katika kipindi cha BBC kilichorushwa jana jioni (20-02-2012), kuna taarifa ya kuwa Tanzania imewekwa katika orodha ya BLACKLIST na hivyo HAIKOPESHEKI, NA UWEKEZAJI NI MGUMU. Kwa maelezo yaliyotolewa ni kwamba nchi ikifikia kuwekwa katika BLACKLIST ina maana ni ngumu kwa nchi wahisani kuikopesha Tanzania kwa hofu ya kutolipwa deni, na pia Wawekezaji wataogopa kuwekeza Tanzania kwa hofu ya kibiashara.
Tanzania inafikia hatua ya kuingia katika orodha ya BLACKLIST kutokana na kukithiri kwa matumizi ya PESA CHAFU (MONEY LAUNDARING) ambazo husababishwa na kukithiri upatikanaji na matumizi ya pesa Haramu.
Je, wadau uchumi wetu miaka mitatu ijayo tutakuwa wapi???
Au ndio Tanzania nayo inakaribia kutangazwa imefilisika?
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!