Tanzania inamhitaji 'Mwamba' ili kifikia malengo ya kuwa huru!!

Kwa heshima na taadhima niwasalimu wanajamvi!
Kwa miaka kadhaa baada na kabla ya uhuru nchi yetu ilijidai kuwa ni nchi ya waungwana sana ...na matokeo yake sitaki kuyasimulia kwa kuwa kila mmoja wetu anayajua.

Timepata uhuru bila kumwaga damu hili ni jambo jema sana lakini limetufanya kuwa wapole sana na hivyo uhuru wetu bado haujatatua matatizo yetu ya msingi kwani bado walami wametushikilia vilivyo.

Walami wametushika kwa kuwa sisi ni waungwana sana...kinadharia...

Napenda kusema kuwa sisi sio legelege pamoja na uungwana wetu we are very aggressive,intellectual masculine,strong n.k lakini tuliamua kuwa tulivyo bila sababu ya msingi.

Tumeonewa sana na dunia hii kwa kuwa tulitumia approach ya uungwana/unyonge na uleiza fea.

Sasa ni wakati wa mabadiliko ya kweli(achana na na yale mabadiliko ya kuzungusha mikono)

Dunia iliyoendelea haikuwahi kuwa wanyonge ...dunia iliyoendelea iliendelea baada ya ubabe na umwamba...historia niliyoanayo inaniambia hivyo....
Kwa maoni yangu ubabe na umwamba ni kipengele muhimu katika kufikia maendeleo ya kweli na aghalabu yale yanayohesibika kuwa ni maendeleo.

Israel,Marekani ,China n.k wamefika hapo walipofika kimwamba/kibabe na sio kilegevu.

Hii ni imani yangu kutokana na historia niliyoisoma na uzoefu wa kimaisha..

Mwamba anayeweza kumuangusha Mwamba ndiye hupewa sifa !! toka enzi na enzi!

Hoja yangu ni moja tu...Tanzania ilikuwa nyonge sana despite having miamba.sasa ni wakati wetu wa kuonesha dunia kuwa sisi ndio Taifa teule la Mungu.

Viongozi wetu wanatakiwa wawe mfano wa miamba ili mwenyezi Mungu ajenge juu ya miamba hiyo.

Wito wangu kwa viongozi wote na wananchi wote ...tuwe miamba ili Mwenyezi Mungu ajenge kanisa (utawala wake) kwenye miamba hiyo.

Simon Petro aliambiwa wewe ni Mwamba na juu ya mwamba ule kanisa(utawala) lake litajengwa.

JINGALAO NITAENDELEA KUWA MWAMBA WA MABADILIKO TANZANIA NA JF !!!


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!!
Hata siku moja huwezi kuwa huku ukiwapigia magoti 'Mabeberu' wakukopeshe Fedha.

Hakuna mdaiwa HURU hata nukta moja, kwani wakati wote anawaza madeni tu. Na huwezi kuwa HURU kwa kuishi kwa uongo, tenq kibaya zaid unaowadanganya ndio unawategemea wakupe huo UHURU, huwezi kuwa HURU kwa ubaguzi wa wazi wazi.
 
Hata siku moja huwezi kuwa huku ukiwapigia magoti 'Mabeberu' wakukopeshe Fedha.

Hakuna mdaiwa HURU hata nukta moja, kwani wakati wote anawaza madeni tu. Na huwezi kuwa HURU kwa kuishi kwa uongo, tenq kibaya zaid unaowadanganya ndio unawategemea wakupe huo UHURU, huwezi kuwa HURU kwa ubaguzi wa wazi wazi.
USA ni huru na inadaiwa
 
Back
Top Bottom