Ndugu,bila siasa fika hata mlimani ujionee. Kuna kitu kinanishangaza,wanachuo wengine walipewa hela kidogo kwa ajili ya mwanzo wa semesta kujikimu,kiasi ambacho wengi walikitumia kujazia %ya karo. Wakiwa wamesubiri sehemu ya pili ya posho,tayari wako hoi jamani. Nimesikitishwa na wanachuo hao ambao baadhi wanaosoma mbali kama faculty ya habari na utangazaji iliyo nje ya main campus,yan Mikocheni ,wameshindwa kwenda na kurudi hostel za mabibo na main compus,wengi wao wameamua kukaa hostel bila kwenda lecturers kwa kusubiri wapate boom la pili waweze pata nauli. Hawa akina dada watakwepa kweli vishawishi? Serikali inafikiriaje kuwa na HESLB mbovu ivi? Jamani ndugu zangu,Tanzania tunajenga taifa la watu wa baadae watakaokuja kuwa wachungu sana. Ndani ya miaka 3 ijayo,nchi itakuwa na wasomi walionyeka vya kutosha na cjui serikali hii itapitia mlango upi. Kama hali hii ipo Udsm,je vyuo vilivyo nje ya dar vina hali gani?