuwa ni dhambi kubwa mumwona mtu anaelekea kutumbukia shimoni na ukanyamaza kimya usimtahadharishe na maafa yaliomkabili, na kama utasikilizwa au utapuuzwa hayo si yako wewe tena maana umeshatimiza wajibu wako wa kutahadharisha.
Wala kuwa katika watakaokusoma wako watakaokupigia makofi na kutaka upewe tunza kubwa na pia kuna watakapo kushambulia vikali sana na kutaka utokomee, haya pia si yako tena na yasikushughulishe.
Iwapo Yesu aliyekuja na ujumbe wa salama na amani walimtenda walivyo mtenda, wewe ni nani mbele yake? Basi timiza wajibu wako.
Katika kitabu hiki tutaonesha wazi kabisa mifano ya propaganda za siasa kali za udini zenye muelekeo wa Vita vya Msalaba zilipoanzia na kupaliliwa, lakini hatutayajadili sana maandishi ya kipropaganda yaliomo vitabuni na kwingineko, kwani haya yatahitaji kuandikwa kitabu kingine.
Tutazungumzia zaidi kukhusu picha ambazo si za Kamera bali ni za ubujifu wa kuchora.
Picha ambazo zimo katika vitabu vya shule za Tanzania zinazotumiwa kasomesha vijana historia yenye ukweli finyu na mengi yasiokuwa ya kweli kwa lengo la kupalilia fitna dhidi ya Waislamu na dini yao.
Wavyele (wazee) wetu hawakukosea walipotuachia msemo usemao "kuona si kusikia" kwani picha aghlabu huacha athari kubwa zaidi katika bongo za watazamaji kuliko maelezo ya jambo hilo hilo, khasa picha zikionesha waziwazi uhabithi hata ukiwa unatokana na ubunifu wa kipropaganda wa mchoraji na hauna msingi katika matokeo ya kweli.
Na hivi ndivyo propaganda zinavofanya kazi kubwa khasa katika bongo za vijana wadogo shuleni. Halikadhalika, hawakukosea wavyele wetu waliponena "udongo upatilize uli maji."
Mimi nashindwa kuelewa vipi serikali ya Tanzania, ambayo inajinata ulimwenguni kuwa haipendelei dini yoyote bali inazihishimu dini zote sawa sawa bila mapendeleo, ikafika hadi kuwaachilia wachache wenye msimamo mkali wa udini kutapakaza sumu zao kali za propaganda mpaka shuleni! Hii ndio sababu moja ya kukiandika kitabu hiki.
Natumai baada ya wahishimiwa wakhusika kunisoma kwa makini niliyoyaandika watachukua khatua za busara, haki na uadilifu na kuyaondosha yote yale yasiyokuwa na ukweli pamoja na yale yaliyokuwa na ukweli finyu na uwongo mwingi na pia yenye fitna za kipropaganda zilizotopea dhulma na khatari.
Tuombe kuwa wakhusika hao hawatakuwa katika washiriki ambao wanaipendelea Tanzania izidi kutekwa na wenye siasa zinazoitokomeza Tanzania kubaya.
Ninaelewa fika kuwa wenye siasa kali za udini hawatakubali kwa urakhisi kuuwacha mwendo wao maovu na tusistaajabu wakifikia hadi kunishambulia mimi binafsi; mkiyaona haya yanatokea, basi juweni kuwa hiyo ni alama kubwa kwa watu muflis wa hoja na kweli hawaitakii mema Tanzania, kwani ni wapungfu wa akili na hawana mapenzi ya kweli na Tanzania.
Tanzania haikukumbwa na siasa kali za udini peke yake, bali imekabiliwa na siasa chafu za ugozi, yaani kumbagua mtu kwa asili yake. Tutaeleza na kuyanakili maneno yao wenyewe magogo wa siasa wa Tanganyika ambao hutapakaza chuki za ugozi zinazopalilia fitina baina ya Wazanzibari ili wapate kuendelea kuitawala Zanzibar vizuri ili, hatimaye, waimeze kabisa kabisa na kuigeuza mkoa wa Tanganyika;
Na kwa mujibu wa kauli zao wenyewe, sababu yao kubwa ni kuwa Zanzibar ina Waislamu wengi sana; na ni huo Uislamu wao Wazanzibari ndilo jambo kubwa linalo wachukiza wenye siasa kali za udini.
Kwa hiyo tutaigusia mada hii na kuonesha kadiri ya athari zake zilivyokuwa mbaya kwa watu wa Zanzibar na nchi yao.
Kwa dasturi yangu huwa sipendi kuzungumza juu ya ukabila ila pale ninapoona kuwa haki ya watu fulani inadhulumiwa kwa siasa chafu za ubaguzi.
Tutaonesha humu vipi uonevu huu na dhuluma za siasa za kigozi zilivyotumiwa vibaya Zanzibar hata ikafika kuwauwa bure watu wengi sana wasiokuwa na hatia yoyote kwa sababu ya kutokana na asili fulani;
Pia watu wengi wameuwawa kwa sababu walikuwa wanachama wa vyama vya Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na Zanzibar And Pemba People's Party (ZPPP).
Hivi karibuni tumeshuhudia maradhi haya yalivyomwagwa hata katika bunge maalum la katiba. Yale ya wananchi kubaguliwa, ambayo ni wajibu yakemewe vikali sana, yamekuwa yanapaliliwa na kupigiwa makofi na wanasiasa waovu.
Pengine kuna watakaopendelea kuujua msimamo wangu wa imani umeelekea wapi? Mimi ni Muislamu mwenye kuamini Mungu Mmoja na tokea utotoni mwangu waalimu wangu vyuoni na skuli na wazee nyumbani wamenifunza kuwa Wakristo na Mayahudi wameteremshiwa vitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu huyo huyo mmoja, wameteremshiwa Mitume wa kuwafundisha watu maagizo yake;
Hivyo basi, wote wanaofuata maagizo ya Mwenyezi Mungu sawa sawa ni ndugu wa kiimani, na huu ni udugu mkubwa zaidi kuliko wa kidamu au hata wa kudai wanafuata dini moja huku hawafuati amri na maagizo yake Mola Mkwasi.
Kuna watu wema wanaofuata dini zao sawasawa na pia kuna watu waovu ambao hudhania kuwa wanafuata amri zake Mola wetu, lakini kwa kweli ni wafuasi wa wa mafunzo ya Sheitani. Watu wema ni watu wema wawe wa dini yoyote na watu waovu ni watu waovu wawe wa dini yoyote ile. Kama watu wema wenye kupendelea viumbe wenzao mema hawashikamani, basi waovu wenye kumfuata Sheitani watashinda na watatawala.
Pili nimekulia na kuishi Shangani, Unguja ambako tulikuwa na majirani wengi wa Kigoa ambao walikuwa Wakristo na pia Wahindu wa Maparisi na Wasiloni (Wasrilanka) na wengineo wenye dini mbali mbali; tukicheza pamoja na kuingia nyumbani mwetu na nyumbani mwao bila ya ubaguzi.
Wengine mpaka leo tunaandikiana kidugu kabisa. Lakini lililonisaidia sana ni msingi nilioupata utotoni kwa wazee na vyuoni kwa walimu wanaopendelea haki sawasawa kwa binaadamu wote na kukataza maovu na ubaguzi na dhulma.
Kwa hivyo sina chuki na mtu yeyote ambae ana imani yoyote yenye kufuata maamrisho mema yenye kuwatakia watu wote mema, na sina udugu na wale wenye siasa za ubaguzi na udini.
Naamini hivi sasa Tanzania ipo haja kubwa sana, Khususan kwa Waislamu na Wakristo wema wenye kufuata maagizo mema ya dini zao, kuungana na kupinga propaganda za udini na za ubaguzi.
Bila ya shaka yoyote ile, wanayokhubiri na kuyatapakaza wenye siasa kali za udini yanakwenda kinyume na kiini cha maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Mafunzo ya Yesu Kristo na Mtume Muhammad (S.A.W.)