Umenena.
Waalim nnaowakumbuka, enzi hizo (60s) walikuwa ni watu wenye heshima kubwa kwa jamii.
70s baada ya kuukumbatia ujamaa, waalim wa maana wakahama nchi, wakapewa nyadhifa zingine serikalini, wakastaafu kwani viwango vya elimu vilishuka ghafla. Matokeo ni haya tunayoyaona, waalim wamekuwa ni kundi la wanafunzi wanaofeli, hivi umefeli masomo yote unakwenda kufundisha nini?
Njia pekee ya kuinua elimu ni kuwajali waalim, kwanza kwa kuhakikisha wanalipwa mishahara ya juu, marupurupu ya juu, na serikali ihakikishe inawahamasiha wanaofanya vizuri masomoni wachukue nyadhifa za ualimu, huwapati kwa mishahara hii ya sasa.
Na hakuna nchi itayoendelea kama haina waalim wazuri. Mwalim mbovu unategemea mwanafunzi aweje?