hazole1
JF-Expert Member
- Jan 3, 2015
- 4,319
- 3,916
kuna utapeli mwingi ambao nimewahi kuusikia hapa tanzania lakini huu umenistua kidogo.
na umenifanya niamini kwamba tanzania nayo inaweza ikawa ipo kwenye listi ya nchi zinazongoza kwa utapeli afrika ukiachilia mbali nigeria na south afrika.
hao wanakuambia ktk afrika ndio mababa wa utapeli.
kuna jamaa mmoja tunaishi naye huku kwetu alikuwa anagrosari ya kuuza pombe. kuna siku moja kuna jamaa mmoja ambaye alikuwa hawafahamiani alimfuta ofisini kwake akaagiza bia. na wakati wanaendelea kupiga stori yule jamaa akamuuliza yule muuzaji kwamba ww hapa kwa siku huwa unauza sh. ngapi? mwenye grosari akasema hapa kwa siku mm huwa nauza laki moja
jamaa akamuambia mm ninadawa yangu ya biashara ambayo nikikupa kwa siku moja utakuwa unauza milioni 1
ila akamwambia kabla sijakuuzia dawa yangu nataka uijaribishe kwanza kama inafanya kazi.
kweli jamaa akampa dawa na jamaa alipo pewa dawa siku ya kwanza kweli akauza milioni moja siku ya pili akauza milioni 1 na siku ya tatu akauza milioni 1.
kweli siku ya nne jamaa akamfuta akamuambia umeiona kwamba dawa yangu inafanya kazi yule
jamaa akasema kweli nimeamimi dawa yako ni kiboko.
sasa jamaa akamwambia mm dawa yangu nauza milion 15 wakashushiana wakafikiana hadi milioni 12. jamaa hela aliyo kuwa nayo ikawa haitoshi ikabidi akope auze na shamba.
hela akampa jamaa.
siku ile amempa jamaa kesho yake jamaa akaenda kufungua ofisi akauza laki moja. na muda huo huo ajakaa sawa akashangaa kuna jamaa anakuja anamuulizia kwamba yule jamaa ambaye tulimkuta hapa siku ile yuko wapi kwamaana yule jamaa alikuwa anatupa hela tuwe tunakuja kunywa pombe hapa.
jamaa akaja kustuka kwamb tayari ameisha tapeliwa.
najua kila mtu amewahi kuibiwa au kutapeliwa na huyo ni mmoja katika wale wengi ambao wamewahi kutapeliwa au kuibiwa.
wapigaji wanakuambia duniani kuna mapigo 360 na kila siku wanagundua mapigo mapya.
je wewe ni utapeli gani ambao umewahi kukuacha kinywa wazi?