wakuu za jioni, mi nina swali nmeshindwa pa kuliweka zaidi ya humu naomba msipondee bana am serious nilimpenda kwelikweli afu sijui pa kumpatia, hivi yule binti alieimba ule wimbo wa
Tanzania eeh
Nakupenda eeh
Nchi yangu eeh,
nmesahau lyrics nakumbuka hiyo half chorus, ila kalikuwa katoto walikuwa wanakaonyesha kwenye kipindi cha watoto wetu itv miaka ile yule eddy anatangaza 1999/ 1998 hivi kama sijakosea.
video yake kuna miti inakatwa katwa wazungu wanamvalisha headphones kana dimples she was so young so so cute, she had an amazing voice, basi mi nikapanga nkikua nimtokee bana.
Sasa shida kubwa ni sijawai msikia tena mazee hata wimbo wake mwingine, video yake nimeisearch google kwa title ya ule wimbo nimjue basi hata jina nimtafute facebook, holaa, nmeulizia raia kibao hawana habari, sasa basi humu jamvini kwa aliye na ufahamu of her whereabouts anijuze kama yu hai au alishakufa au wazungu walishambinafsisha.
au pia kama umekuwa sasa upo JF unaisoma hii thread ni PM basi.