Uliza_Bei
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 3,216
- 990
Ni kwanini nchi yangu haitumii majeshi na vikosi vya ulinzi na usalama katika vyombo na taasisi zake nyeti?
Nimekuwa nikijiuliza, ukipita barabara kuu ya Mbeya au Mwanza kuja Dar Es Salaam huoni askari na wanajeshi (JWTZ) wa kutosha barabarani.
Pia nimekuwa nikijiuliza kwanini hatuoni katika taasisi mfano: TRA, TPA (Bandari), Maabara zake Kuu, TFDA, TBS, Airport, TANESCO na vitengo vya Hospital kama Muhimbili nakadhalika, n.k.
Hili ni tatizo kubwa sana la kushindwa kutumia majeshi yetu vilivyo.
Katika maeneo haya nyeti, watumishi wasiowaaminifu hupata mwanya wa kuhujumu serikali na nchi kama hawakudhibitiwa na vyombo vya dola.
Tujifunze Ulaya na Marekani waliofanikiwa; hata siku moja hawamwachi mtumishi katika vyombo hivi nyeti ajimwage kufanya kila alitakalo.
Intelijensia yetu hapa haioni ama kwa makusudi imeamua kufumbia macho ili serikali iweze kuhujumiwa.
Natoa wito kwa serikali ya MAGUFULI, kama tunahitaji ufanisi katika haya mambo ni lazima tuige wenzetu wanafanyaje. Taasisi nyeti hazitakiwi kuachwa bila udhibiti.
Kwa kawaida maeneo kama niliyoyataja, serikali inakuwa na vijana wake wa intelijensia waliosoma mambo husika na wanaajiriwa humo.Lakini pia serikali inakuwa na inakuwa na wasiowataalam katika eneo hilo wakibaki kuwa wanajeshi ama askari na unifomu zao kwaajili ya kuangalia kila kinachotendeka.
Mfano, wanaweza kuwa wasindikizaji nyuma kila linapotendeka jambo fulani; watu wa intelijensia wananielewa na mimi sitaki kwenda kwa undani zaidi.
Siingii ndani zaidi kulielezea jambo hili kwavile natambua serikali hata kama itachelewa kulichukua bado huko mbeleni itaamua kulifanyia kazi.
Nimekuwa nchi za wenzetu Ulaya na Marekani na nimeshuhudia hilo. Nimekuwa hapa katika ofisi zetu nyeti kadhaa na sijashuhudia hilo.
Haya majipu mengi yametokea kwa kukosa udhibiti, na yapo mengi na kwavile hayajaanza kudhibitiwa bado tunaona haya yakitokea.
Kwa nia nzuri naomba serikali iweke uangalizi wa kiintelijensia lakini pia wa wazi kiusalama katika maeneo yote nyeti itapunguza uvujaji wa siri na pia wizi na uhujumu unaoweza kudhibitiwa.
Nawasilisha.