Tanzania inawahitaji watu aina ya Mch. Gwajima walau kumi hivi

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,998
20,354
Spin Doctoring ni taaluma ya juu sana katika Ujasusi na ili mtu ujifunze ni lazima uwe na kipaji cha hali ya juu cha maswala hayo, ambacho kimsingi mtu huzaliwa nacho.

Nchini Marekani kuna mtu anaitwa Bob Bekwen, huyu ni jasusi wa CIA, hutumiwa kwenye maswala mengi ya ku-spin mambo mengi ndani na nje ya USA hasa kubadili hali ya upepo wa kisiasa.

Nchini Urusi kuna mtu pia anaitwa Lavrov kwa sasa ni waziri wa Mashauri ya nje, huyu ni jasusi wa shirika la ujasusi la FSB, huyu anatumika zaidi kwenye mashauri ya kidiplomasia.

Uingereza ina mtu anaitwa Tony Blair, huyu amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Nchi hiyo, lakini kwa sasa anatumika kama special spinning doctor ndani ya shirika la Ujasusi la nchi hiyo la M16, na vilevile anatumika kwenye misheni iitwayo "IC" ya nchi hiyo ndani ya G8, katika hilo ameweza kusaidia taifa hilo kwa kiwango kikubwa.

Tanzania pia imekuwa na spinning Doctor wazuri wengi japo sio "majasusi", mathalani Dr Slaa, Tundu Lissu, Zitto Kabwe, John Mnyika, Godbless Lema, Salumu Mwalimu nk. Pia yupo bingwa wa wote Tanzania, huyo sio mwingine ni Abdulrahman Kinana, huyu ni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania, ametumia kwa ufanisi mkubwa kipawa chake katika siasa za kijana kwa nyakati zote ndani ya chama hicho, lakini kipawa chake hakikuwahi kuwa na mafaa kwa nchi ya Tanzania zaidi ya angamizo tu.

Ingizo jipya katika medani hizi ni Mchungaji Gwajima huyu ni mmoja ya watu wachache duniani ambao ni special Spinning Doctors ambao taifa limebahatika kuwa nao. Haimaanishi yeye ni jasusi, lakini tendo alilolitenda lina sura na haiba ya kijasusi.

Kwa uwezo wake wa ku-spin mambo, Gwajima ameweza kubadili upepo wa kisiasa ndani ya CCM, na sasa wamebaki kuhaha kumzima, lakini kundi lililonufaika na spinning hizo ambalo kimsingi ndio la wafanya maamuzi ndani ya chama wala halina presha, yaani limeshinda na 23/07/2016 litafunga kitabu cha nyakati za siasa za ubwa.
 
Andiko lako lote limejengeka katika msingi wa hisia huku maelezo mengine yakionyesha hufahamu hata maana ya neno jasusi na msingi wa ujasusi.

Tatizo letu kubwa watanzania ni kudhani tunafahamu mambo mbali mbali kiasi kwamba tunapuuza kutafuta elimu na matokeo yake ni kujenga hoja kwa kudhani/hisia badala ya kutafiti au kutegemea utafiti.

Unakuta kuna watu wanaitwa wachambuzi wa masuala mbali mbali lakini hawana hata elimu inayotambulika kimataifa kuhusu eneo wanalolichambua.

Unakuta mtu hafahamu hata maana ya demand and supply lakini unamuona amekaa mbele ya television akichanbua mambo ya kiuchumi huku shingo imeshupaa.

Wewe huna hata elimu ya ujasusi lakini eti unachambua masuala ya kijasusi. Gosh!
 
Kwahiyo ndugu Yeriko huoni ndugu Gwajima hana sura halisi ya anachokifanya,au mambo ya kubadili gia angani ameamua kuji twist upande wa kijani mwaka huu?
 
Kipi unakijua katika ujasusi ndugu, umetajwa tu na kukurupuka mkuu
Andiko lako lote limejengeka katika msingi wa hisia huku maelezo mengine yakionyesha hufahamu hata maana ya neno jasusi na msingi wa ujasusi.

Tatizo letu kubwa watanzania ni kudhani tunafahamu mambo mbali mbali kiasi kwamba tunapuuza kutafuta elimu na matokeo yake ni kujenga hoja kwa kudhani/hisia badala ya kutafiti au kutegemea utafiti.

Unakuta kuna watu wanaitwa wachambuzi wa masuala mbali mbali lakini hawana hata elimu inayotambulika kimataifa kuhusu eneo wanalolichambua.

Unakuta mtu hafahamu hata maana ya demand and supply lakini unamuona amekaa mbele ya television akichanbua mambo ya kiuchumi huku shingo imeshupaa.

Wewe huna hata elimu ya ujasusi lakini eti unachambua masuala ya kijasusi. Gosh!
 
Andiko lako lote limejengeka katika msingi wa hisia huku maelezo mengine yakionyesha hufahamu hata maana ya neno jasusi na msingi wa ujasusi.

Tatizo letu kubwa watanzania ni kudhani tunafahamu mambo mbali mbali kiasi kwamba tunapuuza kutafuta elimu na matokeo yake ni kujenga hoja kwa kudhani/hisia badala ya kutafiti au kutegemea utafiti.

Unakuta kuna watu wanaitwa wachambuzi wa masuala mbali mbali lakini hawana hata elimu inayotambulika kimataifa kuhusu eneo wanalolichambua.

Unakuta mtu hafahamu hata maana ya demand and supply lakini unamuona amekaa mbele ya television akichanbua mambo ya kiuchumi huku shingo imeshupaa.

Wewe huna hata elimu ya ujasusi lakini eti unachambua masuala ya kijasusi. Gosh!

Kama wewe hujui kitu usidhani wengine nao hawajui kama wewe ulivyo. Kitu kama hujui uliza uelimishwe. Siyo kukosoa bila kutoa maaana halisi unayoijua wewe kama mtoa mada unadhani hajui. Tuambie basi wewe mwenye kujua. Kama una uelewa mdogo usifikirie watu wote duniani wana uelewa mdogo. Nakupa pole kucritisize kitu ambacho hata wewe hukijui.
 
Mkuu hii ndio jamii ya vijana wa tz tulionao, wanaoshughulika na mleta hoja badala ya hoja.
 
Andiko lako lote limejengeka katika msingi wa hisia huku maelezo mengine yakionyesha hufahamu hata maana ya neno jasusi na msingi wa ujasusi.

Tatizo letu kubwa watanzania ni kudhani tunafahamu mambo mbali mbali kiasi kwamba tunapuuza kutafuta elimu na matokeo yake ni kujenga hoja kwa kudhani/hisia badala ya kutafiti au kutegemea utafiti.

Unakuta kuna watu wanaitwa wachambuzi wa masuala mbali mbali lakini hawana hata elimu inayotambulika kimataifa kuhusu eneo wanalolichambua.

Unakuta mtu hafahamu hata maana ya demand and supply lakini unamuona amekaa mbele ya television akichanbua mambo ya kiuchumi huku shingo imeshupaa.

Wewe huna hata elimu ya ujasusi lakini eti unachambua masuala ya kijasusi. Gosh!
mkuu umenena jambo la msingi sana
 
Omba uelekezwe nini kinaongelewa hapa sio kuleta majungu.
 
hakuna uhalisia wa hicho ulichokizungumza, Mch Gwajima hana uwezo wa kusababisha hicho kitakachoenda kutokea 23/07/2016 Ndani ya CCM, Kifupi CCM kama chama kikongwe huwa wana taratibu zao ndio maana hata Olesendeka msemaji wa CCM alishamkanusha GWAJIMA na kumuita mchochezi na suala la uenyekiti wa CCM kila mtanzania anajua utata wake sio GWAJIMA pekee kwani hata magazeti mengi ya tanzania yalizungumzia hili suala.

Naona pia unauelezea ujasusi kwa namna na fikra za kufikirika kama ambavyo kwenye vijiwe vya kahawa wanauzungumzia, unajaribu kufananisha kazi za CIA, M16 Labda na KGB na wanasiasa wa bongo! hapo uko wrong bro.

alichokifanya Gwajima hakina uhusiano na spinning doctoring labda ungekuja na uzi kuelezea hiyo "spinning doctoring" Gwajima ameropoka kama ambavyo ni kawaida yake na kama ambavyo magazeti bongo pia huropoka naye sasa sijui tunayaitaje labda spinning nursing.
 
Mimi napenda sana matukio anayoyafanya Gwajima!, ninakoendelea namuomba Mungu anipe nguvu nitende zaidi ya Gwajima. Ha ha haaaah! ila sio matukio yanayohusu wake za watu. Eeeh Mungu nisaidie nifike huko, Mungu asipoulinda mji walindao wakesha bure. (POLICE walikesha bure kwa kumsubiri Gwajima atoke nje wamkamate!)
 
Kipi unakijua katika ujasusi ndugu, umetajwa tu na kukurupuka mkuu
Ndiyo maana nikasema tatizo lako unajenga hoja kwa kutumia hisia.

Mambo ya kusema nimetajwa na kukurupuka ndiyo hisia zenyewe. Kwani kwenye andiko lako umetaja jina la Msemajiukweli?

Wewe hunifahamu lakini unalazimisha hisia zako zinifahamu.

Mimi kutokujua ujasusi haina maana kuwa wewe ndiyo utakuwa unajua ujasusi.

Kwenye masuala yanayohitaji specialization jifunze kufatuta tafiti katika kujenga hoja kama hukupata nafasi ya kusomea eneo hilo.

Tafiti siyo udaku na udaku hauwezi kusimama kwenye ukweli.
 
Yap tunawahitaji akina Gwajima kumi hivi ili Taifa hili lilaaniwe kabisa kwa 100% mkuu!
Wafuasi kama wa Joseph Kibweteere ambaye alikuwa kiongozi wa Movement for the Restoration of the Ten Commandments of God bado ni wengi sana katika dunia hii!

Unaweza kufanya chochote au kukubaliana na chochote kwa sababu kimesemwa na mtu wa aina ya Joseph Kibweteere!
 
Back
Top Bottom