Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Kwa Tanzania kinacholeta mkanganyiko wa kutopungua umasikini wakati ambapo uchumi unakua ni kwamba ukuaji wa uchumi haujagusa sekta kiongozi ya kilimo. Sekta hii inayoimbwa kila siku kuwa ndio uti wa mgongo wa taifa letu, Licha ya sekta ya kilimo kuchangia kiasi cha asilimia 45 ya pato la taifa, asilimia 85 ya mauzo ya nje na kuajili asilimia 80 ya watanzania wote, ukuaji wa sekta hii umezorota kwa kipindi cha miaka ya karibuni. Mfano sekta hii ilikua kwa asilimia 5.5 mwaka 2001, mwaka 2002 asilimia 5.0, mwaka 2003 asilimia 4.0, mwaka 2004 asilimia 3.8, mwaka 2005 asilimia 3.7, mwaka 2006 asilimia 3.5, mwaka 2006-2015 ikakua kwa asilimia 5.01 tu.
Hii inaonyesha kwamba vipato vya asilimia 80 ya waajiriwa wa sekta hii vimekuwa duni kwa miaka hiyo, hivyo kutia shaka kama umasikini unaweza kupungua miongoni mwa watu hao. Sekta iliyokua kwa kasi ni ya madini ambayo inaonyesha kwamba imekua toka asilimia 13.5 mwaka 2001 hadi asilimia 15.0 mwaka 2002, asilimia 17.0 mwaka 2003 na asimilia 21.01 mwaka 2003-2015.
Sekta hii ni mpya na imekuwa ikipata wawekezaji wengi kwa haraka sana. Tatizo kubwa la sekta kama ya madini na nishati hasa katika nchi za Afrika ambazo husafirisha madini ghafi ni kwamba haizalishi ajira zinazoweza kupunguza umasikini kwa kasi sambamba na ukuaji wa uchumi.
Hii inatokana na ukweli kwamba madini ghafi husafirishwa nje ya nchi na kukatwa katika maumbo mbalimbali tayari kwa uuzaji. Hivyo sekta hii haina uhusiano wa karibu na sekta ya viwanda katika nchi zinazo zalisha na kusafirisha madini ghafi. Pili ajira inayozalishwa ni ndogo kutokana na matumizi ya mashine katika uzalishaji wa madini hayo.
Hali ya ardhi yetu si mbaya na njia pekee itakayo harakisha kupungua kwa umasikini wetu pamoja na kuongeza thamani ya madini ni kuwekeza katika kilimo. Fedha zinazopatika katika madini ziwekezwe katika kilimo ilikuwasaidia asilimia 80 ya watanzani walioajiliwa katika sekta hii. Hii ni changamoto kubwa kwa Tanzania kufikia malengo ya milenia ya kupunguza idadi ya watu wanaoishi katika umuasikini wa kupindukia ifikapo mwaka 2030.
Ili malengo ya timie inatakiwa uchumi ukue kwa wastani wa asilimia 3.8 hadi 4.5 kwa mwaka, mpaka ifikapo 2030. Nimuhimu kutilia mkazo elimu itakayo wawezesha watu kujiajiri wenyewe kwani hii ni njia rahisi ambayo inaweza kumkwamua mtu katika umasikini. Bila shaka nchi nyingi za Asia ya Mashariki ambazo tunapenda kuiga namna zilivyoweza kukua kiuchumi kwa kasi ya ajabu ni kwamba ziliweza kuua ndege wengi kwa jiwe moja mfano, ukuaji wa pato la kila mwananchi kwa wastani ulikua kwa kasi ya kutisha, wastani wa umri wa kuishi uliongezeka, kuongeza kasi ya elimu na upunguzaji wa umasikini kwa kasi.
Waliweza kufanya hayo bila kufuata TORATI walizopewa na mabwana wa IMF na Benki ya Dunia. Walitilia mkazo elimu ya ufundi, utafiti na uwekezaji katika teknolojia sahihi. Ukuaji wa uchumi ambao hauwezi kubadili maisha ya watu masikini hautakuwa na mafaa yoyote. Utakuwa ni ukuaji wa uchumi kitakwimu zaidi kuliko kuleta maisha bora ya watu.
Hayo ndiyo tumekuwa tukishuhudia zaidi katika nchi nyingi za kiafrika na Latini Amerika ambapo takwimu huonyesha kuwa uchumi unapanda kwa kasi nzuri, lakini ukweli ni kwamba ukiingia kwenye nyumba ya mtu wa kawaida kunawaka moto. Ukuaji wanamna hiyo wa uchumi hunufaisha kundi dogo la jamii na kujikita katika ukuaji wa vitu vichache ambavyo huwa nafaida ndogo kwa jamii kubwa.
Mfano: Sekta ya madini ikikua kwa faida kubwa ya mwekezaji, haitakuwa na maana kama watanzania hawafaidi matunda yake. Badala yake tunapewa viini macho vya wawekezaji kwa kujengewa shule na zahanati ambazo maranyingi huwa na lengo la kuwaduwaza wanavijiji na wanaotembelea migodi hiyo. Kinachotakiwa ni maendelo ya kweli yatakayoletwa na ukuaji wa sekta hii kwa maana ya kodi za kutosha na gawio linaloonekana. Tusizugwe na wanayoipa jina la misaada ya milioni 200 kwa kupoteza matrilioni ya fedha zetu za madini na ajira ambazo kwakukata madini hapa nchini tungezipata. Kwaujumla ukuaji wa uchumi haujapunguza makali ya maisha ya watanzania walio wengi
Katika moja ya masimulizi ya kale yenye kuelezea mageuzi ya China toka kwenye lindi la ujamaa mufu mpaka ujamaa wa kimapinduzi ya kiuchumi, Masimulizi yaliyo kwenye makumbusho ya Szechuan yanasomeka kuwa ni matajiri 8 tu ndio walioibadili China mpaka kuja ilipo sasa.
Ni taifa gani duniani lililoendelea bila mabilionea? bila mafisadi? bila mamafia wa ukwasi? bila WEZI?
Naamini tatizo Tanzania ni mfumo wa hawa waitwao "wakwasi" ndio unaoliyumbisha taifa, ni vigumu kuwaondoa, Kitendo cha kujaribu kuwaondoa ni kuliangusha taifa katika mgogoro wa kiuchumi, lakini tunaweza kupunguza kasi yao na kuwaombia wabadili mfumo wao wa ukwasi.
Mfano nchi ya Marekani mabebari hawa wanapiga (wanaiba) sana hela nje ya nchi na wanalipa kodi kwa wingi ndani ya nchi yao. vivyo hivyo ufaransa, Urusi, Uchina, Uingereza na Japan. Lakini Tanzania ni matajiri wangapi biashara zao ni halali na wanalipa kodi stahiki?
Tangu nchi yetu ifuzu kujiunga na kikundi cha nchi tegemezi zinazotembeza bakuli kila kukicha mwaka 1997 baada ya kuifurahisha Benki ya Dunia (WB) na Shirika la fedha la Kimataifa (IMF) juu yauzingatiaji wa TORATI ya mashirika hayo mumiani, zaidi ya watanzania 50% ni masikini wa kutupwa wanaoishi chini ya mstari wa umasikini (Poverty line) kwa matumizi chini ya Tsh 260 kwa siku, asilimia 36% ni masikini sana, Wakati watanzania asilimia 14% ni matajiri wa kupindukia wanaoishi maisha ya anasa, wakimiliki mahekalu, magari ya kifahari na ya gharama kubwa na watoto wao kusoma shule za sifa ya kimataifa. Hawa ndio wanaodhibiti uchumi na siasa ya nchi hii kwa gharama ya watanzania asilimia 86 walio nje ya kundi hili.