Tanzania inahitaji Upinzani wenye nguvu na wa uhakika awamu ya tano

KILIVITE

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
1,302
555
Kama kuna wakati ambao Tanzania inahitaji "Upinzani wenye nguvu na wa uhakika" basi ni wakati huu wa awamu ya tano.Ukitafakari kwa makini utaona dalili za wazi za JPJM pamoja na Serikali yake kuanza kuelekea kuvuka mstari wa demokrasia na kuukaribia mstari wa Udikteta (Imla).Dalili hizi ni;

1.Mgawanyo tata wa madaraka

2.Suala la Zanzibar

3.Kutotambua thamani ya upinzani na wapinzani kwa kuwabeza,kuwabambikia makosa,kuwapiga na kuwadhalilisha mbele ya jamii

4.Mzio (Aleji )ya kukosolewa na watu wa chama na nje ya chama.

5.Kukosekana kwa mzania wa uangalizi (Checks and balances)

6.Haki kugeuzwa kuwa upendeleo

7.Maamuzi ya kukurupuka (Unplanned decisions)

8.Teuzi za wana usalama (Polisi na Wanajeshi) wastaafu kuongeza jamii

9.Maagizo yaliyojaa maswali mengi pasipo ufafanuzi

10.Lugha isiyopendeza yenye dalili ya kuwabagua Watanzania kwa misingi ya vyama.
 
Hujui kuwa upinzani umeimarika zaidi siku za hivi karibuni? Angalia uwepo wa mawaziri wakuu wa zamani (2), katibu mkuu mpya mwenye uwezo mkubwa wa kuratibu migomo hatari zaidi (Dr. Mashinji wa CDM) na mapumziko ya maalim katika hoteli ya kifahari zaidi nchini. Mungu atoe nini zaidi kwa upinzani huu?
 
Back
Top Bottom